Hapa utajifunza namna ambayo utatakiwa kulipa funga ya Ramadhani kwa siku ambazo hukufunga
Kulipia Ramadhani
Mtu anapodaiwa siku alizo kula katika mchana wa mwezi wa Ramadhani,au siku ambazo swaumu yake ilibatilika, si lazima azilipe mara tu baada ya Ramadhani, japo ni bora mtu kumaliza deni lake haraka. Tunafahamishwa katika Hadith kuwa Bibi ‘Aysha (r.a) alikuwa akilipia Ramadhani katika mwezi wa Shaaban:
Aysha (r.a) ameeleza: “Nilikuwa na madeni ya swaumu ya Ramadhani. Sikuweza kulipa kadha ila katika mwezi wa Shaaban. (Bukhari na Muslim).
Hali kadhalika si lazima mtu kulipa mfululizo siku zote anazodaiwa, bali anaweza kuzilipa kidogo kidogo kutokana na Hadith ifuatayo:
Ibn Umar (r.a) ameeleza kwamba Mtume (s.a.w) amesema juu ya kulipa Ramadhani: (Mtu) akitaka na afarikishe; na akitaka na afululize. (Daru Qu tni).
Kama mtu amechelewa kulipa siku anazodaiwa mpaka Ramadhani nyingine ikaingia, basi kwanza ataifunga hiyo Ramadhani iliyomuingilia. Baadaye ndipo alipe hiyo deni yake wala halipi fidia; iwe kuchelewa huko ni kwa udhuru ama si kwa udhuru. Lakini ni vizuri zaidi kulipa siku anazodaiwa kabla ya kuingia Ramadhani nyingine.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza faida za ndoa katika Jamii na kwa wanadamu kiafya, kiroho, kiuchumi
Soma Zaidi...Hii ni orodha ya watu ambao wanaweza kurithi malibya marehrmu.
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunza mambo ambayo ni haramu kwa mwanamke aliye na hedhi na nifasi
Soma Zaidi...Tumesha mzika maiti sasa imebakia mali yae nyumbani, watoto, wake na menginyeo.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkutayamamu.
Soma Zaidi...