Mazao ambayo inapasa kutolewa zaka

Mazao ambayo inapasa kutolewa zaka

(i) Mazao ya Shambani



Mazao yote yanayolimwa shambani, yanastahiki kutolewa Zakat kutokana na amri ya Allah(s.w) katika aya zifuatazo:


Naye (Mwenyezi Mungu) ndiye aliyeiumba miti inayoegemezwa (katika chanja katika kuota kwake), na isiyoegemezwa, na (akaumba) mitende na mimea yenye matunda mbali mbali, na (akaumba) mizaituni na mikomamanga inayofanana na isiyofanana. Kuleni matunda yake inapotoa matunda na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake (kwa kuwapa maskini na jamaa na majirani na wengineo). Wala msitumie kw a fujo, hakika Mw enyezi Mungu) haw apem ndi w atum iao fujo. (6:141).


Aya hizi zinatuthibitishia kuwa mazao yote yatokayo shambani yakiwa ya chakula au ya biashara yanalazimu kutolewa Zakat. Haya ni pamoja na mazao yote ya aina ya mbegu, aina zote za matunda, mazao ya aina ya mizizi, mazao ya biashara kama vile katani, kahawa, pamba, chai, pareto, n.k. Pia kutokana na Hadithi ifuatayo hata asali inapaswa kutolewa Zakat:



Abu Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Juu (ya Zakat) ya asali: Kwa kila chupa kumi (za ngozi) chupa moja itolewe Zakat”.



Nisaab ya mazao ya shambani



Nisaabu ya mazao ya shambani imeelezwa katika Hadithi ifuatayo:
Abu Said al-Khudri (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Hapana Zakat kwa mbegu au tende mpaka zifikie kiasi cha wasaq tano. (Nisai).



Katika Hadith hii tunafahamishwa kuwa mazao ya shambani yanayostahiki kutolewa Zakat ni yale yaliyofikia ‘wasaq’ tano na hapana Zakat chini ya hapo. Katika kipimo tulichokizoea wasaq 1 = kilo 133.2, hivyo wasaq 5 = kilo (5 x 133.2) = kilo 666. Kwa hiyo mtu akiwa na mazao ya shambani yaliyofikia uzito wa kilo 666 itambidi atoe (Zakat) kiasi cha kilo 66.6 (nusu wasaq) na kama yamemwagiliwa maji atatoa kiasi cha kilo 33.3 (robo wasaq).



Kwa hiyo, mazao yote yanayopimwa kwenye pishi au kwenye kilo yapimwe na kutolewa Zakat iwapo yatakuwa yamefikia Nisaab. Jambo lingine muhimu katika utoaji wa Zakat ya mazao ya shambani ni kwamba si lazima utoe mazao yale yale bali unaweza ukayathamanisha kwa fedha taslim(cash) kulingana na bei ya zao hilo kwa wakati uliopo.



Kiasi cha Zakat ya mazao ya shambani



Kima cha mazao kinachotakiwa kutolewa Zakat kimebainishwa katika Hadith ifuatayo:



Abdullah bin Umar (r.a) ameeleza kutoka kwa Mtume (s.a.w) kuwa amesema: ‘Kuna moja ya kumi (1/ 10) kutokana na mazao yaliyonyeshewa na mvua au maji ya chemchem (mto) au yaliyostawi kwenye ardhi yenye rutuba. Na kuna nusu ya moja ya kumi (1/20) kutokana na mazao yaliyonyweshwa kwa kutumia ngamia. (Bukhari).



Katika Hadith hii tunafahamishwa kuwa kiasi cha kutoa kwa mazao ya shambani ni moja ya kumi (1/ 10) au (10%) ya mavuno yote, iwapo mazao hayo yalistawishwa kwa njia ya kawaida ya kutegemea mvua au kunyweshelezwa kwa maji ya mto, au chemchem yanayotiririka yenyewe bila ya kutumia zana na nguvu ya kuyavutia. Kwa upande mwingine, iwapo mazao ya shambani yatastawishwa kwa kunyweshelezwa kwa gharama za mabomba, mashine, mikokoteni, kima cha Zakat kitapungua na kuwa moja ya ishirini (1/ 20) au (5%) ya mavuno yote.



Atta bin ‘Usaid (r.a) ameeleza kuw a Mtume (s.a.w) amesema: Katika Zakat ya Zabibu, zabibu zitapimwa kwa kipimo kile kile cha tende na Zakat yake italipwa baada ya kukaushwa kama Zakat ya tende inavyolipwa baada ya kukaushw a. (Tirmidh, Abu Daud).



Hadith hii inatufahamisha kuwa Zakat itolewe baada ya kuvuna na kukausha kwa yale yanayowekeka yakiwa yamekauka. Vile vile ieleweke kuwa kutajwa tende na zazibu katika Hadithi hii na Hadithi nyingine mbali mbali haina maana kabisa kuwa tende na zabibu ndio matunda pekee yanayotolewa Zakat kama wengi wetu wanavyojaribu kuelewa, bali mazao haya yametajwa mara kwa mara katika Hadith mbali mbali kwa kuwa ndiyo yaliyokuwa katika mazingira ya Mtume Muhammad (s.a.w) na jamii ya Waislamu aliokuwa nao.Ukweli ni kuwa mazao yote yanayolimwa shambani yanastahiki kutolewa Zakat kwa ushahidi wa aya za Qur-an. Rejea Qur-an (6:141) na (2:267).
Muda wa kutoa Zakat ya mazao ya shambani ni mara tu baada ya mavuno. Hata kama utalima au kuvuna mara mbili au mara tatu zote. Ndio kusema Zakat ya mavuno haingoji kumalizika mwaka.




                   


Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1849

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana: