Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu swala ya Istikhara
Istikhaarah maana yake ni kuomba uchaguzi au aumuzi katika jambo. Na Swalaah ya Istikhaarah hakika ni zawadi kubwa tuliyopewa sisi Umma wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwani ina faida kubwa sana kwetu kwani hatuamui jambo letu tunaloliomba katika Swalaah hii, ila baada ya kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atuongoze Yeye hilo jambo kama lina kheri na sisi Atufanikishe nalo na kama ni la shari Atuepushe nalo. Yeye Pekee Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Mwenye kujua ya ghayb yaani yatakayotokea siku za mbele.
Na ndio ilivyokuja katika Du'aa kuwa tunasema:
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْتَخيـرُكَ بِعِلْمِك، وَأسْتَقْـدِرُكَ بِقُـدْرَتِـك، وَأَسْـألُـكَ مِنْ فَضْـلِكَ العَظـيم، فَإِنَّـكَ تَقْـدِرُ وَلا أَقْـدِر، وَتَـعْلَـمُ وَلا أَعْلَـم، وَأَنْـتَ عَلاّمُ الغُـيوب، اللّهُـمَّ إِنْ كُنْـتَ تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ (وَيُسَـمِّي حاجته) خَـيْرٌ لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ أَمْـري، عَاجِلِهِ و آجِلِه , فَاقْـدُرْهُ لي وَيَسِّـرْهُ لي ثـمَّ بارِكْ لي فيـه، وَإِنْ كُنْـتَ تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ شَـرٌ لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ أَمْـري، عَاجِلِهِ و آجِلِه فَاصْرِفْـهُ عَنّيِ وَاصْرِفْني عَنْـهُ وَاقْـدُرْ ليَ الخَـيْرَ حَيْـثُ كانَ ثُـمَّ أَرْضِـني بِـه.
Ee Allaah hakika mimi nakutaka (muongozo) unichagulie kwa ujuzi Wako, na nakuomba Uniwezeshe kwa uwezo Wako, na nakuomba fadhila Zako kubwa, hakika Wewe Unaweza, nami siwezi, Nawe unajua nami sijui, Nawe ni Mjuzi wa ya ghayb. Ee Allaah, iwapo jambo hili kutokana na ujuzi Wako (utalitaja jambo lako) lina kheri na mimi katika Dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu, katika Dunia yangu na Aakhirah yangu, basi nakuomba Uniwezeshe nilipate, na Unifanyie wepesi, kisha Unibariki. Na iwapo Unajua kwamba jambo hili ni shari kwangu katika Dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu, katika Dunia yangu na Aakhirah yangu, basi liepushe na mimi nami niepushe nalo, na nipangie jambo jengine lenye kheri nami popote lilipo, kisha niridhishe kwalo. [Al-Bukhaariy]
Kwa hiyo inampasa Muislamu awe anaitumia sana Swalaah hii kwa kila jambo lake, likiwa ni dogo au kubwa kwani juu ya kupata faida ya kwamba unamuachia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Mwenye Ujuzi na Mwenye Hikma kutuongoza, pia unapata thawabu za kuswali Raka'ah mbili.
Lakini haifai kuswali Swalaah hii kwa ajili ya maasi na maovu au hata katika ‘ibaadah za fardhi. Mfano mwizi haimpasi kuiswali Swalaah hii ili atake uamuzi kama akaibe au la. Au mwanamke asiiswali Swalaah hii ikiwa yuko katika wasiwasi wa shaytwaan unaotaka kumpelekea kufanya zinaa na kadhalika.
Vile vile asiswali mtu Swalaah hii katika kutimiza fardhi; mfano katika kutoa Zakah au jambo la kheri kama swadaqah na kadhalika, kwani huo ni wasiwasi wa shaytwaan kukuzuia kutenda hayo yanayopasa kutendwa.
Swalaah hii inaweza kutumika katika mambo yanayofaa mfano unataka kwenda safari, au umeomba kazi katika shirika fulani, au unataka kuoa au mwanamke amekuja kuposwa na kadhalika.
Vile vile unapokuwa na uamuzi wa mambo mawili na hujui jambo lipi mojawapo ni lenye kheri, mfano unayo akiba yako ya fedha na kuna fursa ya kufungua mojawapo ya biashara za aina mbili, sasa hujui biashara gani katika hizo ndio yenye kheri na wewe, hapo utaswali ili upate mwongozo wa biashara itakayokuwa na kheri na wewe.
Kisha baada ya kuswali Swalaah hii kwa mambo yanayofaa kuiswalia, inakuwa umeshamuachia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akuongoze, kwa hiyo vyovyote utakavyoamua itakuwa ndio mwongozo Wake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na itakuwa ndio kheri yako.
Si lazima mtu aote ndoto kama wanavyofikiria baadhi ya watu baada ya kuswali Swalaah hii.
Swalaah hii haiswaliwi kwa niyyah kuomba haja kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) unapotaka kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) haja yoyote, ni kuomba Du'aa mwenyewe kama kawaida ikiwa ni katika Swalaah au nje ya Swalaah
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1403
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 kitabu cha Simulizi
DARSA ZA NDOA, FAMILIA, SIASA, BIASHARA, UCHUMI, HAKI NA SHERIA KATIKA UISLAMU
1. Soma Zaidi...
kuletewa ujumbe
(c)Kuletewa Ujumbe na Malaika kutoka kwa Allah (s. Soma Zaidi...
Wanaorithi katika wanaume na wanawake na kiwango wanachorithi
Soma Zaidi...
NAMNA YA KUSWALI SEHEMU YA KWANZA
Mtume (s. Soma Zaidi...
Ni mambo yapi hupunguza Swawabu na malipo yamwenye kufunga
Soma Zaidi...
Jinsi ya kutekeleza funga za sunnah
Hapa utajifunza muda wa kutia jia katika funga za sunnah. Pia utajifunza kuhusu uhuru ulio nao Soma Zaidi...
Maana ya mirathi katika uislamu
Post hii itakufundishabkuhusu mirathi ya kiislamu, maana yake. Soma Zaidi...
Aina za swala..
Nguzo za uislamu,aina za swala (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Swala ya Istikhara na jinsi ya kuiswali
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu swala ya Istikhara Soma Zaidi...
Mafunzo ya swala
Jifunze namna ya kuswali, zijuwe aina za swala na ujifunze masharti ya swala, kwa nini swala hazijibiwi? nini kifanyike? Soma Zaidi...
Zijuwe aina za swala za Suna na namna za kuziswaliWitri, Dhuha, Idi, tarawehe, tahajudu na nyingine
Soma Zaidi...