Ni muda gani unatakiwa ufunge ramadhani, je kuandama kwa mwezi kwa kiona ama hata kusiki.
Kuonekana kwa mwezi wa Ramadhani
Swaumu ya Ramadhani inaanza kwa kuona mwezi baada ya siku ya 29 Shaaban au 30 Shaaban kama tunavyofahamshwa katika hadithi zifu atazo:
“Ibn Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Msifunge mpaka muuone mwezi umeandama na msiache kufunga mpaka muone mwezi (wa Shawwal) umeandama. Kama kuna mawingu (hukuuona) hesabu kamili (siku 30). Katika simulizi nyingine amesema: Mwezi una masiku 29, kwa hiyo usifunge mpaka uone mwezi umeandama kama kuna mawingu subiri na kamilisha idadi ya siku 30.”
(Bukhari na Muslim)
Kutokana na Hadithi hii ni wazi kuwa watu hawaruhusiwi kufunga kwa kufuata kalenda. Inabidi juhudi za kuuangalia mwezi ziwepo kwa umma wa Waislamu tangu mwanandamo wa Shaaban.
“Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuw a Mtume w a Allah ameagiza: Hesabu mwandamo wa Shaaban kwa ajili ya Ramadhani”. (Tirmidh).
Kwanini kufuata mwandamo wa mwezi?
Tunafunga kwa kuona mwezi kwa sababu ndivyo alivyotuamrisha Mtume wa Allah (s.w) kama tulivyojifunza kutokana na hadithi zilizonukuliwa hapo juu. Kumtii Mtume (s.a.w) ndio Uislamu. Rejea Qur-an katika aya zifuatazo:
“Sema: “Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkikengeuka (Allah atakuadhibuni) kwani Allah hawapendi makafiri.” (3:32)
“… Na anachokuleteeni Mtume, kipokeeni, na anachowakataza
kiacheni…” (59:7).
“Anayemtii Mtume, kwa yakini amemtii Mw enyezi Mungu…” (4:80)
Pia amri hii ina hekima yake. Mwaka unaohesabiwa kwa mwandamo wa mwezi una siku 354 kwani kwa wastani mwezi mmoja una siku 29?. Mwaka unaohesabiwa kwa kufuata jua, muda ambao dunia huchukua kulizunguka jua una siku 365, saa 5, dakika 48 na nukta 46. Kwa hiyo ukilinganisha mwaka wa hesabu ya mwezi na mwaka wa hesabu ya jua, utaona kuwa mwaka wa mwezi ni mfupi kwa siku10 hivi. Hivyo mwezi wa Ramadhani hurudi nyuma siku kumi katika kila mwaka ukilinganisha na mwaka wa jua. Hivyo basi, mtu yeyote atakayejaaliwa kufunga muda wa miaka 36 hatakuwa na siku au msimu katika mwaka ambao hakuufunga. Yaani atawahi kufunga siku zote za jua, za mvua, za upepo, za shwari, za kusi, za kaskazi na kadhalika. Kama ingelikuwa inafuatwa kalenda ya mwaka wa jua, wengine daima wangalifunga nyakati za joto tu, wengine nyakati za baridi tu, wengine nyakati za njaa tu, wengine nyakati za mavuno na kadhalika ilimuradi pasingalikuwa na mabadiliko.
Ni lazima kila mfungaji aone mwezi?
Mwezi wa Ramadhani akiona mtu mmoja muadilifu inatosha na wengine waliobaki itawabidi wafunge. Hivi ndivyo alivyoamrisha Mtume (s.a.w) kama tunavyojifunza katika hadithi zifuatazo:
“Ibn Abbas (r.a) ameeleza kuwa Mwarabu wa Jangwani alikuja kwa Mtume (s.a.w) akasema: Hakika nimeuona mwezi wa Ramadhani umeandama. Mtume (s.a.w) akamuuliza: Unashuhudia kuw a hapana Mola ila Allah? “Ndio” alijibu. Akamuuliza tena: Unashuhudia kuwa Muhammad ni Mtume w a Allah? Akajibu “Ndio ”. Akasema (Mtume): Ee Bilal! Watangazie w atu kuw a haw ana budi kufunga kesho”. (Abu Daud, Tirm idh, Nisa i, Ibn Majah).
“Ibn Omar (r.a) ameeleza: Watu waliuona mwezi. Kisha nikamfahamisha Mtume (s.a.w): Hakika nimeuona. Kwa hiyo alifunga na aliwaamrisha watu wafunge”. (Abu Daud, Darimi).
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 900
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Simulizi za Hadithi Audio
👉4 Kitau cha Fiqh
👉5 Kitabu cha Afya
👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Taasisi za Kifedha Katika Mfumo wa Uchumi wa Kiislamu
- Ni taasisi za kifedha zinazohusika na kuhifadhi akiba na mali za watu zenye thamani kubwa kama dhahabu, n. Soma Zaidi...
Vipi utapata uchamungu kupitia funga
Vipi lengo la funga litafikiwa na kumfanya mfungaji awe mchamungu. Soma Zaidi...
Nguzo za swala.
Kipengele hiki kinaelezea nguzo mbalimbali za kuswali. Soma Zaidi...
Sanda ya mwanamke na namna ya kumkafini
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Tofauti ya uchumi wa kiislamu na uchumi wa kikafiri
Uchumi wa kiislamu unatofautiana sana na uchumi wa kikafiri. Hapa utajifunza tofauti hizo. Soma Zaidi...
Kutoa vilivyo vizuri
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Aina au migawanyo mbalimbali ya haki katika uislamu
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Kwanini wengi wanaoswali hawafikii lengo la swala zao
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Kwanini lengo la funga halifikiwi na wafungaji wengi
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Taratibu za mahari katika uislamu
Hapa utajifunza taratibu za kutaja mahari katika uislamu. Soma Zaidi...
Usimamizi wa Haki na haki za binadamu Katika Dola ya Kiislamu
Soma Zaidi...
Funga za suna na funga za kafara na nadhiri: Masharti yake, nguzo zake na wakati wa kutekeleza
Funga za Sunnah. Soma Zaidi...