Mwenendo wa Mtu aliyetoa Shahada
Muislamu aliyetoa shahada ya kweli hanabudi kumfanya Mtume (s.
Mwenendo wa Mtu aliyetoa Shahada
Muislamu aliyetoa shahada ya kweli hanabudi kumfanya Mtume (s.a.w) kuwa kiigizo chake kimwenendo na kitabia. Mtume (s.a.w) alikuwa na tabia njema kabisa kama tunavyofahamishwa katika Qur’an:
|
“Na bila shaka (Wewe Muhammad) una tabia njema kabisa.” (68:4) |
Mtume (s.a.w) mwenyewe amewahimiza waumini kujipamba na tabia njema kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:
Abdullah bin Amr (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Aliye kipenzi changu kuliko wote katika nyinyi (Wa is lam u) ni yule aliyew azidi kwa tabia njema”. (Bukhari)
Harithat bin Wahab (r.a) ameeleza kuwa Mtume w a Allah amesema: “Yule ambaye tabia yake ni mbaya na katili, hataingia Peponi”. (Abu Daud)
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuw a Mtume w a Allah amesema: “Mw enye imani iliyopea katika Waislamu ni yule mwenye tabia njema, na aliye mbora katika nyinyi ni yule anayemtendea wema mkewe”. (Tirmidh)
Abu Darda (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Hapana kitu kitakachotia uzito katika m izani ya Muum ini katika siku ya hukum u kuliko tabia njema...” (Tirmidh)
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) aliulizwa juu ya mambo yatakayopelekea watu wengi kuingia Peponi. Alijibu Mtume: “Uchaji - Mungu na tabia njema”. Kisha akaulizwa tena: “Ni mambo yepi yatakayompelekea m tu kuingizw a Motoni? ” Alijibu Mtum e, “Mdom o n a tup u (viungo vy a s iri)”. (Tirm idh)
Hivyo, muumini wa kweli hanabudi kujipamba na vipengele vya tabia njema vilivyoainishwa katika Qur-an na Sunnah. Katika juzuu hii
tumerejea vipengele vya tabia njema vifuatavyo:
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 web hosting 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
NI ZIPI SWALA ZA SUNNAH: (qabliya (kabliya) na baadiya, tahajudi, tarawehe, qiyamu layl, shukr, istikhara)
Sunnah za SwalaSunnah za Swala Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi.
Soma Zaidi...JIFUNZE FIQH
Fahamu darsa mbalimbali za fiqh kama swala, twahara, zaka pamoja na funga. Zijuwe sharti za swala, funga na zaka.
Soma Zaidi...Tofauti ya uchumi wa kiislamu na uchumi wa kikafiri
Uchumi wa kiislamu unatofautiana sana na uchumi wa kikafiri. Hapa utajifunza tofauti hizo.
Soma Zaidi...Hutuba ya Ndoa - Khutbat nikah
Hii ni hutuba ya ndoa kwa ufupi, Imekusanya mambo ya msingi yanayohitajika katika hutuba ya ndoa
Soma Zaidi...Nini maana ya twahara katika uislamu
Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya twahara katika uislamu. Pia utakwenda kujifunza hukumu za twahara, aina za twahara na mambo mengineyo
Soma Zaidi...