Navigation Menu



image

Mgawanyiko katika kuitumia mali unayomiliki

Unajuwa namna ambavyo matumizi ya mali yako, yanavyogawanywa? Jifunze hapa mgawanyiko wa mali yako.

6. Mgawanyo wa mali katika Uislamu

Uislamu unasisitiza kuwa zaidi ya kuchuma, kumiliki na kusambaza mali, mgawanyo pia uwe wa haki katika jamii ili kujenga udugu, amani na utulivu wa kweli. Na katika kuhakikisha hilo mfumo wa uchumi wa Kiislamu (Iqtisad) unatumia njia zifu atazo:

 


1. Zakat
(i)Kilugha, neno zakat lina maana mbili: (a) Utakaso na (b) Ustawi. Hivyo zaka ni Ibada inayochangia sana katika kuleta uadilifu na ustawi wa jamii kiuchumi na hata kisiasa.

 


(ii)Zakat katika Uislamu ni taasisi maalumu na imesisitizwa katika Qur-an. Aya zipatazo 80 zimeitaja Zakat pamoja na Swala Zakat ina upeo mpana sana na ina husisha vipengele vingi kama vile:

 

(a)Kijamii – Zakat ni kama bima ya jamii inayowahakikishia wakazi hifadhi ya kiuchumi endapo watapata matatizo kama ya umaskini au maafa. Zaka pia huondosha chuki na migogoro ya kitabaka na kujenga hisia za kuwa wamoja.

 


(b)Kisaikilojia, Zakat inawalea watu katika moyo wa kuhurumiana na kusaidiana. Inawapa wanyonge na masikini moyo wa kujiamini na kujiona sawa na wengine.

 


(c)Kiuchumi – Zakat ni njia mojawapo ya kupambana na tatizo la umaskini. Tatizo hili linazikabili nchi zote na Uislamu unalenga katika kuondoa umaskini pasi na jitihada za watu binafsi. Uislamu haupiganii usawa bandia na kuwa kipato cha kila mtu kiwe sawa na mwingine wala Uislamu hauinyamazii hali ya wengine watumie na kusaza wakati wengine wanaendelea kutaabika kwa kushindwa kujipatia mahitaji muhimu. Tofauti za kimapato, vipaji na uwezo zitakuwepo katika jamii, lakini pengo la tofauti hiyo lisiwe kubwa sana.

 


(d)Kwa maumbile yake, Zakat huwahimiza watu kuweka vitega uchumi na kuzalisha mali na kupiga vita tabia ya kuhodhi mali. Hii ni kwa sababu Zakat hutozwa kwa kipato kilichokaa mwaka mzima bila kutumika.Kila mtu hanabudi kupata mahitaji ya msingi.

 


2. Sadakat
Hisia za kuhurumiana na moyo wa kusaidiana kama ndugu zinazomsukuma mtu kutoa Zakat kwa kutaraji kupata radhi za Allah ndizo hizo hizo zinazomsukuma mtu kutoa sadaka. Hivyo tofauti kati ya Zakat na sadaka haipo katika lengo la kutoa bali katika wajibu wa kutoa. Zakat ni wajibu kutoa na sadaka ni amali iliyokokotezwa sana japo haikuwekewa kiwango na muda wa kutoa. Hutolewa kulingana na haja. Misingi ya kutoa sadaka ni ile ile ya kuhurumiana na kusaidiana kama Allah alivyoagiza katika Q u r ’an:

 

Na saidianeni katika wema na ucha-Mungu, wala msisaidiane katika dhambi na uadui” (5:2).

 

Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyotoa mashuke saba; ikawa katika kila shuke pana punje mia., Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaa mkubwa na Mwenye kujua.” (2:261).

 


Aidha, Mtume (s.a.w.) amesisitiza katika Hadithi nyingi sana umuhimu wa kutoa sadaka. Katika Hadithi iliyosimuliwa na Bukhari, Muslim, Ahmad na At-Tirmidh, Mtume (s.a.w.) amesema mtu asiyewahurumia watu hatahurumiwa na Allah. Na katika Hadithi iliyosimuliwa na Attabarani na Baihaqi, Mtume (s.a.w.) amesema: Naapa kwa Allah si muumini yule anayelala akiwa kashiba na ilhali jirani yake kalala na njaa.

 


Na katika Hadithi iliyosimuliwa na Al-Hakim, Mtume (s.a.w.) amesema ikiwa wakazi wa eneo fulani (kama vile mtaa) wakiamka asubuhi na ilhali mmoja wao ana njaa basi Allah hujitenga nao.

 


Matukio maalum ya kutolewa kwa sadaka
Baada ya kumaliza mfungo wa Ramadhani kutoa Zakatul Fitr ni lazima
. Zakatul Fitr kiwango chake ni kilo 2? za chakula kilichozoeleka katika mji huo kama vile mchele au ngano.

 


Na mtu hutoa kiasi hicho kwa ajili yake mwenyewe na hutoa tena kiasi hicho hicho kwa kila mtu anayemtegemea katika familia yake. Hivyo atamtoleo pia mkewe, na wanawe wote na wazazi wake iwapo anakaa nao na hawana uwezo.

 


Tukio la pili ni siku ya kuvuna mazao shambani, Mwenyezi Mungu ameagiza siku hiyo mtu atoe baadhi ya mazao yake na awape maskini, jamaa na majirani zake aliposema katika Qur’an:

 


Naye (Allah) ndiye aliyeumba m iti inayoegemezw a (katika chanja) katika kuota kwake na isiyoegemezwa na (akaumba) mitende na mimea ya matunda mbali mbali, na (akaumba) mizaituni na mikomamanga inayofanana na isiyofanana. Kuleni matunda yake inapotoa matunda; na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake (kwa kuwapa maskini na jamaa na majirani na wengineo) Wala msitumie kw a fujo, hakika Yeye (Allah haw apendi w atumiao kw a fujo.” (6:141).

 


Tukio la tatu ni wakati wa ndoa, Kuoana ni jambo lililohimizwa sana katika Uislamu. Hivyo Uislamu unasisitiza kuwa watu wasaidiane sana katika jambo hili. Wanazuoni wengi wanasema kuwa iwapo mtu anao uwezo wa kuoa lakini hapa mwanzo anakabiliwa na matatizo ya kifedha Hazina ya serikali ya Kiislamu (Baitul Maal) itumike kumsaidia. Wakati wa Ukhalifa wa Umar vijana kama hao walikuwa wakisaidiwa. Katika kuonesha ubora wa ndoa Allah amesema:

 

Na waozeni wajane miongoni mwenu (waungwana) na walio wema katika watumwa wenu (wanaume) na wajakazi wenu, kama watakuwa mafakiri Allah ataw atajirisha katika fadhila zake; na Allah ni Mw enye wasaa” (24:32).

 


Tukio la nne ni iwapo mtu atapata wageni. Uislamu unamtaka mtu awakirimu wageni wake. Katika Hadithi iliyosimuliwa na Bukhari na Muslim, Mtume (s.a.w.) amesema: Yule anayemwamini Allah na siku ya mwisho awe mkarimu kwa wageni wake. Kwa mchana mmoja na usiku afanye takrima maalum. Kwa siku tatu zinazofuata afanye takrima ya kawaida na zaidi ya hapo ni sadaka ya hiari.

 


Tukio la tano ni wakati wa kugawa urithi, iwapo watakuwepo watu mafakiri wakati huo wa kugawa basi wapewe chochote, kwani Allah anasema: “Na wakati wa kugawanya wakihudhuria jamaa na mayatima na maskini, wapeni kitu katika hayo (mali ya urithi) na waambieni kauli njema.” (4:8).

 


Tukio la sita ni agizo la Allah la kusaidiana kwa hali mbali mbali hasa majirani.

 


Tukio la saba ni wakati wa uzazi. Kama ambavyo Uislamu unahimiza ndoa ndivyo pia unavyothamini malezi ya watoto. Kihistoria Uislamu ndio ulioanzisha utaratibu wa kutoa malipo fulani maalum kwa familia zenye watoto wachanga.

 


Hivi leo ziko baadhi ya serikali duniani ambazo hutoa msaada wa pesa kwa familia zenye watoto wachanga. Huko Canada kwa mfano upo utaratibu wa kutoa msaada wa pesa kwa kila mtoto aliyezaliwa na kama watoto wakifikia umri wa miaka 18 na bado wanasoma kiwango cha pesa wanachopewa huongezwa.

 

Utaratibu huu ulianza katika karne ya 7 wakati wa ukhalifa wa Umar. Umar alianzisha mfumo wa kutoa dirham 100 kwa kila mtoto aliyezaliwa na kiwango hicho kiliongezwa kadiri mtoto alivyokua. Hivyo mfumo wa kutoa ruzuku kwa familia ni moja ya sadaqa zitolewazo katika mfumo wa uchumi wa Kiislamu.

 


Sadaka wakati wa dharura
Katika Hadithi iliyosimuliwa na Bukhari na Muslim, Mtume (s.a.w.) aliwasifu sana Al-Afariyyin (watu wa ukoo wa Abu Musa). Akasema watu hao walipokuwa vitani au safarini na chakula kikapungua basi walikikusanya pamoja chakula chote kilichosalia na kukigawa tena sawa sawa miongoni mwao.

 


Au nchi ikiingia njaa - ilitokea njaa kubwa kwa mfano wakati wa Ukhalifa wa Umar. Alichokifanya ni kutoa taarifa kwa viongozi wa majimbo mbalimbali na kuwataka walete chakula cha ziada. Na kilipokuja alikigawa bila ya kujali cheo, madaraka au ukoo wa mtu bali kwa kujali mahitaji tu. Kwa bahati njema njaa hiyo ilikwisha mapema. Lakini miongoni mwa maneno aliyoyasema Umar ni kuwa lau njaa hiyo isingekwisha mapema, basi angewakusanya watu wote wenye njaa na angewagawa kwa familia zenye chakula. Akasema hii ni kwa sababu watu hawatakufa wakila chakula hata kama hawatashiba.

 


3. Kodi (Jizya)
Ni njia nyingine itumiwayo na Uislamu katika kuigawanya mali katika jamii. Tafauti na Zakat na Sadaqa ambazo hupasa kutolewa na Waislamu, Jizya hutolewa na wasiokuwa Waislamu (Dhimmi), wanaoishi chini ya dola ya Kiislamu, kwa ajili ya kupata hifadhi na huduma mba limb a li.

 

4. Mikopo
Mikopo kama njia mojawapo ya kugawa mali kwa watu wote, Uislamu unaruhusu watu kukopeshana. Mtu anaweza kumkopesha mwingine fedha ama kwa kutumia (matumizi ya kawaida katika maisha) au kwa kumsaidia mtaji kufanya biashara.

 






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1141


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Taratibu za ndoa ya kiislamu, hatua kwa hatua
Soma Zaidi...

NI ZIPI NGUZO NA SHARTI KUU ZA SWALA ILI IKUBALIWE
Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali. Soma Zaidi...

Hili ndilo hasa lengo la kuamrishwa kufunga
Soma Zaidi...

Njia haramu za uchumi
Soma Zaidi...

Jinsi ya kuelekea qibla katika swala.
Je unadhani ni kwa nini waislamu wanaelekea kibla, na jinsi gani utaweza kukipata kibla. Soma Zaidi...

Ijuwe ibada ya zaka na sadaka na namna ya kuitekeleza
Soma Zaidi...

Shahada nguzo ya kwanza ya uislamu, sifa zake na umuhimu wake.
Soma Zaidi...

darsa nzuri zenye kuelimisha hasa katika ndoa ya kiislam.
Assalaam alykum warahmatullah wabarakatuh. Soma Zaidi...

Maswali juu ya haki na uadilifu katika uislamu
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3:Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Nini maana ya kusimamisha swala?
Je kusimamisha swala kuna maana gani kwenye uislamu? Soma Zaidi...

JIFUNZE FIQH
Fahamu darsa mbalimbali za fiqh kama swala, twahara, zaka pamoja na funga. Zijuwe sharti za swala, funga na zaka. Soma Zaidi...

hizi ndizo sharti za swala
Soma Zaidi...