Watu wanaolazimika kufunga mwezi wa Ramadhani


image


Hapa utajifunza watu ambao wanalazimika kufunga mwezi wa Ramadhani.


Waislamu Wanaolazimika Kufunga Ramadhani

(i)Wenye akili timamu
Kila ibada katika Uislamu inamtaka mja awe hadhiri (conscious) wakati wa kuifanya. Hivyo mwendawazimu au punguani hatalazimika kufunga au kufanya ibada yoyote ile, hana thawabu mbele ya Allah (s.w) kwa jema atakalolifanya na hatapata dhambi kwa ovu atakalolifanya.

 


(ii)Waliofikia Baleghe
Kwa mtazamo wa Uislamu mtu huhesabiwa kuwa amekua kiakili na kuweza kutumia vizuri uhuru wake wa hiari anapofikia baleghe. Baleghe hufikiwa na mtoto wa kiume au wa kike anapokuwa na umri wa miaka 15 au kwa mtoto wa kiume kuota na kutokwa na manii na kwa mwanamke kuanza kupata hedhi hata kama hawajafikia umri wa miaka 15. Muislamu anapokuwa baleghe huhesabiwa kuwa ni mtu mzima mwenye kulazimika kutekeleza kila amri ya Uislamu, hivyo hesabu yake ya amali njema na mbaya huanza kuingizwa katika kitabu chake tangu wakati huo. Hivyo mtoto ambaye hajafikia baleghe halazimiki kufunga kama tunavyofahamishwa katika Hadith ifuatayo:

 


Ali (r.a) ameeleza kwamba Mtume (s.a.w) amesema: “(Watu) watatu wameondolewa kalamu (hawaandikiwi dhambi) Mwenda wazimu mpaka arudiwe na akili, aliyelala mpaka aamke, na mtoto mpaka abaleghe.” (Ahmad, Abu Daud, Tirmidh).

 


Pamoja na kwamba watoto ambao hawajabaleghe hawalazimiki kufunga, wanatakiwa wazoeshwe kufanya hivyo tangu wangali wadogo. Walifanya hivyo masahaba wa Mtume (s.a.w) kama tunavyofahamishwa katika Hadith ifuatayo:

 


Rubayyi bint Mu ’awwidh (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) alimtuma mtu mmoja asubuhi siku ya Ashura, kwenda vijiji vya Answaar (na ujumbe huu): Aliyeamka na hali amefunga basi na akamilishe swaumu yake. na aliyeamka na hali amekula, basi na afunge sehemu iliyobaki ya siku

 

yake. Tukawa tunaifunga siku hiyo (ya Ashura) baada ya hapo, na kuwafungisha watoto wetu wadogo. Tukienda msikitini tulikuwa tukiw atengenezea vitu vya kuchezea vya sufi. Mm oja w ao akililia chakula, tukimpa vitu hivyo (vya kuchezea) mpaka ufike wakati wa kufungua (kufuturu). (Bukhari na Muslim).

 


Si katika ibada ya funga tu tunapotakiwa tuwazoweshe watoto wetu, bali katika kila ibada na kila mwenendo mwema. Katika Hadith nyingine Mtume (s.a.w) ametuagiza tuanze kuwazoesha watoto wetu kufanya hizi ibada maalum kama vile kuswali na kufunga wanapokuwa na umri wa miaka saba na wanapofikia umri wa miaka kumi tuwalazimishe kwa viboko endapo watazichenga ibada hizi.

 


(iii) Wenye afya
Wanaolazimika kufunga ni wale wenye afya nzuri. Wagonjwa wameruhusiwa kutofunga kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:

 

“... Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi (atimize hesabu) katika siku nyingine ...” (2:185).
Mgonjwa akijiona hana afya ya kumuwezesha kufunga au kama anatakiwa kunywa dawa mchana, basi anaruhusiwa kutofunga. Lakini mgonjwa akijiona kuwa anaweza kufunga bila ya kuathirika anaruhusiwa kufunga. Hapa Muislamu amepewa uhuru wa kuamua kufunga au kutofunga kulingana na anavyojisikia yeye mwenyewe. Lakini iwapo Muislamu atafunga kwa kujikalifisha atakuwa amehalifu amri ya Allah (s.w), japo funga yake inaweza kukubalika. Allah (s.w) katika Qur-an anatuasa:

 

“... Wala msijiue, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kukuhurumieni.” (4:29).
Pia baada ya Allah (s.w) kutoa ruhusa ya kutofunga wasafiri na wagonjwa, anaonyesha huruma zake kwa kutufahamisha:

 


“... Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi w ala hakutakieni yaliyo mazito, na pia (anakutakieni) mtimize hisabu hiyo, na (anakutakieni) kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongozeni, ili mpate kushukuru. ” (2:185).

 


Mgonjwa atakayetumia ruhusa hii analazimika kulipa siku alizokula katika miezi mingine atakapokuwa mzima. Mama wajawazito au wale wanaonyonyesha, wakaona kuwa hawataweza kufunga kwa kuhofia afya zao na watoto wao, nao wanaruhusiwa kutofunga Ramadhani na wanalazimika kulipa siku walizokula katika miezi mingine. Wazee vikongwe na wagonjwa wale ambao hawategemei kupona kama vile wagonjwa wa kisukari, ambao hawawezi kufunga katika mwezi wowote ule, watatoa fidia kwa kuwalisha maskini kwa kutoa kibaba kimoja cha chakula kinachopendelewa na wakazi wa mji, au kutoa thamani yake kwa kila siku ya mwezi wa Ramadhani kama Qur-an inavyoelekeza:

 

“... Na wale wasioweza, watoe fidiya kwa kumlisha maskini ...” (2:184).

 


(iv) Wakazi wa Mji

 


Muislamu anayekutwa na Ramadhani akiwa ametulia katika mji ni lazima afunge.
“(... Atakayekuwa katika mji) atakapoushuhudia mw ezi (wa Ramadhani) afunge .... ” (2:185).

 


Kwa upande mwingine msafiri ameruhusiwa kutofunga kama tunavyojifunza katika Qur-an:
“...Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hesabu (ya siku alizoacha kufunga) katika siku nyingine ...” (2:185).

 


Katika aya hii msafiri anaruhusiwa kutofunga akipenda. Pia anaweza kufunga akipenda. Uhuru wa kufunga au kutofunga uko kwa msafiri mwenyewe. Tunajifunza katika Hadith mbali mbali kuwa hawakuwa Maswahaba wote wakifunga walipokuwa safarini wala hawakuwa wote wanakula katika msafara huo huo mmoja. Hebu turejee Hadith zifuatazo:

 


‘Aysha (r.a) amesimulia kuw a Hamza bin ‘Amr Al’Hisham (r.a) alimuuliza Mtume (s.a.w) juu ya funga katika safari: “Ewe Mtume wa Allah, mimi nina nguvu za kufunga katika safari. Je nina kosa (nikifunga)? “Akajibu (Mtume):’Hiyo ni ruhusa kutoka kwa Allah, atakayeichukua vema. Na anayependa kufunga hana kosa. ” (Muslim).

 


Katika Hadith nyingine Sayyid al-Khudri (r.a) ameeleza:
“Tuliungana na Mtume (s.a.w) katika vita vya Jihad, mwezi 16 Ramadhani. Miongoni mwetu walifunga na wengine hawakufunga. Aliyefunga hakumuona ana makosa yule asiyefunga na yule asiyefunga hakumtia makosani yule aliyefunga.” (Muslim).

 


Kama msafiri kutokana na mazoea yake kuhusu safari hiyo, hapana shida yoyote atakayoipata iwapo atafunga, basi ni vema afunge kwa kuzingatia ushauri wa Mtume (s.a.w) katika Hadith ifuatayo:

 


“Salman bin Al-Musabbiq(r.a) amesimulia kuwa mtume wa Allah amesema: Yule ambaye atakuwa anasafiri na mnyama ambaye atamfikisha mahali ambapo atapata chakula cha kutosha, na afunge pop ote pale Ramadhani itakapomkuta ” (Abu Daud).

 


Hadithi hii haiondoi ruhusa ya kutofunga katika safari bali inamrahisishia msafiri kuchukua uamuzi wa kufunga pale ambapo ana usafiri wa uhakika utakaomwezesha kupata futari na daku. Lakini iwapo Muislamu ataanza safari yake akiwa amefunga, kisha katikati ya safari atapatwa na matatizo ni vema afungue kama tunavyojifunza katika Hadith zifu atazo:

 


Anas (r.a) ameeleza: Tulikuwa na Mtume (s.a.w) safarini. Miongoni mwetu w alifunga na miongoni mw etu haw akufunga. Tulitua mahali katika siku ya joto (jua kali). Wale waliofunga walianguka chini (hawakujijua) na wale ambao hawakufunga walibakia imara. Walikita mahema yao na kuwanywesha ngamia wao. Mtume (s.a.w) akasema:“Wale ambao haw akufunga w anatoka na thaw abu leo zaidi kuliko wale w aliofunga).” (Bukhari na Muslim).

 


Jabir (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah alikuwa safarini. Aliona kundi la watu na mtu mmoja aliyelazwa kivulini.Akauliza: “Kuna nini?” Wakamjibu: “Mtu aliyefunga ”. Akasema (Mtume): “Kufunga katika safari si faradhi.” (Bukhari na Muslim).

 


Umbali gani wa safari Muislamu anaruhusiwa kutofunga? Hapana masafa maalum ya safari yaliyowekwa kama kipimo cha kufunga au kutofunga katika safari. Hili nalo limeachwa huru kwa msafiri mwenyewe kutegemeana na njia ya usafiri atakayoitumia. Safari yoyote ile ambayo mtu anaruhusiwa kupunguza swala, pia ameruhusiwa kutofunga.

 


Hali kadhalika, msafiri atakapokuwa ugenini anaruhusiwa kula kwa muda wa siku anazoruhusiwa kupungaza swala zake. Tunazidi kusisitiza kuwa uamuzi wa kufunga au kutofunga utategemea hali atakayoikuta msafiri huko ugenini. Iwapo atafika mahali ambapo anapata futari na daku yake pasina wasiwasi ni vyema afunge. Kama huko ugenini patakuwa na wasiwasi wa kupata mahitaji haya, basi ni vyema kutofunga mpaka anaporejea nyumbani. Jambo muhimu la kuzingatia ni kwamba, msafiri atalazimika kukamilisha siku alizokula katika miezi mingine.

 


(v) Kwa Mwanamke, asiwe katika Hedhi wala Nifasi
Mwanamke aliye katika hedhi au nifasi ni haramu kwake kufunga, na analazimika kufunga siku alizoacha tofauti na swala kama tunavyojifunza katika Hadith ifu atayo:
‘Aysha (r.a) amesema: Tulikuwa tukipata hedhi wakati wa Mtume (s.a.w) tukaamrishwa kulipa saum wala hatukuamrishwa kulipa swala.” (Bukhari na Muslim).



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu       ðŸ‘‰    2 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    3 Madrasa kiganjani offline       ðŸ‘‰    4 Download App zetu hapa ujifunze zaidi    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Uzuri wa Benki za kiislamu
Kwa nini benki za kiislamu ni bora kuliko benki nyingine? Soma Zaidi...

image Mambo muhimu ya kuzingatia katika kujenga uchumi wa kiislamu
Nazingatio muhimu katika uchumi unaofuata sheria za kiislamu. Soma Zaidi...

image Mambo ambayo hayafunguzi funga
Hii ni orodha ya mambo ambayo hayawezi kuharimu funga yako endapo utayafanya. Soma Zaidi...

image Mgawanyiko katika kuitumia mali unayomiliki
Unajuwa namna ambavyo matumizi ya mali yako, yanavyogawanywa? Jifunze hapa mgawanyiko wa mali yako. Soma Zaidi...

image Taratibu za mahari katika uislamu
Hapa utajifunza taratibu za kutaja mahari katika uislamu. Soma Zaidi...

image Hukumu ya kufinga kwa kifuata kuandama kwa mwezi
Ni muda gani unatakiwa ufunge ramadhani, je kuandama kwa mwezi kwa kiona ama hata kusiki. Soma Zaidi...

image Ni nini maana ya twahara na kujitwaharisha?
Posti hii inakwendabkukujiulisha maana ya twahara na jinsi ya kujitwaharisha. Soma Zaidi...

image Jinsi ya kuswali kuswali swala ya maiti
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya maiti, nguzo za swala ya maiti, sharti za swwla ya maiti na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...

image Jinsi ya kukaa itiqaf na taratibu zake
Hapa utajifunza kuhusu taratibu za ibada ya itiqaf yaani kukaa msikitini kwa ajili ya ibada. Soma Zaidi...

image Jinsi ya kuoga josho la kiislamu ( janaba, hedhi na nifasi)
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kuoga josho kisheria. Soma Zaidi...