Sunnah zinazoambatana na funga ya Ramadhani
Katika Mwezi wa Ramadhani kuna mambo kadhaa aliyoyafanya Mtume (s.a.w) na kutusisitiza nasi tuyafanye. Matendo haya ya Sunnah ambayo hurutubisha funga zetu na kutupelekea kufikia lengo la funga kwa ufanisi zaidi ni pamoja na:
(i) Kula na kuchelewesha Daku
Daku ni chakula kinacholiwa usiku wa manane kwa ajili ya kujiandaa kufunga siku inayofuatia. Kula daku ni sunnah iliyokokotezwa kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Anas (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: ... Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajir katika weusi wa usiku .. (2:187)
(ii) Kufuturu Mapema
Wakati wa kufuturu ni mara tu linapokuchwa jua kama tunavyofahamishwa katika Hadith:
Umar (r.a) ameeleza kuw a Mtume w a Allah amesema: Usiku unapoingia na mchana ukitoweka, na jua likitua, mtu aliyefunga atafungua.(Bukhari na Muslim).
Ni sunnah iliyokokotezwa kufanya haraka kufuturu mara tu linapokuchwa jua na kabla ya kuswali swala ya Magharibi kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:
Sahl (r.a) amesimulia kwamba Mtume wa Allah amesema: Watu w ataendelea kunawiri (kufanikiwa) pindi w atakuw a wanaharakisha kufuturu. (Bukhari na Muslim).
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Allah (s.w) amesema: Mpendwa zaidi kwangu kati ya waja wangu ni yule ambaye mw epesi kuliko w ote katika kufuturu. (Tirmidh).
Pia ni Sunnah kufuturu kwa Tende au kwa maji kwani tunajifunza katika Hadith kuwa Mtume (s.a.w) alifanya hivyo na akatuagizia tufanye h ivyo:
Anas (r.a) ameeleza kuwa mtume (s.a.w) alikuwa akifungua kwa Tende mbivu kabla ya kuswali (Magharibi), kama hizi hazikuwepo alifungua kw a Tende kavu, na kam a hizi hazikuw epo alikunyw a m afunda macha che y a m aji. (Tirm idh n a A bu Da ud).
Salman bin Amir (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Mmoja wenu atakapokuwa anafuturu, na afuturu kwa Tende kwa sababu ni baraka, kama hakupata Tende, na afuturu kwa maji, kwa sababu yametakasika (ni twahara). (Ibn Majah).
Vile vile ni sunnah wakati wa kufuturu kusoma dua ifuatayo: (Allahumma laka swumtu wa’alaariz-qika aftwar-tu)
“Ewe Mola! Nimefunga kwa ajili yako, na kwa riziki yako ninafuturu”. (Abu Daud).
Ni sunnah vile vile mtu kuzidisha dua anapokuwa katika swaumu kwani Mtume (s.a.w) amesema:
“Watu watatu dua yao hairejeshwi - aliyefunga mpaka afungue. Imamu muadilifu na mtu aliyedhulumiwa. ” (Tirmidh).
(iii)Kuzidisha Ukarimu
Pamoja na kuwa siku zote tumekokotezwa kuwakirimu na kuwasaidia wenzetu wenye shida mbalimbali, katika mwezi wa Ramadhani tunatakiwa tuzidishe. Mtume (s.a.w) alikuwa karimu zaidi katika mwezi wa Ramadhani, kuliko alivyokuwa katika miezi mingine kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Amesimulia Ibn Abbas (r.a) kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa ni mkarimu sana kuliko watu wote na alikuwa akizid is ha ukarimu wake katika mwezi wa Ramadhani wakati ambao Jibril (a.s) alikuwa akimjia. Jibril (a.s) alikuwa akikutana naye kila usiku wa Ramadhani mpaka mwisho wa mwezi. Mtume (s.a.w) alikuwa akisoma Qur-an mbele ya Jibril, na Jibril alipokutana naye alikuwa mwema (mkarimu) zaidi kuliko upepo wa kusi (wa mvua) (Bukhari).
Kufuturisha aliyefunga kumeahidiwa malipo makubwa kama tunavyojifunza katika hadith ifuatayo:
Zaidi bin Khalid(r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Atakayemfuturisha mtu aliyefunga, au atakayempa askari wa Allah zana za vita, kwake kuna malipo sawa na malipo ya mwenye kufunga au ya mpiganaji (bila wao kupunguziwa). (Baihaqi).
(iv)Kuzidisha kusoma Qur’an
Kusoma Qur’an kumesisitizwa nyakati zote kwani Qur’an ndio mwongozo pekee wa maisha wanaotakiwa Waumini wa kweli waufuate hatua kwa hatua katika kila kipengele cha maisha yao ya kila siku. Lakini, katika mwezi wa Ramadhani, ambamo Qur-an imeanza kushuka, tumesisitizwa kuzidisha kusoma Qur’an katika swala na nje ya swala angalau tuumalize msahafu mzima katika mwezi huu. katika Hadith tumejifunza kuwa, Mtume (s.a.w) alikuwa akisoma Qur-an mbele ya Jibril kwa mwezi mzima.Kuhusu kushuka Qur-an katika mwezi wa Ramadhani tunafahamishwa katika aya ifuatayo:
“Ni mw ezi wa Ram adhani ambamo imeteremshwa Qur-an ili iw e uongozi kwa watu na hoja zilizo wazi za uongozi na upambanuzi .. (2:185).
Ili Qur’an iwe mwongozo na kipambanuzi cha haki na batili, hatuna budi kuisoma kwa mazingatio na kwa hiyo ni muhimu kujua tafsiri ya yale tuyasomayo. Tukumbuke kuwa kusoma Qur’an bila ya mazingatio ni kama kuiangukia kwa uziwi na upofu, sifa ambayo waumini wa kweli wanatakiwa wajiepushe nayo. Kwani Allah (s.w) anatufahamisha kuwa miongoni mwa waja wake watakaofuzu ni pamoja:
“Na wale ambao wanapokumbushwa aya za Mola wao hawaziangukii kwa uziwi na upofu” (25:73).
(v)Kusimamisha Swala ya Usiku ya Tarawehe
Swala ya Tarawehe ambayo tumeshajifunza habari zake, ni miongoni mwa Sunnah zilizokokotezwa katika mwezi wa Ramadhani.
(vi)Kuutafuta usiku wa Lailatul-Qadr
Lailatul-Qadr au Usiku Wenye Cheo na Baraka ni usiku mmoja katika mwezi wa Ramadhani. Ni katika usiku huu Qur’an tukufu ilianza kushushwa kwa Mtume (s.a.w) kwa mara ya kwanza alipokuwa katika pango la mlima Hiraa (Jabal Hiraa). Aya za kwanza kumshukia Mtume (s.a.w) ni aya tano za mwanzo wa suratul-Alaq, sura ya 96 katika msahafu. Kuhusu kushuka Qur’an katika usiku huu tunafahamishwa katika Qur’an yenyewe:
“Kw a yakini Tumeteremsha (Qur-an) katika usiku uliobarikiw a. Bila shaka Sisi ni Waonyaji. ” (44:3).
“Hakika tumeiteremsha (Qur-an) katika Lailatul-Qadr (Usiku Wenye heshima kubwa)” (97:1).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 1357
Sponsored links
👉1
Kitabu cha Afya
👉2
Simulizi za Hadithi Audio
👉3
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4
kitabu cha Simulizi
👉5
Madrasa kiganjani
👉6
Kitau cha Fiqh
Namna ya kumvalisha sanda maiti, na kushona sanda ya maiti
Soma Zaidi...
Kutoa kati kwa kati
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
mambo gani ni haramu kwa mwenye damu ya Hedhi na nifasi (damu ya uzazi)
Soma Zaidi...
Aina 12 za swala za sunnah na idadi ya rakaa zake wakati wa usiku na mchana
Aina za Swala za Sunnah. Soma Zaidi...
Nini maana ya twahara katika uislamu
Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya twahara katika uislamu. Pia utakwenda kujifunza hukumu za twahara, aina za twahara na mambo mengineyo Soma Zaidi...
Funga ya ramadhan na nyinginezo
Nguzo za uislamu (EDK form 2; dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
NAMNA YA KUSWALI SEHEMU YA KWANZA
Mtume (s. Soma Zaidi...
Mambo yanayoharibu Udhu (yanayobatilisha udhu)
Post hii inakwenda kukufundisha mambo ambayo hubatilisha udhu yaani mam,boa mbayo yanaharibu udhu. Soma Zaidi...
maana ya Eda na aina zake
Ni kipindi au muda wa kungojea mwanamke aliyepewa talaka (aliyeachwa) au kufiwa na mumewe kabla ya kuolewa na mume mwingine. Soma Zaidi...
Jinsi ya kutoa zakat al fitiri na umuhimu wa zakat al fitri kwa waislamu
Hapa utajifunza kuhusu zakat al fitiri, kiwango chake, watu wanaostahili kupewa na kutoa, pia umuhimu wake katika jamii. Soma Zaidi...