image

Haki na wajibu kwa mayatima

Haki na wajibu kwa mayatima

Wajibu kwa MayatimaYatima ni mtoto aliyefiwa na wazazi wake, hasa baba, kabla ya kufikia baleghe. Uislamu unatuhimiza kuwatendea wema yatima na kuwatunzia urithi wao kwa uadilifu mpaka wafikie baleghe yao na kuwa na akili ya kutunza mali.


"... Na wanakuulizajuu ya mayatima: Sema: Kuwatendea mema ndivyo vizuri. Na kama mkichanganyika nao (ndivyo vyema vile vile) ,kwani ni ndugu zenu..." (2:220)
Tunajifunza kutokana na aya hii kuwa tunatakiwa tuwatendee wema mayatima na tuishi nao katika familia kama tunavyoishi na watoto wetu. Kukaa nao pamoja kwa huruma na mapenzi kutawafariji na kuziba pengo Ia kufiwa na mzazi au wazazi wao. Si katika mwenendo wa Kiislamu kuwatenga mayatima kwenye makazi maalumu. Tuishi nao katika familia zetu na tuwasomeshe katika shule wanazosoma watoto wetu.Kuwanyanyasa mayatima ni katika madhambi makubwa mbele ya Allah (s.w). Si muumini wa kweli yule anayemnyanyasa yatima kama tunavyojifunza katika Qur-an:


".Je, umemuona yule anayekadhibisha dini (asiyeamini malipo ya akhera)? Huyo ni yule anayemsukuma (anayemnyanyasa) yatima." (107:1-2)Msisitizo wa kuwatendea wema mayatima pia tunaupata katika hadith zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: "Kaya (familia) bora kuliko zote ni ile ambamo anatendewa wema yatima; na kaya mbovu kuliko zote ni ile ambamo ananyanyaswa yatima." (Ibn Majah)Sahl bin Sa 'ad (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: 'Mimi na yule anayemlea yatima (kwa wema), akiwa wa kwake au kwa wengine, tutakuwa naye peponi kama hivi - akionyesha kidole cha mwanzo (cha shahada) na kinachofuatia (cha kati) huku vikiwa vimeshikamana bila ya kuachana mwanya wowote ". (Bukhari)
Kuwatendea wema mayatima ni pamoja na kuwatunzia mali zao za urithi kwa uadilifu kama inavyosisitizwa katika Qur-an:


"Na wapeni mayatima mali zao. Wala msibadilishe kibaya kwa kizuri. Wala msile mali zao pamoja na mali zenu. Hakika (yote) hayo nijukumu kubwa." (4:2)Na wajaribuni mayatima (wanapokuwa karibu ya kubaleghe kama wataweza kutumia fedha zao vizuri wakati watakapobaleghe. Wajaribuni kidogo kidogo) mpaka wafike wakati wa kuoa (kubaleghe). Kama mkiwaona wana akili njema, wapeni mali zao. Wala msizile kwa fujo na kwa haraka ya kwamba watakua (wazitake; hebu tuzile upesi). Na mwenye kuwa tajiri basi ajiepushe (na kuchukua ujira katika kuwafanyia kazi zao). Na atakayekuwa mhitaji basi ale kwa namna inayokubaliwa na Sharia. Na mtakapowapa mali zao, basi wawekeeni mashahidi (/uu ya kuwa Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi. (4:6)


Hakika wale ambao wanakula mali ya mayatima kwa dhuluma, bila shaka wanakula moto matumboni mwao; na wataungua katika huo Moto (wa Jahannam) uwakao. (4:10)
Kutokana na aya hizi tunahimizwa kutunza mali za mayatima mpaka watakapofikia umri stahiki ndio tuwakabidhi. Kama tuna uwezo tusitumie chochote kutokana na mali hiyo katika kuwalea. Kama hatuna uwezo tunaruhusiwa tuitumie katika kuwapa mahitaji ya lazima kama vile Elimu, mavazi, n.k; lakini vile vile kwa tahadhari na ungalifu.
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 249


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Zijuwe aina za swala za Suna na namna za kuziswaliWitri, Dhuha, Idi, tarawehe, tahajudu na nyingine
Soma Zaidi...

Kumuandaa maiti punde baada ya kufariki dunia
Soma Zaidi...

Kuandama kwa Mwezi na Kufunga ama kufungua ramadhani, sheria na hukumu za kuangalia mwezi
Soma Zaidi...

Funga za kafara
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Masharti ya utoaji wa zakat na sadaqat
Nguzo za uislamu, masharti ya utoaji wa zakat na sadaqat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kufunga Mwezi wa ramadhani kisheria
Soma Zaidi...

haki na wajibu kwa wakubwa
Soma Zaidi...

Swala ya jamaa na mnamna ya kuswali swala ya jamaa, nyumbni, msikitini na kwa wanawake
Soma Zaidi...

Sera ya uchumi katika uislamu
Hapa utajifunza sera za kiuchumi katika uchumi wa kiislamu. Hapa utajifunza sera kuu tatu za uchumi wa kiislamu. Soma Zaidi...

Tathmini ya swala zetu, kwa nini swala zetu hazijibiwi?
Soma Zaidi...

Je manii ni twahara au najisi?
Post hii itakwenda kukufundisha hukumu ya manii kuwa ni twahara ama ni najis Soma Zaidi...

Taratibu za ndoa ya kiislamu, hatua kwa hatua
Soma Zaidi...