Ni nini maana ya uchumi katika uislamu

Ni nini maana ya uchumi katika uislamu

Katikabuislamu dhana ya uchumi imetofautiana na dhana ya kidunia hivi leo ambapo kamari na riba ni moja ya vitu muhimu katika uchumi.

Maana ya Uchumi
Mfumo wa maisha wa Kiislamu humuelekeza binaadamu kujenga na kudumisha uhusiano wake na Al-lah (s.w), uhusiano wake na binaadamu wenziwe na uhusiano wake na vinavyomzunguka katika ulimwengu huu. Aidha mfumo wa Kiislamu una lengo la kuelekeza namna ya kukiendea kila kipengele muhimu cha maisha ya binaadamu uchumi ukiwa miongoni.

 


Uchumi hujumuisha uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa mali na huduma. Uislamu umelipa suala la uchumi nafasi muhimu kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:

 

“Wala msiwape wapumbavu mali zenu ambazo Allah amezijaalia kuwa msingi wa maisha yenu…” (4:5)
Uislamu umeweka utaratibu wa kiuchumi unaohakikisha kuwa haki inatendeka kwa wote ili kudumisha amani, utulivu na mshikamano wa kweli katika jamii. Katika sura hii tutaangalia uchumi katika Uislamu kwa kuzingatia maeneo yafuatayo:

 

1.Nadharia ya uchumi wa Kiislamu.
2.Umuhimu wa uchumi katika Uislamu.
3.Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu.
4.Sera ya uchumi katika Uislamu.
5.Haki na Uhuru wa kuchuma katika Uislamu.
6.Mgawanyo wa mali katika Uislamu.
7.Umuhimu wa Benki katika Uchumi.
8.Tatizo la Riba.

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views: 2470

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Dua za Mitume na Manabii     👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 web hosting    

Post zinazofanana:

Kuenea kwa dhana ya udhibiti uzazi na uzazi wa mpango

Kustawi kwa Kampeni ya Kudhibiti UzaziMiongoni mwa sababu zilizosaidia kustawi kwa kampeni hii ni matokeo ya mapinduzi ya viwanda (Industrial revolution) ya huko Ulaya.

Soma Zaidi...
Jinsi Uislamu Ulivyokomesha Biashara ya Utumwa wakati na baada ya Mtume Muhammad (s.a.w)

- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.

Soma Zaidi...