image

Sifa za kuwa maamuma kwenye swala na namna ya kumfuata imamu

Post hii inakwenda kukuelezea sifa za kuwa maamuma na taratibu za kumfuata imamu.

Kumfuata Imamu

Wanaoswalishwa (Maamuma) ni lazima wafuate amri ya Imamu na wasimtangulie Imamu kwa hali yoyote itakayokuwa. Msisitizo wa kumfuata Imamu vilivyo umewekwa bayana katika Hadithi zifuatazo:

 


Anas (r.a) amesimulia. Mtume wa Allah siku moja aliwaongoza katika sw ala. Alipomaliza swala yake alitugeukia na kusema: “Enyi w atu ”Mimi ni Imamu wenu. Kwa hiyo msin itangu lie katika kuinama (rukuu), wala katika kusujudu, wala katika kusimama wala katika kutoa salaam, kwa sababu ninakuoneni kwa mbele yangu na nyuma yangu” (Muslim).

 


Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Usijaribu kumtangulia Imamu. Soma takbira (Allahu Akbar) baada yake, na sema, “Amiin” baada ya yeye kusema “Ghairil-magh’dhuubi a’layhim waladhwaaliin” na anaporukuu nawe rukuu na anaposema: “Sami’allaahu limanhamidah” sema: “Allahuma Rabbana lakal-hamdu”.(Bukhari na Muslim).

 


Anas (r.a) amesimulia: Mtume wa Allah alipanda farasi akaanguka na kuumia upande wake wa kulia. Aliswali swala mojawapo ya swala (tano) akiwa amekaa, nasi pia tuliswali tukiwa tumekaa nyuma yake. Alipomaliza kuswali alisema: Imamu amechaguliwa ili afuatwe. Akiswali akiwa amesimama, nanyi swalini mkiwa mmesimama, anaporukuu nanyi mrukuu anapoinuka (kuitidali) nanyi inukeni, anaposema, “Samia Llaahu limanhamidah ”, semeni “Rabbana lakal hamdu ”. (Bukhari)

 


Abu Hurairah (r.a) amehadithia kuwa Mtume wa Allah amesema, Je, haogopi yule anayetanguliza (anayeinua) kichwa chake mbele ya (kwa kumtangulia) Imamu.Haogopi kwamba, Allah atageuza kichwa chake kuwa kichwa cha punda? (Kwa maana nyingine kuwa na kichwa cha punda ni kuwa na kichwa kisicho na uwezo wa kufikiri kama kile cha punda). (Bukhari na Muslim).

 


Hadithi zote hizi zinaonesha umuhimu wa kumfuata Imamu vilivyo katika swala za Jamaa. Funzo la ujumla tunalolipata hapa, ni kuwa kiongozi wa Kiislamu ni lazima atiiwe endapo atakuwa anatekeleza wajibu wake kulingana na mipaka ya Qur-an na Sunnah. Kuvunja amri ya kiongozi iliyo katika mipaka ya Qur-an na Sunnah ni kuvunja amri ya Allah na Mtume wake. Msisitizo huu wa kuwatii viongozi kwa mnasaba huu tunaupata katika Qur-an:

 

Enyi mlioamini, Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka juu yenu, walio katika nyie (Waislamu wenzenu). Na kama mkikhitalifiana juu ya jambo lolote basi lirudisheni kw a Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Hiyo ndiyo kheri, nayo ina matokeo bora kabisa. (4:59).

 


Je, Ni lazima Maamuma kurudia kusoma suratul Faatiha baada ya Imamu?

 

Pamekuwa na kutofautiana watu juu ya maamuma kurudia kusoma suratul-Faatiha baada ya Imamu kusoma katika swala za kusoma kwa sauti. Baadhi ya watu wanasema ni lazima kurudia kusoma suratul-Fatiha kwa sababu ya Hadith ya Mtume (s.a.w) iliyosisitiza kuwa “Hapana swala bila ya suratul-Faatiha”.
Kwa mujibu wa Qur-an na Sunnah hapana haja kwa maamuma kurudia tena kusoma suratul-Faatiha baada ya Imamu kusoma na wote wakaitikia “aamin” kwa hoja zifuatazo:

 


Kwanza, kitendo cha kuitikia “aamin” inaashiria kuwa Maamuma alishiriki kuisikiliza suratul-Faatiha wakati Imamu anasoma. Kama ilivyo katika kusoma dua za pamoja, mmoja kati yetu huongoza katika kusoma dua na wengine tuliobakia tunaitikia “aamin”. Hivyo, kwa namna hii suratul-Faatiha itakuwa imepatikana kwa Imamu aliyesoma na kwa maamumah waliomsikiliza na kumfuatilia wakati anasoma, na kisha wote kwa pamoja wakaitikia “aamin”.

 


Pili, ni amri ya Allah (s.w) kunyamaza na kuzingatia wakati Qur-an inasomwa:“Na isomwapo Qur-an isikilizeni na nyamazeni ili mpate kurehemew a” (7:204).
Kwa mujibu wa aya hii tunajifunza mambo mawili:

 


(1)Tunalazimika kuwa watulivu na kumfuatilia Imamu kwa makini wakati anasoma suratul-Faatiha.
(2)Ulazima wa kutulizana na kumsikiliza Imamu uko pale pale atakapokuwa anasoma sura au aya baada ya suratul-Faatiha. Hivyo kusoma suratul-Faatiha wakati Imamu anaendelea kusoma Qur-an baada ya suratul Faatiha ni kukhalifu amri ya Allah (s.w).

 


Tatu, kunyamaza kwa baadhi ya Maimamu ili kuwapa maamuma wasaa wa kusoma suratul-Faatiha, si utaratibu uliofuatwa na Mtume (s.a.w). Ni kweli kuwa, ni sunnah kutulia kidogo baada ya kusema “aamin” kabla ya kuanza kusoma sura au aya nyingine za Qur-an katika rakaa ya kwanza na ya pili kwa swala za kusoma kwa sauti, lakini si kimya kirefu kiasi cha kumaliza kusoma suratul-Faatiha kwa utulivu na unyenyekevu.

 


Nne, kama suala ni maamuma kurudia kusoma suratul-Faatiha kwa kuwa Mtume (s.a.w) kasema “Hapana swala bila suratul-Faatiha”, mbona tunajua kutokana na hadithi sahihi kuwa rakaa hupatikana kwa kumkuta Imamu katika rukuu na kujituliza naye pale bila hata ya kuisikia hiyo suratul-Faatiha ikisomwa na imamu.

 


Hivyo kwa mujibu wa hoja hizi zilizojengwa juu ya msingi wa Qur-an na Sunnah, maamuma hahitaji kurudia suratul-Faatiha bali analazimika kunyamaza na kumsikiliza imamu kwa makini na kwa unyenyekevu wakati anaposoma surah hiyo na kisha kuitikia “aamin” baada ya kumaliza. Kisha maamuma ataendelea kumsikiliza imamu kwa makini na kwa unyenyekevu wakati akisoma sura au aya nyingine baada ya suratul-Faatiha.

 


Ama kwa swala au rakaa zile ambazo imamu anasoma kimyakimya, maamuma atalazimika kusoma suratul-Faatiha na sura au aya nyingine baada yake kwa kimya kimya kama anavyofanya katika kuleta visomo mbalimbali katika swala.

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1597


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Funga za kafara, aina zake na sababu za funga hizi za kafara na hukumu zake
Soma Zaidi...

Kuwapa wanaostahiki
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

haki na wajibu kwa watumishi wa nyumbani (house boy and house girl)
Soma Zaidi...

Kutoa kati kwa kati
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Zijuwe Suna zinazofungamana na swaumu na funga ya ramadhani
Soma Zaidi...

Jinsi ya kuoga josho la kiislamu ( janaba, hedhi na nifasi)
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kuoga josho kisheria. Soma Zaidi...

Kujiepusha na ria na masimbulizi
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Swala ya maiti, namna ya kuiswali, nguzo zake, sharti zake na suna zake, hatua kwa hatua
Soma Zaidi...

Nini maana ya najisi, na ni zipi Najisi katika uislamu na aina za najisi
Soma Zaidi...

Kwanini funga imefaradhishwa mwezi wa ramadhani
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

haki na hadhi za mwanamke katika jamii inayoishi kiislamu
Soma Zaidi...

TOFAUTI KATI YA MAKATOZO NA MAAMRISHO KATIKA SUNNAH
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ صَخْرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْت رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم يَقُولُ: "م... Soma Zaidi...