Zaka ya mapambo ya dhababu na fedha, mali ya bishara na mali iliyofukuliwa ardhini
(iv)Vito (mapambo )vya Dhahabu na Fedha
Mapambo ya dhahabu na fedha yameharamishwa kwa Waislamu Wanaume. Wanawake wenye mapambo ambayo kiasi cha dhahabu au fedha kilichopo kwenye mapambo hayo kinafikia Nissab,wanalazimika kutoa Zakat kila mwaka unapopindukia.
Zainab mke wa Abdullah(r.a) ameeleza: Mtume wa Allah alituhutubia na akasema: “Enyi jumuia (mkusanyiko wa) wa wanawake! Toeni Zakat hata kutoka kwenye mapambo yenu, kwa sababu katika wakazi wa motoni mtakuwa w engi zaidi katika siku ya Kiyama ” (Tirmidh).
Amr bin Shuaib(r.a) amesimulia kutoka kwa baba yake na baba yake alisema kuwa wanawake wawili walikuja kwa Mtume (s.a.w) na bangili mbili za dhahabu wamevaa mikononi mwao Mtume aliwauliza “mmelipa Zakat yake” ‘Hapana’, walijibu. Kisha Mtume (s.a.w) akawauliza: ‘Mngetaka kwamba Allah awavalishe bangili za moto?’ ‘Hapana ’ walijibu. Alisema (Mtume): “Basi lipeni Zakat yake ” (Tirmidh).
(v)Mali yakuchimbuliwa chini ya ardhi au mali ya kuokota
Mali iliyofukuliwa chini au madini hutolewa ushur au Zakat kiasi cha moja ya tano (1/5 au 20%) ya thamani ya mali hiyo kama tunavyofahamishwa katika Hadith.
Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “... Na kuna moja ya tano (1/5) inayolazimu kutolewa Zakat kutokana na mali iliyo chini ya ardhi”. (Bukhari na Muslim).
Hadith hii inatufahamisha kuwa mali yoyote iliyochimbuliwa chini ya ardhi ambayo haikuwa na mmiliki yoyote kabla ya hapo, itakuwa ni halali kwa aliyeigundua na kuichimbua lakini atalazimika kutoa ushuru au kiwango cha Zakat kiasi cha 1/ 5 au 20% ya mali hiyo. Hali kadhalika mali yoyote ya kuokota iliyokosa mwenyewe baada ya kutangazwa kwa muda mrefu wa kutosha unaokubalika katika sharia ya kiislamu inakuwa ni mali ya mwenye kuokota, na atalazimika kuitolea Zakat kiasi cha 1/5 au 20% ya mali hiyo. Mali ya kuchimbuliwa chini au mali ya kuokota haina Nisaab wala haina muda bali Zakat yake hutolewa pale pale inapopatikana.
(vi)Mali ya Biashara
Bidhaa za biashara pamoja na fedha taslimu zinatakiwa zihesabiwe na kutolewa Zakat baada ya mwaka kupindukia.
Samura bin Jundab (r.a) ameeleza: Mtume wa Allah alikuwa akituelekeza tukusanye Zakat kutoka kwenye vile tulivyovihesabu kama bidhaa (za biashara). (Abu Daud).
Bidhaa za biashara zitatolewa Zakat kwa kuthamanishwa na fedha taslim kwa kiasi cha 1/40 au 2.5% ya mali yote ya bidhaa zote za biashara. Kwa hiyo mali ya biashara nisaab yake itakuwa sawa na nisaab ya fedha au dhahabu. Tofauti na dhahabu, fedha na fedha taslim ambazo hutolea Zakat baada ya kukaa kwa kipindi cha mwaka mmoja, bidhaa za biashara si lazima zikae kwa kipindi cha mwaka mmoja ndio ijuzu Zakat juu yake bali kila mwisho wa mwaka, mfanyabiashara atahesabu bidhaa zake zote anazozifanyia biashara na kuzitolea Zakat kwa kiwango cha 2.5%. Hapana Zakat juu ya vifaa vinavyotumika kwa matumizi ya nyumbani au vitendea kazi. Kwa mfano, nyumba za kufanyia kazi kama vile maduka, ofisi, na hoteli, mashine za kufanyia kazi, samani za nyumbani, ofisini dukani, hotelini, n.k. magari ya kusafiria na kusafirishia bidhaa, vyote hivi havistahiki kutolewa Zakat.
Kwa msisitizo zaidi Zakat inajuzu tu kwa mali inayotengenezwa kwa ajili ya kuuzwa au mali inayonunuliwa kwa ajili ya kuuzwa; kwa mfano magari yaliyonunuliwa au nyumba zilizotengenezwa kwa ajili ya kuuzwa zitatolewa Zakat kila mwisho wa mwaka.Jambo muhimu linalotakiwa lizingatiwe kabla ya kutoa Zakat ni madeni. Ni sharti madeni na haki nyingine zote za watu zitolewe ndio mali ihesabiwe kwa ajili ya Zakat.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 845
Sponsored links
👉1
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2
Madrasa kiganjani
👉3
kitabu cha Simulizi
👉4
Simulizi za Hadithi Audio
👉5
Kitabu cha Afya
👉6
Kitau cha Fiqh
Namna ya Safari ya Hija inavyoanza
Soma Zaidi...
NI KWA NINI TUNASWALI?, NI UPI UMUHIMU WA KUSWALI NA NI ZIPI FADHILA ZA KUSWALI
Umuhimu wa KusimamishaSwala Kwa mujibu wa Hadith ya Ibn Umar (r. Soma Zaidi...
Msimamo wa uislamu juu ya utumwa
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Nini maana ya twahara katika uislamu
Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya twahara katika uislamu. Pia utakwenda kujifunza hukumu za twahara, aina za twahara na mambo mengineyo Soma Zaidi...
maana ya Eda na aina zake
Ni kipindi au muda wa kungojea mwanamke aliyepewa talaka (aliyeachwa) au kufiwa na mumewe kabla ya kuolewa na mume mwingine. Soma Zaidi...
haki na wajibu katika jamii
Soma Zaidi...
nyakati za swala
3. Soma Zaidi...
Kutoa kati kwa kati
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Njia haramu za uchumi.
Njia hizi ni haramu katika kukuza uchumi wako. Soma Zaidi...
Ni zipi sifa za imamu wa swala?
Soma Zaidi...