(b)Najisi Kubwa:
Najisi hii imeitwa kubwa kutokana na uzito unaochukuliwa katika kujitwah aris ha.
Namna ya kujitwaharisha kutokana na najisi ya mbwa na nguruwe ni kuikosha sehemu hiyo mara saba na mojawapo katika hayo makosho saba iwe kwa kusugua kwa udongo safi. Hivi ndivyo Mtume (s.a.w) alivyotufundisha kama inavyobainika katika Hadithi zifu atazo:
Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Kutw aharisha chombo cha yeyote kati yenu, baada ya kulambwa na mbwa ni kukikosha mara saba, ukitumia udongo katika safari ya kwanza. (Muslim)
Ibn Mughafal amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) aliamuru kuuawa mbwa (wenye ugonjwa au wasio na waangalizi) kisha akaulizwa: “Vipi juu ya mbwa wengine?” Kisha akaruhusu kufuga mbwa kwa ajili ya kuwindia, kuchungia (na ulinzi kwa ujumla) na akasema: Mbwa atakapolambachombo, kioshe mara saba na kisugue na udongo kwa mara ya nane”. (Muslim)
Hadithi hizi zinatupa msimamo wa Uislamu juu ya mbwa, ufugaji wake na namna ya kujitwaharisha kutokana na naye. Tumejifunza kuwa japo mbwa ni mnyama najisi tunaruhusiwa kumfuga kwa ajili ya kuwindia, na ulinzi wa nyumbani. Kama itabidi tufuge mbwa kwa ajili ya madhumuni haya, tutalazimika kuwafunza na kuwatayarishia makao yao yasiyohusiana na watu kwa malazi, chakula au ukaribu wowote.
Katika utafiti uliofanywa na Daktari mmoja huko Marekani (1978) iligundulika kuwa mbwa (na nguruwe) ni wachukuzi wa vijidudu vya magonjwa mbali mbali. Baadhi ya vijidudu hivyo havifi kwa dawa yoyote isipokuwa udongo