UMUHIMU WA UCHUMI KATIKA UISLAMU


image


Post hii itakufundisha faida na umuhimu wa kijenga uchumi katika jamii ya kiislamu.


2. Umuhimu wa uchumi katika Uislamu
Mwanaadamu ameumbwa na mahitajio mengi ambayo hana budi kuyapata ili aweze kuishi kwa furaha na amani hapa ulimwenguni. Kwa kuwa mwanaadamu ni mchanganyiko wa mwili na roho, pia mahitajio yake yamegawanyika, ana mahitajio ya kiroho na kimwili. Mahitajio ya kiroho ambayo humuwezesha mwanaadamu kuishi maisha ya utulivu yenye furaha na amani, hupatikana kwa kufuata kwa utii na unyenyekevu mwongozo wa Allah (s.w).

 


Mahitajio ya kimwili kama vile chakula, mavazi, vipando na njia ya uchumi hupatikana kwa kuchapakazi chini ya mazingira yatokanayo na itikadi sahihi yenye kusimamiwa na viongozi wanaozingatia haki itokayo kwa Muumba. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Allah (s.w) amejaalia mali anayoichuma mwanaadamu iwe ndiyo inayoboresha maisha yake: “Wala msiw ape w apumbavu mali zenu ambazo Mw enyezi Mungu amezijaalia kwa ajili ya maisha yenu …” (4:5)

 

Kutokana na aya hii, kuchuma mali si jambo la hiari kwa mwanaadamu kwani kwa namna Allah (s.w) alivyokadiria, maisha ya mwanaadamu kwa hapa ulimwenguni hayawezekani pasi na kuchuma. Ni kweli kwamba vitu vyote vilivyomzunguka mwanaadamu katika ulimwengu huu vimeumbwa kwa ajili yake kwa ushahidi wa Qur-an: “Yeye ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi…” (2:29).

 


Lakini mara nyingi vitu hivi haviko katika hali ya kutumiwa na mwanaadamu moja kwa moja. Bali mwanaadamu analazimika kutumia elimu yake, Maarifa yake, juhudi zake na vipawa vyake vingine ili ayabadilishe mazingira yake yaweze kumtumikia na kukidhi haja zake.
Kwa mtazamo huu Uislamu unatuamrisha kuchuma kama unavyotuamrisha kusimamisha Swala, kutoa Zakat na kutekeleza Ibada nyingine maalumu kama hizi:

 

Na itakapokwisha swala, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi, ili mpate kufaulu. (62:10)
Tunajifunza kutokana na aya hii kuwa, kuchuma ni wajibu unaompasa Muislamu mara tu baada ya kutekeleza Ibada maalum. Hili linabainishwa katika Hadithi ifuatayo:
“Abdullah bin Mus ’ud ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Kutafuta chumo la halali ni faradhi baada ya kutekeleza faradhi nyingine.” (Baihaqi).
Pia Mtume (s.a.w) amebainisha wazi ubora wa kujizatiti katika kutafuta chumo la halali kwenye Hadith ifuatayo:

 


“Miqdam bin Ma ’ad Yakrab ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Hapana mmoja wenu aliyekula chakula kizuri kuliko kile alichokula kutokana na kazi ya mkono wake mwenyewe. Na Daud, Mtume wa Allah, alikuwa anakula kutokana na kazi ya mikono yake.” (Bukhari)

 


Kwa upande mwingine Uislamu unalaani uvivu na kuwategemea wengine pasi na sababu au dharura maalum kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:
“Jubair bin Awam ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Mmoja wenu kuchukua kamba na kisha akaja na mzigo wa kuni akiwa amebeba mgongoni mwake na akauuza, na kwakufanya hivyo Allah akailinda hadhi yake, ni bora kwake kuliko kuomba omba watu, wakimpa chochote au wasimpe (Bukhari.)

 


Mpaka hapo tumejifunza kuwa kwa mtazamo wa Uislamu, uchumi ndio msingi wa maisha ya mwanadamu hapa ulimwenguni na Uislamu umewajibisha kuchuma kwa kila mwenye uwezo. Ni makosa katika Uislamu mtu mwenye uwezo na afya kubweteka na kuwategemea wengine katika kukidhi mahitaji yake.

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    3 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    5 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    6 Maktaba ya vitabu    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Taratibi za malezi ya watoto wadogo baada ya talaka katika uislamu
Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi? Soma Zaidi...

image Njia haramu za uchumi.
Njia hizi ni haramu katika kukuza uchumi wako. Soma Zaidi...

image Jinsi ya kuswali kuswali swala ya maiti
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya maiti, nguzo za swala ya maiti, sharti za swwla ya maiti na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...

image Sifa nyingine za kuchaguwa mchumba ambazo watu wengi hawazijui
Hizi ni sifa za ziada za mchumba katika uislamu. Sifa hizi wengi hawazijui ama hawazingatii. Soma Zaidi...

image Jinsi ya kujitwaharisha Najisi hafifu na najisi ndogo
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi hafifu na najisi ndogo. Soma Zaidi...

image Jinsi ambavyo mgonjwa anatakiwa aswali
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ambavyo mgonjwa anatakiwa aswali kulingana na ugonjwa wake. Soma Zaidi...

image Jinsi ya kushona sanda ya maiti na kumvisha yaani kumkafini
Hapa utajifunza taratibu za kumkafini maiti wa kiislamu. Yaani kushona sanda yake na kumvisha. Soma Zaidi...

image Jinsi ya kumuandaa maiti baada ya kufa
Haya ni maandalizi ya kumuandaa maiti baada ya kufariki. Soma Zaidi...

image Swala ya idil fitir na idil haji nanjinsi ya kuziswali
Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya idil haji na swala ya idil fitir Soma Zaidi...

image Swala ya witiri na faida zake, na jinsi ya kuiswali
Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya witiri na faida zake kwa mwenye kuiswali. Soma Zaidi...