Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mtu anaweza kupata ikiwa homoni ya estrogen imeongezeka, hizi dalili zikitokea mama anapaswa kuwahi hospital ili kuweza kupata matibabu au ushauri zaidi.
1. Dalili ya kwanza ni tumbo kujaa gesi.
Kwa kawaida tumbo kujaa gesi ni kitu cha Kawaida kwa sababu ya kuwepo kwa magonjwa mbalimbali kwa hiyo ikitokea tumbo likajaa gesi, likakaza au kuvimba ni vizuri kabisa kuwahi hospital kwa ajili ya. Uangalizi zaidi.
2. Kuongezeka uzito wa ghafla.
Kuna wakati mwingine mama anaweza kuongezeka uzito kwa ghafla si kwa sababu ya kwamba ni afya ila ni kwa ajili ya kuwepo kwa ongezeko la homoni ya estrogen.
3. Mabadiliko ya hisia ya mara kwa mara au kwa kitaalamu huitwa mood change
Kuna kawaida Kuna kipindi mtu anahisi kuwa na hasira au kuwa na furaha yaani Kuna mabadiliko mengi kwa mtu utokea kwa hiyo Mama akifikia wakati wa manopause na akaona Dalili kama hizi ni vizuri kabisa kuwahi hospital kwa matibabu zaidi.
4. Kuwepo kwa wasiwasi na msongo wa mawazo kwa kitaalamu huitwa anxiet.
Kuna kipindi Mama huwa na wasi wasi hata kwa kitu au vitu vidogo kwa kufanya hivyo ni sababu ya homoni kubadilika.
5. Kukosa usingizi.
Kuna wakati mwingine usingizi unakosa kabisa kwa hiyo sio kusema kwamba ni uchawa au vipi ila ni dalili za ongezeko la homoni ya estrogen.
6. Kuwepo kwa vipele vyekundu usoni.
Kuna wakati mwingine mama anakuwa na vipele vyekundu usoni, hali hii haiwatokei watu wengi ila ni kwa akina Mama Wachache.
7. Kuota kwa vinyama kwenye via vya uzazi .
Kuna wakati mwingine kunakuwepo kwa vinyama kwenye via vya uzazi hali hii inatokea lakini si kwa wanawake wengi.
8. Kuvimba kwa maziwa.
Kuna kipindi ambapo Mama anaweza kumaliza miaka mingi amenyonyesha lakini kwa sababu ya kuwepo kwa ongezeko la homoni mwilini usababisha maziwa kuvimba hali ambayo usababisha wasiwasi mwingi kwa akina Mama walio wengi.
9. Utokaji mwingi wa damu wakati wa hedhi kwa kiasi ambacho si kawaida na siku nyingine.
10. Maumivu ya kichwa ya mara Kwa mara.
Kuna wakati mwingine mama uhisi maumivu ya kichwa yasiyo ya kawaida kila mara hata akitumia dawa hali ni Ile Ile tu.
11. Kupoteza kumbukumbu na kuongezeka kwa uzito.
Kuna wakati mwingine mama anaongezeka Uzito ghafla na kuambatana na kupoteza kumbukumbu .
12. Pamoja na Dalili tulizoziona si kila dalili ni matatizo ya homoni kuongezeka ila ni vizuri kabisa kwenda hospital kwa ajili ya uangalizi zaidi na kupata ushauri wa daktari
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii itakwenda kukuletea orodha ya vyakla vinavyoaminika kuongeza nguvu za kiume.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa maji yaliyomo kwenye mfuko wa mtoto akiwa tumboni. Ni maji ambayo kwa kitaalamu huitwa (Amniotic fluid)
Soma Zaidi...Kuna uwezekano una ujauzito ila hujajijuwa, huwenda hujapata dalili zozote. Unataka kujuwa kama una ujauzito baada ya tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kuziba kwa mrija wa kizazi ambayo kwa kitaalamu huitwa follapian tube, ni sababu ambazo ufanya mirija ya follapian tube kuziba.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mapendekezo muhimu kwa wajawazito, haya ni mapendekezo yaliyotolewa na wataalamu wa afya ili wajawazito waweze kule mimba zao vizuri na kuweza kujifungua vizuri na kupata watoto wenye afya njema na makuzi mazuri pasipokuwepo na ule
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za kujifungua hatua kwa hatua
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza njia za kuhakiki Kama u-mjamzito
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi sababu za ugumba kwa Mwanaume, ni sababu ambazo umfanye mwanaume ashindwe kumpatia mwanamke mimba.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukupa sababu zinazoweza kupelekea uke kuwa mkavu yaani kukosa majimaji wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Soma Zaidi...