Kuzika-namna ya kuzika hatua kwa hatua

Kuzika-namna ya kuzika hatua kwa hatua

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Kuzika.

 

-    Waislamu (watu) wataongozana nayo mpaka kaburini kimya kimya.

-    Jeneza lisitanguliwe na watu (msafara).

-    Haitakiwi watu kukaa kabla ya jeneza kukalishwa chini.

 

-    Kaburi liwe pana na kina cha kutosha, mtu kuweza kusimama na kunyoosha mkono kama kuna uwezekano.

-    Kisha lichimbwe shimo dogo (mwana ndani) upande wa Qibla ndani ya kaburi.

-    Urefu na ukubwa wa kaburi unategemea na ukubwa wa maiti.

 

  1. Waingie watu kaburini kwa idadi ya witiri; 3, 5, 7, n.k.
  2. Jeneza liwekwe upande wa kaburi itakapokuwa miguu ya maiti.
  3. Maiti itolewe na kutanguliza kichwa kuelekea kaburini.
  4. Wapokeaji kaburini watamuweka magotini mwao ili kufungua kamba kichwani, tumboni na miguuni. Pia watafunua shavu la kulia ili liguse ardhini (mchanga) atakapolazwa ndani ya mwana-ndani.

 

  1. Maiti italazwa katika mwana-ndani kwa ubavu wa kulia na kuelekezwa Qibla. Wakati wa kuilaza ni sunnah kusema, 

Kama ilivyosimuliwa na Ibn Umar (r.a) kuwa, Mtume (s.a.w) alipokuwa akizika alikuwa akisema: 

        “Bismillaah wabilahi wa’alaa millati Rasuulullaahi”         

        Tafsiri:

“Kwa jina la Allah na kwa uwezo wa Allah na kwa mujibu wa mwenendo wa Mtume wa Allah.” (Ahmad, Tirmidh, Ibn Majah).

 

  1. Maiti ipindishwe miguuni na kichwani ili uso na miguu iweze kugusa kuta za mwana-ndani. Kifua, tumbo na sehemu za katikati zibinuliwe nyuma kidogo.

 

  1. Maiti iwekewe mawe au udongo nyuma ya kichwa na miguu isibinuke. Pia ni sunnah kusoma aya za Qur’an (2:1-5) au (2:285-286).

 

  1. Baada ya maiti kulazwa na kusomewa aya hizi, ifunikwe kwa ubao na kama kuna matundu ya kupitisha udongo pazibwe kwa majani.

 

  1. Kabla kaburi halijafunikwa, vitupiwe viganja vitatu vya udongo, na kila tupo unasoma aya ya Qur’an (20:55).
    • Tupo la 1: “Min-haa khalaq-naakum” – Kutokana na hii (ardhi) tumekuumbeni.
    • Tupo la 2: “Wa fiyhaa nughiydukum” – Na humo (katika ardhi)                          tutakurudisheni.
    • Tupo la 3: “Wa min-haa nukhrjukum taaratan-ukhraa” – Na humo 

                      (katika ardhi) tutakutoweni mara nyingine.

 

  1. Kaburi lijazwe udongo mpaka lijae na kuinuliwa kiasi cha shiburi moja na kuwekewa alama miguuni na kichwani au kupanda miti mibichi.

-  Ni vizuri kumiminia maji juu yake ili kuepusha vumbi kupeperushwa na upepo.  

- Ni haramu kujengea kaburi kwa namna yeyote ile, kukaa juu   yake, kuwasha taa

   juu yake na kuielekea wakati wa kuswali.

‘Jabir (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amekataza kuyajengea makaburi   au kuyajengea nyumba juu yake au kukaa juu yake’. (Muslim)

 

Abu Marsad Al-ghafariyyi ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: 

     “Msikae juu ya makaburi na wala msiswali kwa kuyaelekea.” 

                    (Muslim)

 

        -  Baada ya kuzika Mtume (s.a.w) alikuwa akisimama na kusema: 

            “Muombeeni msamaha ndugu yenu na muombeeni awe

                na kauli thabiti kwani sasa anaulizwa”

 

        -  Ni sunnah baada ya mazishi kuwapa mikono wafiwa na kuwausia subira

            Rejea Qur’an (2:155-156).

        -  Pia haifai kusema (kusengenya) mabaya ya marehemu.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views: 2862

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 web hosting     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 ai web app     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zinazofanana:

Tofauti kati ya fiqh na sheria

Kipengele hichi tutajifunza tofauti kati ua fiqh na sheria.

Soma Zaidi...
namna ya kuswali 6

Lugha ya Swala Lugha ya swala,kuanzia kwenye Takbira ya kuhirimia Swala mpaka kumalizia swala kwa Salaam, ni Kiarabu.

Soma Zaidi...
Swala ya jamaa.

Kipengele hiki tutajifunza kusimamisha swala ya jamaa,swala za ijumaa.

Soma Zaidi...
Watu hawa huruhusiwi kuwaoa katika uislamu

Hapa utajifunza watu ambao ni halali kuwaoa na wale ambao ni haramu kuwaoa.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kiswali swwla ya dhuha na faida zake

Post hii inakwenda kukufunza kuhusu swala ya dhuha, faida zake wakati wa kuiswali swala ya dhuha na jinsi ya kuiswali.

Soma Zaidi...