Mtoto wa tajiri na maskini (sehemu ya pili)

Post hii inahusu zaidi watoto wa wawili ambapo mmoja ni mtoto wa tajiri na mwingine ni mtoto wa maskini.

Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini.

1.basi hao watoto wakiendelea kukua na kusoma shule na kila mtu na ratiba yake mmoja ratiba yake ya maisha ya kitajiri na mwingine maisha yake ya umaskini, katika maisha ya mitihani shuleni mtoto wa tajiri alikuwa anakuwa wa kwanza kwa sababu waalimu walikuwa wanahongwa ela na mtoto wa maskini alikuwa anakuwa wa pili au wa tatu kwa kutumia akili zake,

 

2. Basi ikafika wakati wa mtihani wa mwisho yaani kumaliza darasa la Saba, wazazi wa mtoto wa tajiri wakapiga akili namna ya kumsaidia mtoto wao kwa sababu alikuwa kilaza, kwa hiyo walienda kwa familia ya mtoto maskini na kusonga Hela kubwa na  kishirikiana na waalimu kusudi mtoto wa tajiri akae karibu na mtoto wa maskini Ili wawe wanaonyeshana majibu, basi wale wazazi wakapewa Hela na yule mtoto wa maskini alihaidiwa kupewa laptop na simu kubwa baada ya kumaliza shule na yule mtoto alifurahi sana kusikia hivyo.

 

3. Na siku ya mtihani ikafika kwa sababu wale wazazi walikuwa na ela waliongea pia na msimamizi wa mtihani naye alikubali wakae wote kusudi wamwonyeshe majibu, basi mtihani ukaanza yule mtoto wa tajiri akakaa na mtoto wa maskini na akamwonyesha kila kitu na mtihani ukimalizika salama na pia matokeo yakatoka na kwa kuwa yule mtoto wa maskini alikuwa na akila sana alichaguliwa kwenye shule za vipaji maalumu na pia yule mtoto wa tajiri naye alichaguliwa kwenye shule za vipaji maalumu kwa sababu mtihani alifanyiwa na mtoto wa tajiri.

 

4. Basi matokeo yalipotoka yule baba tajiri alifurahi sana na akamwongezea yule mtoto wa maskini zawadi kubwa na akahaidi kumlipia karo ya mwaka wa form one, na siku zilifika za kwenda shule yule mtoto wa tajiri alikuwa na kila kitu kilichohitajika shuleni ila mtoto wa maskini alikuwa na karo aliyofadhiriwa nauli na madaftari, karamu na sabini pamoja na uniform, hali iliyomfanya kuridhika na alichonacho, kwa sababu safari ilikuwa ndefu mtoto wa maskini alifungiwa mhogho wa kula njiani na maji ila yule wa tajiri alifungiwa vitu vingi mno vya kula njiani.

 

Itaendelea

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jamvini Main: Burudani File: Download PDF Views 3342

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 web hosting    👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina   

Post zinazofanana:

Kila kitu ambacho wanaume wanatakiwa kufahamu kuhusu wanawake.

Hii ni siri kubwa kuhusu wanawake. Hapa utajifunza jinsi ya kumfanya mwanamke asikuache.

Soma Zaidi...
SAFARI YA MUUJIZA

Post hii inahusu hadithi moja iliyotokea Kwa mama mmoja mwenye familia ya watoto watano.ambapo mama aliolewa na mwanaume mwenye maambukizi ya virus vya ukimwi na kupata watoto bila maambukizi kusambaa kutoka Kwa baba kwenda Kwa mama.

Soma Zaidi...
Chemsha bongo na bongoclass

Jipime uwezo wako wa kufikiri pamoja nasi.

Soma Zaidi...
Ni nani kama mama

Nani kama mama? Hadithi hii itakufunza umuhimu wa kuwa muwazi kuhusu familia yako.

Soma Zaidi...
Hasara za wivu na kutokuwa wazi ( sehemu ya 2)

Posti hii inahusu zaidi hasara za wivu na kutokuwa wazi sehemu ya pili, sehemu hii inahusu mama Lisa anaenda kwa mama lina ili kuuliza kinachoendelea kwa mtoto wake , kwa hiyo tuona atapata jibu gani.

Soma Zaidi...
Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili

Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili,ambapo Mama yake na Jackie pamoja na jack wakiwa hospital na jack anaendelea kumwita Julius kila mara.

Soma Zaidi...
Hadithi ya Binti mfalme

Posti hii inahusu zaidi hadithi ya Binti mfalme ni hadithi ya kusisimua, kuhusu hadithi hii ni kwamba mfalme alihitaji mtoto wa kiume ila wanawake wote hawakumpata ila alitokea mke mdogo mmoja wa mfalme akajifungua watoto wawili mapacha mmoja wa kiume na

Soma Zaidi...
WAKATI WA KUFUMBUKA SEHEMU YA 1

Post hii inahusu zaidi hadithi mpya na nzuri inayoitwa wakati wa Kufumbuka, ni hadithi inayohusu maisha ya kawaida ambapo watu ushindwa kudhamini watu wa karibu nao na kuona watu wa mbali ndio wenye maana ila shida zikifika ndipo wanaona umuhimu wao.

Soma Zaidi...
NIMLAUMU NANI (sehemu ya nne)

Post hii inahusu zaidi kijana Frank anayelazimishwa kuolewa na Amisa yeye hayuko tayari ila kwa sababu ya maisha kuwa magumu anaamua kulala na Amina na kumbebesha Mimba ya watoto mapacha.

Soma Zaidi...
Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya tatu)

Post hii inahusu zaidi mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini wakipanda gari kuelekea shule kuanza maisha mapya.

Soma Zaidi...