image

(b)Umbile la Mwanaadamu ni la kidini

Ukizingatia maana halisi ya dini, kuwa dini ni utaratibu wa maisha, utadhihirikiwa kuwa umbile la mwanaadamu ni la kidini.

(b)Umbile la Mwanaadamu ni la kidini

(b)Umbile la Mwanaadamu ni la kidini


Ukizingatia maana halisi ya dini, kuwa dini ni utaratibu wa maisha, utadhihirikiwa kuwa umbile la mwanaadamu ni la kidini.


Umbile la mwanaadamu kama maumbile mengine yaliyomzunguka hufuata mfumo maalum bila ya matashi au hiari ya mwanaadamu.


Kwa maana nyingine umbile la mwanaadamu limedhibitiwa na sheria za maumbile (natural Laws - biological, chemical, and physical laws).


Kwa mfano, ukichunguza hatua anazozipitia mwanaadamu katika tumbo la uzazi mpaka kuwa kiumbe kamili, ni utaratibu madhubuti ambao uko nje kabisa ya uwezo au matashi yake. Kuhusu kuumbwa kwa mwanaadamu Allah (s.w) anatukumbusha katika Qur-an:


Na kwa yakini tulimuumba mwanaadamu kwa udongo ulio safi, kisha tukamuumba kwa tone la manii lililow ekw a katika makao yaliyohifadhika.


Kisha tukalifanya tone hilo kuwa kitu chenye kuning’inia na tukakifanya hicho chenye kuning’inia kuwa pande la nyama, kisha tukalifanya pande hilo la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivisha nyama,kisha tukamfanya kiumbe kingine.


Basi Ametukuka Allah, Mbora w a w aumbaji… (23:12-1 4)
Si tu kuwa mwanaadamu hana mamlaka na kuzaliwa kwake bali pia hana mamlaka na kukua kwake, na kufa kwake kama tunavyokumbushwa tena katika Qur-an:


Enyi watu! Kama mumo katika shaka juu ya ufufuo, basi (tazameni namna tulivyokuumbeni)! Kwa hakika tulikuumbeni kwa udongo, kisha kwa manii, kisha kuwa kitu chenye kuning’inia, kisha kuwa kipande cha nyama kinachoumbika na kisichoumbika, ili tukubainishieni.


Nasi tunakikalisha tumboni tunachokitaka mpaka muda uliowekwa, kisha tunakutoeni kwa hali ya utoto, kisha tunakuleeni mpaka mfikie baleghe yenu. Na kuna wanaokufa (kabla ya kufikia umri huu).


Na katika nyinyi kuna wanaorudishwa katika umri dha lili, asijue chochote baada ya kule kujua kwake… (22:5).
Aya hizi zinatukumbusha na kututhibitishia kuwa kuumbwa kwa mwanaadam, kukua kwake na kufa kwake hufuata utaratibu madhubuti uliowekwa na Muumba wake bila ya hiari yake.
Vile vile ukizingatia ufanyaji kazi wa mwili wa mwanaadamu utagundua kuwa mwili wa mwanadamu ni mashine ya ajabu inayofanya kazi kwa kufuata utaratibu uliofungamana


na sheria madhubuti. Kwa mfano ukichunguza mwili wa mwanaadamu utakuta kuwa kuna mifumo mbali mbali kama vile mfumo wa usagaji chakula (digestion system), mfumo wa hewa (respiratory system), mfumo wa fahamu (nervous system), mfumo wa uzazi (reproduction system) na kadhalika.


Mifumo hii hufanya kazi yake kwa kufuata utaratibu na sheria madhubuti nje kabisa ya mkono wa mwanaadamu. Utaona kuwa mwili wa mwanaadamu hufanya kazi yake na kumwezesha mwanaadamu kuwa katika hali ya uzima alionao, kwa kufuata sheria madhubuti za maumbile zilizowekwa na Muumba wake kama tunavyofahamishwa katika Qur-an:


Basi uelekeze uso wako katika dini iliyo sawa sawa - ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu (yaani dini hii ya Kiislamu inaafikiana bara bara na umbile la binaadamu). Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mw enyezi Mungu. Hiyo ndiyo dini ya Haki, lakini watu wengi hawajui.


(30:30)
Katika aya hii tunajifunza kuwa mwili wa mwanaadamu hufuata dini ya Allah (s.w), yaani hufuata bara bara utaratibu au sharia madhubuti alizoweka Allah (s.w).


Lakini mwanaadamu mwenyewe katika kuendesha maisha yake ya kila siku ana uhuru kamili wa kufuata dini ya Allah (s.w) kwa kufuata kwa ukamilifu na kwa unyenyekevu sharia madhubuti alizoziweka Allah (s.w) katika kukiendea kila kipengele cha maisha (rejea juzuu ya 2 EKP uk. 33 au kufuata dini za watu kwa kufuata utaratibu wa maisha walioufuma watu katika kukiendea kila kipengele) kinyume na utaratibu wa Allah (s.w). Ni katika kuutumia uhuru huu, Allah (s.w) anamtanabahisha mwanaadamu.



Je, wanataka dini isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu na hali kila kilichomo m binguni na ardhini kinam tii yeye, kipende kisipende? Na kwake watarejeshwa wote.


(3:83).
Aya hii inamtanabahisha mwanaadamu ili achukue uamuzi wa busara wa kufuata dini ya Allah (s.w), ambayo dini hiyo ndiyo inayofuatwa na mwili wake na maumbile mengine yote yaliyomzunguka.


Ni dhahiri kwamba atakapoamua kufuata dini nyingine yoyote isiyokuwa dini ya mwili wake, atakuwa ameamua kufuata utaratibu wa maisha unaopingana na umbile lake, na matokeo yake ni kukosa furaha na amani, katika maisha au kuishi maisha ya migongano, vurugu na huzuni.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 442


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Dalili na ishara za jeraha kwenye ngozi
Posti hii inaonyesha dalili,sababu na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa aliyepata jeraha kwenye ngozi kwa kuingiliwa na kitu Kama mwiba,Pini,sindano n.k Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat As-Sajida
Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya? Soma Zaidi...

KUAMINI MALAIKA WA ALLAH (S.W.)
Soma Zaidi...

Makatazo ya kujiepusha nayo
Soma Zaidi...

Dalili Kubwa za kukaribia Siku ya kiama
Soma Zaidi...

Sababu za kutokubalika kwa vitabu vilivyotumwa kuwa muongozo sahihi wa maisha ya mwanadamu zama hizi
Soma Zaidi...

Nini chanzo cha elimu zote na ujuzi wote
Ninichanzo cha Elimu? (EDK form 1 Dhanaya Elimu) Soma Zaidi...

Ni nini maana ya Ilhamu katika uislamu?
Ilhamu ni moja katika njia ambazo Allah huwasiliana na wanadamu na kuwafundisha mambo mablimbali. Soma Zaidi...

Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na sababu zifuatazo
Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na nini? (EDK form 1: mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na sababu zifuatazo) Soma Zaidi...

Maana ya uislamu.
Kwenye kipengele hichi titajifunza maana ya uislamu,na maana nyingine tofauti. Soma Zaidi...

Mitume wa uongo
Wafuatao ni baadhi ya wale waliodai utume wakati Mtume (s. Soma Zaidi...

Kujiepusha na kukaribia zinaa
Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa. Soma Zaidi...