picha

Jinsi ya kuelekea qibla katika swala.

Je unadhani ni kwa nini waislamu wanaelekea kibla, na jinsi gani utaweza kukipata kibla.

4. Kuelekea Qibla

Kuelekea Qibla ni sharti la nne la kusimamisha swala. Katika hali ya kawaida Muumini ni lazima aelekee “Qibla wakati akiswali.Qibla ni neno la Kiarabu linatokana na neno “Qabala” lenye maana ya kuelekea sehemu au upande ambao watu huelekeza nyuso zao. Kwa mtazamo wa Qur-an, Qibla ni sehemu wanapoelekea waislamu wakati wa kuswali. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Qibla ni sehemu ya katikati inayowaunganisha waumini kuwa mwili mmoja (kitu kimoja).

 

“Na po pote wendako geuza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu . Na hiyo ndiyo haki itokayo kwa Mola wako. Na Mw enyezi Mungu si Mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda. (2:149)

 


Ummati wa Muhammad (s.a.w) Qibla chake ni Ka’aba, nyumba tukufu ya Allah iliyoko mjini Makkah, Saudi Arabia. Waislamu wote ulimwenguni huielekea Ka’aba wakati wa kuswali. Swala yoyote itakayoswaliwa bila ya kuelekea upande ilipo Ka’aba, pasipo na dharura inayokubalika kisheria kama vile kuwa mgonjwa, au kuwa safarini, ha is wih i.

 


Namna ya Kutafuta Qibla

 


Kukisia ulipo mji wa Makka, Saudi Arabia, ambao ndani yake iko Ka’aba ni jambo rahisi kwa kutumia utaalamu wa Jiografia. Chombo

 

kizuri cha kumuwezesha mtu kukisia ilipo Ka’aba ni ramani ya dunia. Utakapojua ulipo katika sehemu yoyote ya dunia utaweza kujua Ka’aba iko upande gani wa dira kutokea pale ulipo kwa kutumia jua au chombo cha dira (Magnetic Compass). Kwa mfano ukiwa Tanzania, utaelekea Kaskazini kamili, ukiwa Pwani kama vile Dar es Salaam na ukiwa bara kama vile Kigoma, utaelekea Kaskazini ya Kaskazini Mashariki.

 


Kabla ya Muislamu hajaanza kuswali, hasa anapokuwa mgeni wa mahali hana budi kufanya jitihada ya kutafuta Qibla kwanza. Ni vyema mtu asafiripo awe na dira (Magnetic Compass) na ramani ili vifaa hivi vimsaidie kutafuta Qibla, vinginevyo itabidi awaulize wenyeji wa sehemu h iyo.

 


Mtu akishindwa kabisa kukibaini Qibla baada ya kujitahidi mwisho wa jitihada zake, popote atakapoelekea patafaa, kwani hii sasa imekuwa ni dharura, huku tukizingatia kuwa “Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu”.

 

Na Mashariki na Magharibi ni ya Mw enyezi Mungu. Basi mahala popote mgeukiapo (alikokuamrisheni Mw enyezi Mungu mtazikuta) huko radhi za Mwenyezi Mungu. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa (mkubwa kabisa) na Mwenye kujua (kukubwa kabisa vile vile). (2:115)

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views 2392

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 ai web app     ๐Ÿ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio     ๐Ÿ‘‰3 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰4 web hosting     ๐Ÿ‘‰5 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Hatua za kinga za ugumba na Utasa.

Ugumba ni รขโ‚ฌล“ugonjwa wa mfumo wa uzazi unaofafanuliwa kwa kushindwa kupata ujauzito baada ya miezi 12 au zaidi ya kujamiiana bila kinga mara kwa mara. Utasaร‚ย  kutoweza kwa kiumbe hai kufanya uzazi wa ngono au kutoweza kupata mimba au kuchangia mimba.

Soma Zaidi...
udhaifu wa hoja za kuunga mkono kuzibiti uzazi na uzazi wa mpango

Udhaifu wa Hoja za Kudhibiti Uzazi:Hoja nyingi zinazotolewa kuunga mkono udhibiti wa uzazi zimejengwa juu ya hali na mazingira ya maisha yaliyoletwa na utamaduni na maendeleo ya nchi za Ulaya na Marekani.

Soma Zaidi...
Sifa nyingine za kuchaguwa mchumba ambazo watu wengi hawazijui

Hizi ni sifa za ziada za mchumba katika uislamu. Sifa hizi wengi hawazijui ama hawazingatii.

Soma Zaidi...
Nafasi ya serikali katika ugawaji

Serikali ina nafasi katika kufanya mgawanyiko katika uchumi.

Soma Zaidi...