2.
2. Kusoma Dua ya Kufungulia Swala
Kusoma dua ya kufungulia swala ni sunnah. Katika Hadithi ya Bukhari na Muslim iliyosimuliwa na Abu Hurairah (r.a), baada ya kuhirimia swala Mtume (s.a.w) alikuwa akileta dua ifuatayo: โwajahtu wajhi lilladhi fatwaras-samaawat wal-ardha hanifam-muslima wamaa ana minal-mushrikina. Inna swalatiy wanusukii, wamah-haya, wamaamatiy, lillahi rabil-alamiina laa sharikalahu wabidhalika umirtu wa-ana minal-muslimina.โโNimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi. Nimeacha dini za upotovu. Mimi si miongoni mwa washirikina. Hakika swala yangu (na ibada zangu zote) na uzima wangu na kufa kwangu (yote) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, bwana (Rabbi) wa walimwengu wote. Hana mshirika wake. Na haya ndio niliyoamrishwa na mimi ni wa kwanza walio jisalimisha kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu. (6:79, 162-163)
3. Kupiga Audhu Billah Kabla ya kuanza kusoma Qur-an ni amri ya Allah (s.w) kujikinga na sheitwani kama inavyodhihirika katika aya ifuatayo: 109 โNa ukitaka kusoma Qur-an piga Audhu billah (jikinge) kwa Allah (akulinde) na Sheitwani aliyefukuzwa (kwenye Rehema). (16:98) Hivyo tuanze kusoma Qur-an kwa kusema โAโudhu-billahi minash-shaytwanir- Rajiimโ Najikinga kwa Allah na sheitwan aliyefukuzwa-kwenye Rehma yako
4. Kusoma Suratul-Fatiha Kusoma Suratul-Fatihah ni nguzo ya tatu ya swala na ndio nguzo kubwa ya swala. Tunasoma suratul-Fatiha kama ifuatavyo:- Bismillahir Rahmaanir Rahiim (1) Alhamdu liLLahi rabbil-โAalamiin (2). Rrahmaanir Rahiim (3) Maaliki yaumiddiin (4) Iyyaakana โabudu waiyyaaka nastaโiin (5) Ih dinasw-swiraatwal mustaqiim (6) Swiraatwa lladhiina an โamta โalaihim; ghairil maghdhuubi โalaihim wala dhw-dhwaaliin (7)
Tafsri:
(1) Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye kurehemu: (2) Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola wa Walimwengu wote: (3) Mwingi wa Rehema mwenye kurehemu (4) Mwenye kumiliki siku ya malipo: (5) Wewe tu ndiye tunayekuabudu, na wewe tu ndiye tunaye kuomba msaada: (6) Tuongoze njia iliyonyooka: (7) Njia ya wale uliowaneemesha; siyo (ya wale ) waliokasirikiwa, wala ya wale waliopotea
5. Kusoma Qur-an baada ya Suratul-Fatiha Katika rakaa ya kwanza na ya pili ni Sunnah baada ya kusoma Suratul-Fatiha kuleta Surah au aya nyingine za Qur-an:
Umeionaje Makala hii.. ?
Hspa utajifunza taratibu za kuonana na mchumba katika uislamu.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...ุนููู ุฃูุจูู ููุนูููู ุดูุฏููุงุฏู ุจููู ุฃูููุณู ุฑูุถููู ุงูููู ุนููููู ุนููู ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู ููุงูู: "ุฅููู ุงูููููู ููุชูุจู ุงููุฅูุญ...
Soma Zaidi...Umuhimu wa KusimamishaSwala Kwa mujibu wa Hadith ya Ibn Umar (r.
Soma Zaidi...Lugha ya Swala Lugha ya swala,kuanzia kwenye Takbira ya kuhirimia Swala mpaka kumalizia swala kwa Salaam, ni Kiarabu.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha namna ya kutwaharisha Najisi.
Soma Zaidi...Fahamu darsa mbalimbali za fiqh kama swala, twahara, zaka pamoja na funga. Zijuwe sharti za swala, funga na zaka.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kuhusu taratibu za ibada ya itiqaf yaani kukaa msikitini kwa ajili ya ibada.
Soma Zaidi...