Mali inayojuzu kutolewa Zakat, Nisaab na kiwango cha Zakat
Aina ya mali inayojuzu kutolewa Zakat imeelezwa kwa wazi katika
Qur-an na Hadith sahihi. Mali inayojuzu kutolewa Zakat ni ile iliyofikia au kuzidi kima maalum kiitwacho Nisaab na kubakia katika milki ya mwenye hiyo mali kwa kipindi chote cha mwaka mmoja. Kila aina ya mali ina nisaab yake, Nisaab ni kiwango cha mali kinachostahiki kitolewe Zakat. Aina ya mali inayojuzu kutolewa Zakat ni:
(i)Mazao yote ya shambani
(ii)Wanyama wafugwao kwa ajili ya chakula
(iii)Dhahabu (gold), fedha (silver), au fedha taslim (cash)
(iv)Vito (mapambo ya dhahabu na fedha)
(v)Madini na mali ya kuchimbuliwa chini ya ardhi au mali ya kuokota
(vi)Mali ya biashara
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi hafifu na najisi ndogo.
Soma Zaidi...Lengo la funga ni kuwa mchamungu sasa ni kwa nini wafungaji hawalifikii lengo hili na kuwa wachamungu.
Soma Zaidi...Huu ni utaratibu unaotakiwa kufanyika baada ya kuzika.
Soma Zaidi...Milki ya RasilimaliIli kujipatia maendeleo ya kiuchumi katika zama zote mwanaadamu anahitaji rasilimali za kumwezesha kufikia azma hiyo.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...