Ni nini maana ya swala
Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu maana halisi ya ibada ya swala.
Maana ya Swala
(a)Kilugha
Katika lugha ya Kiarabu neno “Swalaat” lina maana ya “ombi” au “dua”. Katika Qur-an tunaamrishwa kumswalia Mtume, yaani kumuombea dua Mtume (s.a.w) katika aya ifuatayo:
“Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamswalia Mtume (w anamtakia Rehema). Basi, enyi mlioamini mswalieni (muombeeni au mtakieni Mtume) Rehema na muombeeni amani”. (33:56)
Vile vile katika Hadith, Mtume (s.a.w) anatuambia:
“Yule atakayealikwa kwenye karamu ya harusi aitikie wito huo, kama hataweza kuitika amswalie (amuombee dua) aliyemkaribisha. ” (Muslimu)
(b)Kisheria
Katika sheria ya Kiislamu, “swalaat” ni maombi maalumu kwa Allah (s.w) yanayofanywa kwa kufuata utaratibu maalumu uliowekwa na Allah (s.w) na kufundishwa kwa matendo na Mtume wake. Katika maombi haya maalumu mwili mzima huhusika katika maombi haya kwa kusimama, kurukuu, kuitidali, kusujudu, kukaa na kuzingatia yale yote anayosema katika kuleta maombi haya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 ai web app 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Ni zipi najisi katika uislamu
Post hii inakwenda kukupa orodha ya vitu vilivyo najisi.
Soma Zaidi...Jukumu la serikali katika kuzuia dhuluma
Serikali ina nafasi kubwa katika kuzuia dhulma na kufanya uchumibuwe huru kuyokana na dhulma.
Soma Zaidi...