Nini maana ya Kushahadia nguzo ya kwanza ya uislamu

Nini maana ya Kushahadia nguzo ya kwanza ya uislamu

Kutoa Shahada Mbili

Kwa mujibu wa Hadith, tuliyoirejea katika utangulizi, nguzo ya kwanza ya Uislamu ni kutoa shahada mbili kwa kusema:Ash hadu an laailaha illa llaahu wa ash hadu anna Muhammadar Rasuulu llahi

Tafsiri:

Nashuhudia kuwa hapana mungu ila Allah na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah.

Shahada ndio kiingilio cha Uislamu. Yaani wasiokuwa Waislamu, wakiamua kuingia katika Uislamu, hukaribishwa na Waislamu kwa kutamkishwa hizi shahada mbili. Ukweli ni kwamba mtu hatakuwa Muislamu kwa kutamka tu haya maneno ya shahada bila ya kufahamu maana ya ndani.Maana ya Shahada ya Kwanza:

“Nashuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah”

Maana yake ni kwamba, huyu mja baada ya uchunguzi wa kina kwa kuzingatia dalili mbali mbali zinazodhihiri katika umbile la mbingu na ardhi na vyote vilivyomo, katika nafsi ya mwanaadamu, katika historia ya mwanaadamu, katika maisha ya Mitume na mafundisho yao, anayakinisha moyoni mwake kuwa yuko Mungu Muumba, Mpweke, Mwenye Uwezo juu ya kila kitu na Mmiliki wa kila kitu. Baada ya kuwa na yakini hii, huyu mja sasa anatoa ahadi kwa Allah(s.w) na kwa walimwengu wote kuwa, hatakuwa na mwingine yeyote atakaye muabudu au atakayemtii katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake kinyume na Allah (s.w).Kwa maana nyingine mja anayetoa shahada hii, anaahidi kuwa ataendesha maisha yake yote ndani ya mipaka aliyowekewa na Allah (s.w) katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kibinafsi na kijamii. Yaani wenye kumshuhudia Allah kikweli ni wale wanaofuata Uislamu katika kila kipengele cha maisha yao kama Allah (s.w) anavyowaamrisha katika aya zifuatazo:“Enyi Mlioamini! Ingieni katika Uislamu wote (katika hukumu zote za Uislamu) wala msifuate nyayo za Shetani, kwa hakika yeye kwenu ni adui aliye dhahiri”. (2:208).“Enyi m lioam ini! Mcheni Mw enyezi Mungu kam a ipasavyo kum cha; w ala msife isipokuwa mmekwishakuwa Waislamu kamili”. (3:102). 

Maana ya Shahada ya Pili

“Na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah”

Hii ndio sehemu ya pili ya shahada ambayo huikamilisha shahada ya kwanza. Labda swali litaulizwa: “Kumshuhudia Mtume Muhammad (s.a.w) kunakamilishaje shahada ya kwanza?” Tumeona kuwa maana halisi ya kumshuhudia Allah (s.w) ni kumuabudu Allah pekee katika kila kipengele cha maisha yetu.Tutamuabudu vipi Allah (s.w) katika kila kipengele cha maisha yetu? Tutajuaje ni yepi aliyoyaharamisha Allah na yepi aliyoyahalalisha? Ni njia ipi tuifuate ili tupate radhi zake na ipi tuiepuke ili tuepukane na ghadhabu zake? Tutajuaje ipi njia sahihi na ipi potofu? Yote haya hatuwezi kuyajua mpaka tupate muongozo kutoka kwa Allah (s.w) mwenyewe.Utaratibu aliouweka Allah (s.w) katika kuwaongoza wanaadamu ni kuwaleta Mitume miongoni mwa wanaadamu wanaume ambao huwaletea mwongozo na kuwafanya Waalimu wajuzi wenye hekima ili wawafundishe wanaadamu wenzao kinadharia na kimatendo juu ya Allah (s.w) na namna ya kumuabudu. Hivyo ili mja aweze kumjua Allah (s.w) na kumuamini ipasavyo na kisha aweze kumuabudu inavyostahiki katika kila kipengele cha maisha yake, hanabudi kwanza kumuamini Mtume na kufuata mafundisho yake. Kwahiyo, sisi watu wa Umma huu wa Mtume wa mwisho, hatuwezi kuwa Waumini wa kweli wa Allah (s.w) bila ya kumshuhudia Mtume Muhammad (s.a.w) kuwa ni Mtume wa Allah (s.w).Kumshuhudia Muhammad (s.a.w) kuwa ni Mtume wa Allah (s.w), ni kutoa ahadi kuwa utafuata mafundisho ya Mtume (s.a.w) vilivyo kwa kutekeleza yale yote aliyoyaamrisha na kuacha yale yote aliyoyakataza na kumuigiza mwenendo na tabia yake kama inavyosisitizwa katika Qur’an:

“Sema ( Muhammad kuwaambia watu): ‘Ikiwa nyinyi mnampenda Mw enyezi Mungu, basi nifuateni; (hapo)Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakughufirieni madhambi yenu.Na Mwenyezi Mungu ni mwenye Maghufira na Mwenye Rehema ”. (3:31)“...Na anachokupeni Mtum e basi pokeeni na anachokukatazeni jiepusheni nacho. Na muogopeni Mw enyezi Mungu; kwa yakini Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu”. (59:7)“Bila shaka mnao mfano mw ema kw a Mtume wa Mw enyezi Mungu kw a mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho, na kumtaja Mwenyezi Mungu sana ”. (33:21)

Kwahiyo, Muumini anapotoa shahada mbili anaahidi kwa dhati ya moyo wake kuwa atamtii Allah(s.w) na Mtume Muhammad (s.a.w) kwa unyenyekevu kwa kukiendea kila kipengele cha maisha ya kibinafsi na ya kijamii kwa mujibu wa mwongozo wa Qur-an na Sunnah ya Mtume (s.a.w). Mtu hatakuwa Muumini pale atakapoendesha maisha yake ya kibinafsi au ya kijamii kinyume na shahada kama tunavyokumbushwa katika aya ifuatayo:“Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake w anapokata shauri,

w awe na hiari katika shauri lao. Na Mw enye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu uliowazi.” (33:36).                   Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1872


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Isa(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Isa(a. Soma Zaidi...

Sifa za wanafiki zilizotaja katika surat An-Nisaa (4:60-63, 88, 138-145)
Huwaoni wale wanaodai kwamba wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako? Soma Zaidi...

Ni kwa nini lengo la Funga na swaumu halifikiwi na wafungaji?
Kwa nini Lengo la Funga halifikiwi na Wafungaji Wengi? Soma Zaidi...

DUA ZA KUONDOA WASIWASI
DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah. Soma Zaidi...

Kuwa na mwenye haya, na faida zake
24. Soma Zaidi...

DUA ZA WAKATI WA HASIRA
DUA ZA WAKATI UNAPOKUWA NA HASIRA. Soma Zaidi...

Tathmini ya swala zetu, kwa nini swala zetu hazijibiwi?
Soma Zaidi...

HISTORIA YA BI KHADIJA (HADIJA) MKE WA KWANZA WA MTUME MUHAMMAAD (S.A.W)
HISTORIA YA BI KHADIJABi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara. Soma Zaidi...

MAADILI MEMA KATIKA UISLAMU
Yajuwe maadili mema yaliyotajwa katika quran Soma Zaidi...

kuwa mwenye huruma na faida zake
25. Soma Zaidi...

familia
Soma Zaidi...

Misingi na Maadili Katika Uislamu
5. Soma Zaidi...