image

Swala ya jamaa na mnamna ya kuswali swala ya jamaa, nyumbni, msikitini na kwa wanawake

Swala ya jamaa na mnamna ya kuswali swala ya jamaa, nyumbni, msikitini na kwa wanawake

Kusimamisha Swala ya Jamaa



Ni wajibu na imekokotezwa sana kwa Waislamu wanaume kusimamisha swala za faradh katika jamaa. Swala ya Vita kama ilivyobainishwa katika Qur-an (4:102) ni kielelezo cha umuhimu wa kusimamisha swala za faradhi katika jamaa. Kama katika vita waislamu wamesisitizwa kuswali pamoja katika jamaa, itakuwaje tena katika hali ya kawaida Muislamu ajiamulie kuswali peke yake nyumbani kwake?



Mtume (s.a.w) ametuagiza kwa msisitizo mkubwa kusimamisha swala katika jamaa kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:
Ibn Abbas (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Atakaye msikia muadhini (kwa ajili ya swala), pasina udhuru wa kumzuia, hana budi kumuitikia. Wakauliza:Ni dharura gani (itakayomruhusu Mu is lamu kutomuitikia muadhini)? Alijibu (Mtume). Hofu ya kudhuriwa njiani na ugonjwa. Hana sw ala atakayeswali mwenyewe bila ya jamaa (baada ya kusikia adhana),(Abu Daud)



Abu Darda (r.a) ameeeleza kuwa Mtume wa Allah amesema, hapatakuwa na watu watatu katika kijiji au jangwani, wakaamua kuswali kila mmoja peke yake, ila Shetani huwemo katika swala zao.Hapana budi kuswali jamaa kwa sababu mbwa mwitu humkamata kondoo aliyejitenga na kundi. (Ahmad, Abu Daud, Nisai).



Hadithi hizi mbili zinasisitiza umuhimu wa kuswali swala ya jamaa. Imesisitizwa kwamba, kila mwenye kusikia adhana, kwa sauti ya kawaida (bila ya kipaza sauti) au kila aliyeko karibu na msikiti inamlazimu atoke kuitikia mwito wa adhana kwa swala ya jamaa. Hata wale walio mbali na msikiti, (vijijini au shambani) hawana budi kukusanyika pamoja na kuswali jamaa. Hekima ya kusisitizwa kuswali jamaa imeelezwa katika Hadithi ya pili kuwa ni silaha ya kuunganisha nyoyo na kuziwezesha kumshinda Shetani. Hii ina maana kuwa vishawishi vingi vinavyomjia mtu kwenye swala hupungua au hutoweka wakati mtu anaposwali katika jamaa.



Pia Hadithi zifuatazo zinaonesha umuhimu wa swala ya jamaa: Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema, “Naapa kwa yule ambaye maisha yangu yako mikononi (mwake), hakika nataka kutoa amri zikusanywe kuni, kisha itolewe adhana kwa ajili ya swala, kisha nitoe amri mtu mmoja awe Imamu wetu, kisha (wakati huo wa swala) nitoke nikatie moto majumba ya wale wasiotoka kwa swala ya jamaa...” (Bukhari).
Pia katika Hadithi nyingine,



Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) kasema, “Kama si kwa sababu ya kuwepo watoto na wanawake katika nyumba, ningetaka nianze kuswalisha jamaa ya swala ya Isha na papo hapo kuwaamrisha vijana wachome moto nyumba zile watakazokuta humo watu ” (Ahmad)



Abdullah bin Ummi Makhtuumi (r.a) aliuliza: “Ewe Mtume w a Mwenyezi Mungu Madina imejawa na wanyama wenye sumu na wanyama mwitu na mimi sioni (kipofu). Je, unanipa ruhusa ya (kuswali nyumbani)?” (Mtume) alimuuliza: Je, unasikia - Njoo kw enye swala, njoo kw enye kheri (yaani unasikia adhana)? ” Ndio, alijibu (yule kipofu). Akasema (Mtume): Sasa kwanini usije (msikitini)? Kwa hiyo Mtume (s.a.w) hakumruhusu kuswali nyumbani. (Abu Daud, Nisai)



Swala ya faradhi iliyoswaliwa katika jamaa ni bora zaidi mara 27 kuliko ile ya mtu peke yake kama tunavyojifunza katika Hadithi ifuatayo:
Ibn Umar amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Swala moja iliyoswaliwa katika jamaa malipo yake ni bora zaidi mara ishirini na saba (2 7) kwako kuliko malipo ya swala (hiyo hiyo) iliyoswaliwa bila ya jamaa”. (Bukhari na Muslim).



Swala ya jamaa huanza na watu wawili - Imamu (Mwenye kuswalisha) na Maamuma (Mwenye kuswalishwa), kama tunavyofahamishwa katika Hadithi ifuatayo:
Abu Musa al-Ash-ariyyi amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Wawili au zaidi ya hapo hufanya jamaa”. (Ibn Majah).



Ruhusa kwa Wanawake Kuswali Jamaa Msikitini



Msisitizo wa kuswali swala za faradhi katika jamaa ya msikitini umewekwa kwa Waislamu wanaume. Kwa wanawake si lazima kwao kuswali jamaa msikitini lakini wakitaka kwenda msikitini wapewe ruhusa na waume zao au mawalii wao kutokana na kauli ya Mtume (s.a.w) ifuatayo:



Ibn Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah kasema: “Mke wa mmoja wenu atakapotaka ruhusa ya kwenda mskitini, hana budi kumruhusu” (Bukhari na Muslim).
Lakini pamoja na ruhusa hii, Wanawake wa Kiislamu wanapotoka nje ya njumba zao kwenda msikitini au kwingineko hawana budi kujiheshimu kwa kujistiri ipasavyo na wasijipake manukato.



Udhuru wa Kutoswali Jamaa Msikitini



Tumeona kuwa katika hali ya kawaida Muislamu mwanamume aliye karibu na msikiti kiasi cha kusikia adhana ni lazima mara tu asikiapo adhana aitikie wito na kwenda kujiunga na jamaa msikitini. Lakini kama tujuavyo, Uislamu ni dini ya wastani, yaani ni dini pekee inayozingatia hali halisi ya maisha ya kawaida ya mwanadamu na mazingira yake. Uwastani wa Dini ya Kiislamu, unaonekana katika kauli mbali mbali za Mtume (s.a.w) juu ya nyudhuru za kusamehewa kusali jamaa na kuruhusiwa kuswali nyumbani.
Ibn Umar (r.a) amesimulia kuwa: Katika siku ya baridi kali na upepo aliadhini akasema, “Sikilizeni Sw alini nyum bani mw enu ”. Baadaye alisema, “Mtume wa Allah alikuwa akimuelekeza muadhini katika usiku wa baridi na mvua kuwa aseme: Sikieni swalini nyumbani kwenu”. (Bukhari na Muslim).



Ibn Umar (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah (s.a.w) amesema mmoja wenu atakapotengewa chakula (mezani) na wakati huo huo swala(ya jamaa) Ikaanza, naanze kula kwanza na asifanye haraka mpaka amalize kula. Na Ibn Umar alipotengewa chakula wakati swala inaanza, hakuja kwa swala (ya jamaa) mpaka alipomaliza kula, japo alikuwa akisikia Qur-an inasomwa na Imamu. (Bukhari na Muslim)



Aysha (r.a) ameeleza: Nimemsikia Mtume wa Allah (s.a.w) akisema: Hakuna swala wakati chakula kimetengwa (mezani) wala hapana swala wakati mtu amebanwa na haja ndogo (au kubwa). (Muslim)


Abdullah bin Arqama (r.a) amesimulia: Nimemsikia Mtume wa Allah (s.a.w) akisema: Iqama ikitolewa kwa kuanza swala, na kisha mmoja wenu akajisikia kubanwa na choo kikubwa au kidogo na akajisaidie kwanza. (Tirmidh)



Kutokana na mafunzo ya Qur-an na Hadithi tunajifunza kuwa nyudhuru za kutoswali swala katika jamaa iliyowadia ni hizi zifuatazo:
(1)Machafuko ya hali ya hewa; mvua, baridi kali sana au jua
kali sana.
(2)Wakati ukiwa na njaa na chakula kimeshatengwa mezani.
(3)Kushikwa na haja ndogo au kubwa.
(4)Kuwa mgonjwa au muuguzi.
(5)Kuwa na khofu ya kudhuriwa njiani.



Inaruhusiwa kuswali swala moja mara mbili
Kwa sababu mbali mbali, mtu akiona haja ya kurudia swala ya faradhi anaweza kuswali tena. Kwa mfano, mtu akiwakuta watu wanaswali swala ya jamaa anashauriwa aifuate jamaa ile hata kama atakuwa amesha swali swala hiyo. Swala yake hii ya pili itakuwa ni Sunnah kwake na atapata ujira wake kamili. Tunafahamishwa katika hadithi ifuatayo:



Yazid bin Amir (r.a) amesimulia: Nilikuja kwa Mtume (s.a.w) akiwa katika swala. Nilikaa bila ya kujiunga katika swala na wao. Mtume wa Allah alipomaliza kuswali aliniona nikiwa nimekaa pale akaniuliza: Ewe Yazid! Hujaukubali (hujaingia) Uislamu? ‘Ndio Ewe, Mtume wa Allah, nimeukubali Uislamu. Akasema (Mtume (s.a.w)): Ni kitu gani kilichokuzuia kujiunga na watu katika swala yao? Alijibu: Nimeswali nyumbani kwangu, nafikiri sw ala hiyo hiyo mliyoisw ali. Alisema (Mtume): “Unapokuja kwenye swala na ukawakuta watu wanaswali, swali nao japo utakuwa umeshaswali. Itakuwa ni Sunnah kwako na malipo yake yatadhibitiwa. (Abu Daud).

Namna ya Kuswali Katika Jamaa



Swala ya jamaa itakamilika iwapo masharti ya kuswali jamaa yatafuatwa ipasavyo. Ya muhimu katika swala ya jamaa ni kusimama inavyostahiki na kumfuata Imamu.
1. Jamaa ya watu wawili
Kama jamaa itakuwa ni ya watu wawili tu, Imamu na Maamuma basi Imamu atakuwa mbele na Maamuma atakuwa nyuma kidogo upande Pia Imamu anatakiwa asiwe mbali zaidi na Maamuma bali wawe katika usawa mmoja.



2. Jamaa ya Watu Watatu
Maamuma wakiwa wawili watasimama dhiraa moja nyuma ya Imamu katika mstari ulionyooka . Mmoja atakuwa sawa na imamu na mwingine atakuwa upande wa kulia.


3. Jamaa ya Watu Zaidi ya Watatu
Maamuma wakiwa watatu na kuendelea watasimama dhiraa moja nyuma ya Imamu katika mstari ulionyooka na kumfanya Imamu awe katikati. Wanaokuja baadaye kuunga jamaa watajaza mstari kulia na kushoto. Mstari mpya utajazwa kulia na kushoto kuanzia katikati usawa wa Imamu, dhiraa moja nyuma ya mstari wa kwanza.


Jamaa ya watu zaidi ya watatu wakiwa nyuma ya Imam- dhiraa moja. - Dhiraa ni kipimo cha mkono ulionyooshwa



Kusimama Katika Mistari



Mwenye kukimu anaposema, “Qad-qaamatis-swalaa” - swala iko tayari kusimamishwa: yawapasa Waislamu wasimame haraka haraka na kujiweka sawa na kunyoosha mistari huku wakiwa wamekaribiana kiasi cha kugusanisha mabega yao na vidole vyao vya miguu. Mtume (s.a.w) amesisitiza sana utaratibu huo kama tunavyojifunza katika Hadithi ifu atayo:-



Anas (r.a) amesema: Iqama ilitolewa kwa ajili ya swala kisha Mtume wa Allah alitusogelea huku akiwa ametugeukia akasema: Nyoosheni mistari yenu na simameni bega kwa bega, kwa sababu ninawaona kwa nyuma (kama ninavyowaona kwa mbele).(Bukhari)


Anas (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah alikuwa akigeukia kulia na kusema: Kaeni sawa na nyoosheni mistari yenu kisha alikuwa akigeukia kushoto na kusema: Kaeni sawa na nyoosheni mistari yenu”.



Pia Mtume (s.a.w) pamoja na kusisitiza kunyoosha mistari, kukaribiana na kujaza nafasi, amefundisha na kusisitiza vile vile utaratibu wa ujazaji nafasi. Hebu tuangalie hadithi zifuatazo:



Abu Masud Ansari (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah (s.a.w) alikuwa akishika mabega yetu katika swala na kusema nyookeni (kaeni sawa) na msifarikiane, nyoyo zenu zisije zikafarikiana.Wale walio wazee na wenye hekima (elimu) na wasimame karibu yangu, kisha wafuate wanao wafuatia (kwa umri na elimu), kisha wafuatie wanaowafuatia hawa, Abu Mas ’sud akasema leo utaratibu huu hamuufuati vilivyo. (Muslim).



Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Mstari ulio bora kwa Wanaume ni mstari wao wa mbele (karibu na Imamu), na mstari ulio mbaya (duni) kuliko yote ni mstari wao wa nyuma, na mstari ulio bora kuliko yote kwa Wanawake ni mstari wa nyuma na mstari ulio mbaya kwao kuliko yote ni mstari wao wa mbele (karibu na wanaume). (Muslim).


Abu Sa ’d Al-Khudriyyi (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah aliona tabia ya baadhi ya Maswahaba wake kujirudisha nyuma, kwa hiyo aliwaambia njooni mbele na nifuateni na wale walio nyuma yenu wawafu ate. Watu hawataacha kujiweka nyuma mpaka Allah awabakishe nyuma kabisa (Allah atawaweka nyuma wanaojiweka nyuma) (Muslim).
Hadithi hizi zinatufahamisha kuwa mstari ulio bora kabisa unaostahiki ukimbiliwe kwa juhudi kubwa, kwa wanaume ni mstari wa mbele na kwa wanawake ni mstari wa nyuma. Mwenye kuwahi ndiye atakayestahiki kukaa mstari wa mbele. Pamoja na sifa hii ya kuwahi, sifa nyingine mbili za ukaaji katika mstari zimezingatiwa. Hizi ni sifa za elimu na umri. Watu wenye elimu na wazee watakaa mistari ya mbele karibu na Imamu na watoto watakaa mistari ya nyuma kwa upande wa wanaume. Utaratibu huu utakuwa kinyume chake kwa upande wa Wan awake.



Kuswali na Wanawake Nyumbani katika Jamaa



Tunaposwali na familia zetu nyumbani, wanawake watakaa mstari wa nyuma. Hawatasimama mstari mmoja na Wanaume hata kama ni maharimu kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:



Anas(r.a) amesimulia, Mimi na Yati’in tuliswali katika nyumba ya Mtume (s.a.w) na Ummu Salaam aliswali nyuma yetu”. (Muslim)
Pia Anas (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) aliswali pamoja naye na pamoja na Mama yake mdogo na amesema: (Mtume) alinisimamisha kuliani kwake na akamfanya yule mwanamke asimame nyuma yao”. (Muslim).



Jamaa ya Wanawake Wenyewe
Wanawake wanalazimika kuswali kama wanaume maadam hawakuwepo katika hedhi au nifasi. Wanapokuwa katika hedhi au nifasi hawalazimiki kulipa swala walizoacha kuswali kwa sababu ya hedhi au nifasi.



Wanawake hawalazimiki kuadhini au kukimu lakini si vibaya iwapo wataadhini na kukimu. Wakiwa wengi, wawili au zaidi, watalazimika kuswali jamaa. Mmoja wao atakuwa Imamu lakini hatajitokeza mbele kama tunavyofahamishwa katika hadithi ifuatayo:



Amesema Aisha (r.a) kuwa yeye (Aisha) alikuwa akiadhini na kuqimu na kuwaswalisha wanawake wenzake, lakini alikuwa akisimama nao katika safu ya mbele. (Baihaqi)




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1243


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

.Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu
3. Soma Zaidi...

haya ndiyo mambo yanayaribu swala na yanayobatilisha swala
Soma Zaidi...

Nafasi ya serikali katika ugawaji
Serikali ina nafasi katika kufanya mgawanyiko katika uchumi. Soma Zaidi...

Swala ya witiri na faida zake, na jinsi ya kuiswali
Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya witiri na faida zake kwa mwenye kuiswali. Soma Zaidi...

Ni mali ipi inatakiwa kutolewa zaka?
Soma Zaidi...

Nini maana ya kusimamisha swala?
Je kusimamisha swala kuna maana gani kwenye uislamu? Soma Zaidi...

Kutoa vilivyo vizuri
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Jinsi ya kuoga josho la kiislamu ( janaba, hedhi na nifasi)
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kuoga josho kisheria. Soma Zaidi...

Umuhimu, Ubora na Fadhila za kufunga
Soma Zaidi...

Sera ya uchumi katika uislamu
Hapa utajifunza sera za kiuchumi katika uchumi wa kiislamu. Hapa utajifunza sera kuu tatu za uchumi wa kiislamu. Soma Zaidi...

Madhara ya riba kwenye jamii
Haya ni madhara ya riba katika jamii. Ni kwa namna gani jamii inadhurika kutokana na riba? Soma Zaidi...

haki za mwanamke za kisiasa katika uislamu
Haki ya Kushiriki Katika Siasa. Soma Zaidi...