Maana ya Swaumu na Lengo la kufunga
Maana ya Swaumu (Funga)
Kilugha; neno “Swaum” lina maana ya kujizuilia kufanya jambo lolote la kawaida. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Bibi Maryam baada ya kumzaa nabii Isa (a.s) alijizuilia (alikuwa katika Swaum ya) kutosema na mtu yoyote juu ya mtoto wake.
“... Na kama ukimuona mtu yeyote (akauliza habari za mtoto huyu) sema: `Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa Rehema ya Swaum (kufunga), kwa hiyo leo sitasema na mtu’” (19:2 6).
Katika Sharia ya Kiislamu kufunga (Swaum) ni kujizuilia kula, kunywa, kujamii, kuingiza kitu chochote katika matundu ya mwili na kujizuilia kumuasi Allah (s.w) kuanzia alfajiri ya kweli mpaka kuingia ma gharibi.
Lengo la Swaumu
Lengo la Swaum katika Uislamu ni kumuwezesha mja awe mcha Mungu kwa kufuata maamrisho yote ya Allah (s.w) na kuacha makatazo yake yote. Hivyo, ili lengo hili litimie mfungaji pamoja na kujizuilia kula, kunywa, kujamii, hanabudi pia kujizuilia na kitendo chochote kitakachompelekea kuvunja amri ya Allah (s.w) na Mtume wake (s.a.w). Kwa maana nyingine, ili Swaum ya mfungaji iwe na maana na yenye kufikia lengo, mfungaji hana budi kukizuilia (kukifungisha) kila kiungo chake cha mwili - macho, ulimi, masikio, mikono na miguu pamoja na fikra na hisia zake -na matendo aliyoyakataza Allah (s.w.).
Funga ya macho ni kujizuilia kutazama yale yote aliyoyakataza Allah (s.w), funga ya ulimi ni kujizuilia na mazungumzo yote aliyoyakataza Allah (s.w), kama vile kusengenya, kusema uwongo, kugombana n.k., funga ya masikio ni kujizuilia kusikiliza yale yote aliyoyaharamisha Allah (s.w); funga ya miguu ni kujizuilia kuendea yale yote aliyotukataza Allah (s.w); funga ya fikra na hisia, ni kujizuilia na fikra na dhana mbaya ambazo zinampelekea mja kuvunja amri na makatazo ya Allah (s.w). Ni katika maana hii Mtume (s.a.w) anasema katika Hadith zifuatazo:
“Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Yule ambaye haachi kusema uwongo na haachi kufanya vitendo viovu, Allah hana haja na kuona kuw a anaacha chakula chake na kinyw aji chake - ( Allah (s.w) hana haja na funga yake). (Bukhari).
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema; Ni wangapi wamefunga lakini hawana funga ila kukaa na kiu tu, ni wangapi wanaoswali usiku ambao hawana swala ila huambulia kupoteza usingizi tu. (Darimi).
Hadith hizi zinatuthibitishia kuwa ufungaji usioambatana na kujizuilia na maovu na machafu, haumpatii mfungaji faida yoyote.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 ai web app 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Vipi funga yaani swaumu itapelekea uchamungu na kutekeleza lengo
Funga inavyomuandaa mtu kuwa mcha-Mungu.
Soma Zaidi...Ni kwa nini lengo la Funga na swaumu halifikiwi na wafungaji?
Kwa nini Lengo la Funga halifikiwi na Wafungaji Wengi?
Soma Zaidi...Ubainifu kati ya halali na Haramu na kujiepusha na mambo yanayo tatiza
عَنْ أَبِي عَبْدِ اللَّهِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَ: سَمِعْت رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم يَقُ?...
Soma Zaidi...Yaliyo haramu kwa mwenye hadathi kubwa.
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ya haramu kwa mwenye hadathi kubwa
Soma Zaidi...