picha

Misingi ya fiqh

Kwenye kipengele hichi tutajifinza vyanzo mbalimbali vya sheria ua kiislamu.

  1. Qur’an.

-  Ndio chem. chem. kuu ya sheria za Kiislamu.

    Rejea Qur’an (13:37) na (13:39).

 

2.Sunnah (Hadith).

- Ni msingi wa pili unaotokana na mwenendo wa Mtume (s.a.w) katika kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu (s.w).

Rejea Qur’an (53:2-4), (3:31-32), (33:21) na (59:7).

 

3.Ijtihad (Qiyaas na Ijmaa).

- Ni hali ya kufanya jitihada katika kufafanua sheria na hukumu mbali mbali za Kiislamu zilizomo katika Qur’an na (Sunnah) Hadith za Mtume (s.a.w) kwa misingi ya ‘Qiyaas’ na ‘Ijmaa’.

Qiyaas.

Maana yake ni kuyapatia hukumu mambo yasiyo na hukumu ya moja kwa moja katika Qur’an na Sunnah kupitia misingi sahihi ya sheria, hukumu na kanuni zilizopo katika Qur’an na Sunnah..

 

Ijma’a.

Maana yake ni maafikiano ya wanachuoni (wanataaluma) wa Kiislamu katika kutoa hukumu juu ya jambo fulani lisilo na hukumu ndani ya Qur’an au Hadith kwa kupitia misingi ya Qur’an au Sunnah (Hadith).

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2021/12/22/Wednesday - 10:29:29 am Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 3703

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉6 web hosting   

Post zinazofanana: