Sifa za waumini wa ukweli katika uislamu

Je unamjuwq ni nani muumini, na ni zipi sifa za muumini?

SIFA ZA WAUMINI

i) Wana yakini kuwa Allah (s.w) yupo
Waumini wa kweli huwa na yakini nyoyoni mwao juu ya kuwepo Allah (s.w) na Mtume wake. Yaani wanashuhudia kwa dhati nyoyoni mwao kuwa Allah (s.w) ni Mola wao pekee na Muhammad (s.a.w) ni Mtume wake wa mwisho na katika matendo yao yote huishi kwa kufuata mwongozo wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na daima hukumbuka msisitizo wa aya ifuatazo:

 

“Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini,Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi (kabisa).” (33:36)

 


(ii)Hum cha Allah (s.w) kwa kutekeleza amri zake
Anapotajwa Mwenyezi Mungu au wanapokumbushwa juu ya maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu, nyoyo zao hunyenyekea na kufuata kama walivyokumbushwa. Hufanya hivyo kwa kuhofu ghadhabu za Mwenyezi Mungu na kutarajia radhi zake.

 


(iii)Huongezeka imani yao kwa kusoma na kufuata Quran
Wanaposoma aya za Mwenyezi Mungu huwazidishia imani. Kwa maana nyingine, waumini wa kweli hufuata mwongozo wa Allah (s.w) katika kuendesha maisha yao ya kila siku. Hawako tayari kufanya jambo lolote kinyume na mwongozo wa Allah (s.w).

 


(iv)Humtegemea Mwenyezi Mungu peke yake
Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu. Wanamsimamo thabiti na hawayumbishwi na yeyote katika kutekeleza wajibu wao kwa Mola wao. Wana yakini kuwa aliyenusuriwa na Allah (s.w) hakuna wa kumdhuru na aliyeandikiwa kupata dhara na Allah (s.w) hakuna wa kumnusuru.

 


(v)Husimamisha swala
Husimamisha swala katika maisha yao yote. Huswali swala tano kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa, na kwa hiyo hufikia lengo la swala kwa kutojihusisha kabisa na mambo machafu na maovu. Na zaidi huamrisha mema na kukataza maovu katika jamii.

 


(vi)Husaidia wenye matatizo katika jamii
Huwa wepesi wa kutoa msaada kwa hali na mali kwa wanaadamu wenziwe wanaohitajia msaada.

 


(vii)Hufanya bias hara na Allah (s.w)
Wanafanya jitihada za makusudi kwa kutumia mali zao na kujitoa muhanga nafsi zao ili kuhakikisha kuwa dini ya Allah inasimama katika jamii. Yaani wanajitahidi kwa jitihada zao zote ili kuzifanya sharia za Allah (s.w) ziwe ndizo zinazotawala harakati zote za maisha ya jamii.
Pia sifa za Waumini zinabainishwa katika Suratul-Muuminuun kama aya zifuatavyo:

 

Hakika wamefuzu Waumini ambao katika swala zao huwa wanyenyekevu.(23:1-2)

 

Na ambao hujiepusha na Lagh-wi (mambo ya upuuzi). Na ambao Zaka wanaitekeleza.(23:3-4)

 


Na ambao tupu zao wanazihifadhi isipokuwa kwa wake zao au kwa (wanawake) wale iliyomiliki mikono yao ya kuume. Basi hao ndio wasiolaumiwa.(23:5-6)

 

Lakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka. Na ambao amana zao na ahadi zao w anaziangalia (23:7-8).

 

Na ambao swala zao wanazihifadhi. Hao ndio w a rith i(2 3:9-10).

 

Ambao watarithi Firdaus (Pepo ya daraja ya juu) wakae humo milele. (23:11)
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa waumini wa kweli waliofuzu na watakaostahiki kupata pepo ya Firdaus, ya daraja ya juu kabisa ni wale wanaojipamba na sifa zifuatazo:


(viii)Wenye khushui katika swala
Waumini wa kweli waliofuzu huwa na khushui (unyenyekevu) katika swala. Yaani huswali kwa kutulizana kimwili, kimoyo,kiroho na kifikra, huku wakizingatia yale wayasemayo mbele ya Mola wao wakiwa na yakini kuwa anawaona na anawasikia.


(ix)Wenye kuhifadhi swala
Waumini wa kweli waliofuzu huhifadhi swala kwa kutekeleza kwa ukamilifu shuruti zote za swala nguzo zote za swala na huswali kama alivyoswali Mtume (s.a.w) na hudumu na

 

swala katika maisha yao yote: Rejea Qur-an (70:23)
Zingatio: Swala husimama kwa kuhifadhiwa na kuswaliwa kwa khushui na kudumu na swala katika maisha yote.


(x)Wenye kuepuka lagh-wi
Waumini wa kweli waliofuzu hujiepusha na Lagh-wi. Lagh-wi ni mambo ya upuuzi yanayomsahaulisha mtu kumkumbuka Mola wake, yanayosababisha ugomvi au bughudha baina ya watu na yanayomsahaulisha mtu kusimamisha swala: Rejea Qur-an (5:91). Mahala ambapo Allah (s.w) hakumbukwi, shetani huchukua nafasi. Michezo yote ni lagh-wi isipokuwa ile tu inayochezwa kwa kuchunga mipaka yote ya Allah (s.w) kwa lengo la kukuza ukakamavu na siha.


(xi)Hutoa Zakat na Sadakat
Waumini wa kweli waliofuzu hutoa Zakat wakiwa na mali na hutoa misaada na huduma waziwezazo kwa wanaadamu wenziwe kwa kadiri ya haja ilivyojitokeza. Asiyejali kuwasaidia binaadamu wenziwe, huku ana uwezo si Muumini. Rejea Qur-an (1 07:1-7).


(xii)Huepuka zinaa na tabia za kizinifu
Waumini wa kweli waliofuzu hujihifadhi na zinaa au hujiepusha kufanya jimai nje ya mipaka aliyoiweka Allah (s.w). Hatua ya kwanza ya kujilinda na zinaa ni kujiepusha na vishawishi vyote vinavyokurubisha watu kwenye zinaa. Muumini wa kweli hutekeleza pasina kusita ile amri ya Allah(s.w) ya katazo kuwa:

 

Wala usiikaribie zinaa; kwa hakika huo ni uchafu na ni njia mbaya kabisa (17:32)


(xiii)Huwa muaminifu
Waumini wa kweli waliofuzu huchunga amana. Hutunza amana aliyopewa na kuirejesha au kuitumia kwa mujibu wa maelekezo ya mwenyewe. Amana kuu aliyopewa mwanaadamu na Mola wake ni kule kufadhilishwa kwake kuliko viumbe vingine vyote ili asimamishe Ukhalifa (utawala wa Allah) katika ardhi kama tunavyokumbu shwa katika Qur-an:

 


“Kwa yakini Sisi Tulidhihirisha amana kwa mbingu, ardhi na milima,vikakataa kuichukua na vikaiogopa,lakini mwanaadamu aliichukua. Bila shaka yeye ni dhalimu mkubwa, mjinga sana ”. (33:72)


(xiv) Wenye kutekeleza ahadi
Hutekeleza ahadi zao wanapoahidiana na wanaadamu wenziwao maadamu ni katika mipaka ya Allah (s.w). Ahadi kubwa wanayotoa Waislamu mbele ya Allah (s.w) ni shahada; pale wanapo ahidi kuwa hawatamshirikisha Allah (s.w) na chochote na kwamba wataishi maisha yao yote kwa kufuata mwongozo wa Allah (s.w) kupitia kwa Mtume wake, Muhammad (s.a.w). Rejea (6: 162 -163)
Katika Suratul-Fur-qaan sifa za Waumini zinabainishwa tena kama ifuatavyo:

 

“Na waja wa Rahmaan; Ni wale wanaokwenda ulimwenguni kwa unyenyekevu; na wajinga wakisema nao (maneno mabaya) huwajibu (maneno ya) salama. (25:63).

 


Na wale wanaopitisha baadhi ya saa za usiku kwa ajili ya Mola wao kwa kusujudu na kusimama. Na wale wanaosema:“Mola wetu! Tuondolee adhabu ya Jahannam, bila shaka adhabu yake ni yenye kuendelea(25 :64-65).

 

Hakika hiyo (Jahannamu) ni kituo kibaya na mahali (pabaya kabisa) pa kukaa ”.Na wale ambao wanapotumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo. (25:66-6 7)

 

Na wale wasiomuomba mungu mwingine pamoja na Allah, wala hawaui nafsi aliyoiharamisha Allah ila kwa haki, wala hawazini; na atakayefanya hayo atapata madhara (papa hapa ulimwenguni).(25:68).

 

Na atazidishiwa adhabu siku ya Kiyama na atakaa humo kwa kufedheheka milele (25:69).

 


Ila yule atakayetubia na kuamini na kufanya vitendo vizuri, basi hao ndio Mwenyezi Mungu atawabadilishia maovu yao kuwa mema; na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa ku reh em u. (25:70).

 

Na aliyetubia na kufanya wema, basi kwa hakika yeye anatubu kw eli kw eli kw a Mwenyezi Mungu.(25:71)

 

Na wale ambao hawashuhudii shahada za uwongo, na wanapopita penye upuuzi, hupita kwa hishima (yao). (25:72)

 

Na wale ambao wanapokumbushwa aya za Mola wao haw aziangukii kw a uziw i na upofu.(25:73)

 


Na wale wanaosema: “Mola wetu! Tupe katika wake zetu na wototo wetu yaburudishayo macho (yetu) (nyoyo zetu), na Utujaalie kuwa waongozi kwa wamchao (Mungu). (25:74).

 

Hao ndio watakaolipwa ghorofa (za Peponi) kwa kuwa walisubiri, na watakuta humo hishima na am ani(25 :75).

 

Wakae humo milele; kituo kizuri na mahali pazuri (kabisa pa kukaa.) (25:76)
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa sifa za Waumini ambao hapa wameitwa “Waja wa Rahman” ni pamoja na:


(xv)Kuishi na watu kwa wema
Waumini wa kweli huishi na watu wema kwa kuwathamini na kuwaheshimu; kujizuia na kuwafanyia watu kibri, kujizuia na kujikweza na kujitukuza mbele ya wengine, kujizuia na kuwadhalilisha watu na kuwavunjia heshima.


(xvi)Huepuka ugomvi na mabishano
Waumini wa kweli huepuka kabisa tabia ya ugomvi na mabishano. Waumini hufahamu fika kuwa kwenye ugomvi na mabishano shetani huwepo na huchochea faraka baina ya ndugu.


(xvii)Hudumu katika kuswali Tahajjud
Kuamka usiku na kuswali swala ya “Tahajjud”(kisimamo cha usiku) kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah (s.w) na Rehema zake. Swala hii huswaliwa usiku wa manane hususan katika theluthi ya mwisho ya usiku inayokaribiana na Al-fajiri.

 

(xviii)Huo gopa adh abu ya Allah (s .w)
Waumini wa kweli huogopa adhabu ya Allah (s.w) aliyowaandalia watu waovu huko akhera kwa kujitahidi kutenda mema na kujiepusha na maovu na kila mara kuomba:

 

“Mola wetu! Tuondolee adhabu ya Jahannam, bila shaka adhabu yake ni yenye kuendelea. Hakika hiyo (Jahannamu) ni kituo kibaya na mahali (pabaya kabisa) pa kukaa ”(25:65)


(xix)Hutumia neema kwa insafu Waumini wa kweli hutumia neema walizopewa na Allah kwa insafu. Hawafanyi ubadhirifu au israfu wa neema kama vile kutumia vibaya mali, wakati, vipaji na ujuzi. Waumini daima huzingatia kuwa Allah hawapendi waja wanaofuja neema alizowatunukia. Mubadhirina ni watu wanaofuja neema walizotunukiwa na Allah (s.w). Wasiotumia neema kwa insafu, ni wafuasi wa shetani. Quran inasema:

 

Na wape jamaa wa karibu haki zao,na mayatima (vilevile) na masikini, w ala usifanye ubadhirifu.(1 7:26).

 

Hakika wafanyao ubadhirifu ni marafiki wa shetani, na shetani ni mwenye kumkufuru Mola wake (17:2 7).


(xx)Hawamshirikishi Allah (s.w)
Waumini wa kweli hawamshirikishi Allah(s.w). Hujiepusha na aina zote za shirk- shirk katika dhati, shirk katika sifa, shirk katika hukumu na shirk katika mamlaka ya Allah(sw). Kufanyah shirk ni dhambi kubwa ya daraja la kwanza. Quran inaonya na kutahadharisha kuwa:

 

Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi (dhambi ya) kushirikishwa na kitu na husame yasiyokuwa haya kwa amtakaye. Na anayemshirikisha Allah bila shaka amebuni dhambi kubwa. (4:48).


(xxi)Hulinda na kutetea haki uhai wa nafsi
Waumini wa kweli hulinda na kutetea haki ya uhai wa kila nafsi yenye haki ya kuishi. Hivyo, kwa namna yeyote ile ya kisheria, hujitahidi kujiepusha na ushiriki wa kusababisha au kufanya mauwaji ya nafsi ambayo kwa mujibu wa mwongozo wa Allah hustahiki kuishi. Ulinzi na utetezi huu wa haki ya uhai wa nafsi unatokana na mwongozo wa Allah katika Quran kuwa:

 

Mwenye kuiuwa nafsi pasina nafsi (hiyo iliyouliwa kuuwa) au kufanya fisadi katika ardhi,huyo itakuw a kana kwamba ameuwa watu wote. Na atakayeilinda nafsi hiyo, huyo atakuwa kana kwamba amelinda uhai wa watu wote(5:32).


(xxii)Hawafanyi uzinzi
Waumini wa kweli hawaikaribii zinaa wala kufanya uzinifu. Na zaidi hawashawishi wala kushiriki kwa namna yoyote ile katika mambo yanayosababisha zinaa kufanyika.

 

“Wala usikaribie zinaa. Hakika hiyo ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa).” (17:32). 63

 

(xxiii)Husema kweli daima
Waumini wa kweli husema kweli daima. Hawatowi ushahidi wa uongo au kutetea batili. Wanapowajibika kutoa ushahidi juu ya jambo, husema ukweli hata kama ni dhidi ya nafsi zao wenyewe au watu wao wa karibu.(rej 4:135, 5:8)


(xxiv)Hawavutiwi na mambo ya kipuuzi
Waumini wa kweli ni wale ambao hawavutiwi na mambo ya kipuuzi ambayo wafuasi wa ibilisi huyatumia katika kuwavuta watu kwa lengo la kuwapumbaza na kuwateka akili zao. Muumini huwa hana muda wa kupoteza au fursa ya kuikabidhi akili yake kwa twaghuti aichezee. Hivyo, kwenye mambo ya kipuuzi waumini hupita haraka kwa heshima zao, na ikibidi kuweka jambo m-badala lenye maana na manufaa kwa jamii.


(xxv)Hum witikia Allah (s .w) an apowaita
Waumini wa kweli humwitikia Allah (s.w) anapowaita kwa makatazo na maamrisho yake katika Quran. Hivyo hutii kwa unyenyekevu maagizo ya Allah (s.w) kila wanapokumbushwa kwa kusomewa au kusoma wenyewe aya za Kitabu cha Allah (s.w). na Allah (s.w) ananadi katika Quran kuwa:

 

Na waja wangu wanapokuuliza kuhusu mimi, basi (w aambie) hakika Mimi nipo karibu najibu maombi ya mwombaji pindi anaponiomba. Basi na waniitike na waniamini Mimi ili wapate kuongoka (2:186)


(xxvi)Hujenga familia za kiislamu
Waumini hujitahidi kujenga familia za kiislamu kwa kumuongoza mke na kuwalea watoto na wale wote walio chini ya mamlaka yake katika mipaka ya Ucha-Mungu kwa kuwaamrisha kutenda mema na kuwakataza maovu. Pamoja na jitihada hiyo huomba msaada wa Allah kwa kuleta dua ifuatayo:

 


“Mola wetu! Tupe katika wake zetu na wototo wetu yaburudishayo macho (yetu) (nyoyo zetu), na Utujaalie kuwa Viongozi kwa wamchao (Mungu). (25:74).
Kwa ujumla waumini wa kweli ni wale wanaojipamba na tabia njema kama iliyoelekezwa katika Qur-an na Sunnah.

 



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/15/Thursday - 11:21:39 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1167


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Nini maana ya Iqlab katika hukumu za tajwid
Hapa utajifunza maana ya iqlab katika usomaji wa Quran kwa tajwid Soma Zaidi...

Nafasi ya Elimu katika uislamu
Elimu imepewa kipaumbele kikubwa kwenye uislamu. Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu nafasi ya Elimu katika uislamu. Soma Zaidi...

Mtazamo wa uislamu juu ya Elimu, nini maana ya elimu na nani aliye elimika.
Ni nini maana ya Elimu na ni nani aliye elimika? Uislamu una mtazamo gani juu ya Elimu? Soma Zaidi...

Mtazamo wa kikafiri juu ya maana ya dini.
Maana ya dini kwa mujibu wa makafiri ina utofauti mkubwa na vile ambavyo uislamu unaamini kuhusu dini. Soma Zaidi...

Hukumu za waqfu na Ibtida
waqfu ni misimamo ambapo msomaji wa Quran anaruhusiwa kusimama, kuhema au kumeza mate. Na ibtidai ni kuanza baada ya kutoka kwenye waqf Soma Zaidi...

Njia ambazo Allah hufundisha wanadamu elimu mbalimbali
Ni kipi chanzo cha Elimu, na ni kwa namna gani Allah hufundisha Elimu kwa wanadamu? Soma Zaidi...

Kwa nini uislamu umeipa elimu nafasi ya kwanza
Elimu imepewa nafasi kubwa sana katika uislamu. Soma Zaidi...

Mgawanyiko wa Elimu katika mtazamo wa Uislamu
Katika Uislamu elimu imegawanyika katika Elimu ya muongozo na elimu ya mazingira. Soma Zaidi...

Kwa namna gani Allah huwasiliana na wanadamu kwa kupitia ndoto.
Ndoto za kweli ni moja kati ya njia ambazo Allah huwasiliana na wanadamu. Soma Zaidi...

Kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila dini?
Mwanadamu hawezi kuishi bila dini, kwani dini imekusanya mfumo mzima wa maisha yake. Soma Zaidi...

Ni nini maana ya Ilhamu katika uislamu?
Ilhamu ni moja katika njia ambazo Allah huwasiliana na wanadamu na kuwafundisha mambo mablimbali. Soma Zaidi...

Sifa za waumini wa ukweli katika uislamu
Je unamjuwq ni nani muumini, na ni zipi sifa za muumini? Soma Zaidi...