Endapo muislamu hatafunga mwezi wa Ramadhani bila ya ruhusa je atatakiwa afanye nini. Je ataweza kuilipa funga hiyo?
Hukumu ya Muislamu Aliyeacha Kufunga kwa Makusudi
Japo kadha ya Ramadhani inaruhusiwa kwa yule aliyeruhusiwa kutofunga kutokana na udhuru wa kisheria, kadha haitajuzu kwa mtu aliyeacha makusudi, kwani hata akifunga mwaka mzima hawezi kuilipia siku hiyo moja aliyoacha kufunga pasi na udhuru kwa ushahidi wa Hadith ifu atayo:
Abu Hurairah (r.a) amesema kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Mwenye kula siku moja ya Ramadhani bila ya ruhusa iliyotolewa na Mwenyezi Mungu, basi Swaum hiyo hailipiki hata akifunga mwaka mzima. (Abu, Daud, Ibn Majah n a Tirm idh).
Fundisho kubwa tunalolipata hapa ni kuwa kuacha makusudi kutekeleza amri ya Allah katika wakati wake uliowekwa ni jambo baya sana hata kama utatekeleza amri hiyo wakati mwingine. Ikumbukwe kuwa anachokiangalia Allah (s.w) si utekelezaji wa vitendo tu, bali huangalia na kumlipa mja kutokana na utii na unyenyekevu katika kufanya kitendo alicho kiamrisha.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Uislamu ndio dini pekee ambayo inatoa ufumbuzi juu ya suala la riba.
Soma Zaidi...Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kuhusu zakat al fitiri, kiwango chake, watu wanaostahili kupewa na kutoa, pia umuhimu wake katika jamii.
Soma Zaidi...Uchumi wa uislamu umeweka taratibu mbalimbali katika kuchuma mali.
Soma Zaidi...