(c) Najisi Hafifu:
Najisi hafifu ni mkojo wa mtoto mdogo wa kiume chini ya miaka miwili ambaye hajaanza kula chakula ila maziwa tu. Uhafifu wa najisi hii hupatikana katika kutwaharisha. Tofauti na najisi ndogo, najisi hafifu hutwaharishwa kwa kumwagia maji tu ile sehemu iliyonajisika bila ya kusugua. Hivi ndivyo alivyofanya Mtume (s.a.w) kama tunavyojifunza katika hadith ifuatayo:
Aysha (r.a) amesimulia kuw a mtoto mchanga wa kiume aliyekuwa angali ananyonya aliletwa kwa Mtume (s.a.w) aliagiza maji na kuyamiminia juu ya pale palipo kojolewa ”. (Muslim)
Hadathi Ndogo
Kuwa katika hadathi ndogo ni kuwa katika hali ya kutokuwa na udhu na huondolewa hadathi hiyo kwa kutia udhu baada ya kuzingatia na kutekeleza kwa ukamilifu masharti na nguzo za udhu.