Mali inayojuzu kutolewa Zakat, Nisaab na kiwango cha ZakatAina ya mali inayojuzu kutolewa Zakat imeelezwa kwa wazi katika


Qur-an na Hadith sahihi. Mali inayojuzu kutolewa Zakat ni ile iliyofikia au kuzidi kima maalum kiitwacho Nisaab na kubakia katika milki ya mwenye hiyo mali kwa kipindi chote cha mwaka mmoja. Kila aina ya mali ina nisaab yake, Nisaab ni kiwango cha mali kinachostahiki kitolewe Zakat. Aina ya mali inayojuzu kutolewa Zakat ni:(i)Mazao yote ya shambani
(ii)Wanyama wafugwao kwa ajili ya chakula
(iii)Dhahabu (gold), fedha (silver), au fedha taslim (cash)
(iv)Vito (mapambo ya dhahabu na fedha)
(v)Madini na mali ya kuchimbuliwa chini ya ardhi au mali ya kuokota
(vi)Mali ya biashara