image

Njia za kujitwaharisha, na vitu vinavyotumika kujitwaharisha

Post hii inakwenda kukufundisha njia zinazotumika kujitwaharisha.

Chakujitwah aris hia

Nafsi ya mtu hutwaharika kwa mtu huyo kumuamini Allah (s.w) ipasavyo na kufuata mwongozo wake katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kibinafsi na kijamii.
Muislamu atatwaharika kutokana na Najisi na Hadath kwa kutumia maji safi au udongo safi kwa kufuata masharti na maelekezo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

 

Sifa za Maji Safi
Maji safi kwa mtazamo wa twahara ni yale yanayofaa kujitwaharishia yaliyogawanyika katika makundi yafuatayo:

(a)Maji Mutlak (maji asili)
Maji yoyote katika hali yake ya asili ni maji safi yanayofaa kujitwaharishia. Maji asili (natural water) ni maji ya mvua, chem chem, visima, mito, maziwa na maji ya bahari.

 


(b)Maji mengi:

Maji mengi ni maji yaliyokusanywa au yaliyokusanyika pamoja na kuwa na ujazo wa mabirika (qullatain) au ujazo usiopungua madebe 12. Mfano wa maji mengi yaliyokusanywa ni maji ya mapipa yenye ujazo wa lita 240, maji ya mabirika (matangi) maalum yaliyojengwa kuhifadhia maji msikitini na nyumbani. Mfano wa maji mengi yaliyojikusanya ni yale ya madimbwi makubwa yanayojikusanya wakati wa mvua.

 


Maji mengi hayahabiriki upesi. Hayaharibiki kwa kujitwaharishia ndani ya chombo kilichoyakusanya au ndani ya mkusanyiko huo wa maji. Pia maji mengi hayaharibiki kwa kuingiwa na najisi. Bali maji mengi yatakuwa hayafai kujitwaharishia iwapo yatabadilika asili yake katika rangi au utamu (ladha) au harufu.

 


(c)Maji machache:

Maji machache ni yale yaliyokusanywa katika chombo au yaliyojikusanya katika ardhi yakiwa na ujazo chini ya Qullatain* au chini ya ujazo wa pipa lenye ujazo wa madebe 12 au chini ya ujazo wa lita 224. Mfano wa maji machache ni ya ndoo, maji ya mtungi na maji yaliyojikusanya kwenye vidimbwi vidogo vidogo wakati wa mvua.

 


Maji machache hayatafaa kujitwaharishia iwapo

 


(i)yataingiwa na najisi japo kidogo sana.
(ii)Iwapo yatakuwa yametumika katika kujitwaharishia humo humo kwa kuondoa najisi au Hadath.
(iii)Iwapo yatakuwa yametumika kwa kufulia au kuoshea vyombo au kuogea humo humo.
(iv)Iwapo yataingiwa na kitu kikayabadilisha asili yake katika rangi, harufu au tamu(ladha).

 


Kutokana na haya tunajifunza kuwa, tunapokuwa na maji machache hatuna budi kuwa waangalifu wakati wa kuyatumia ili tusiyaharibu. Tusijitwaharishe ndani ya vyombo vilivyohifadhia maji hayo, bali tuyateke na kujitwaharisha mbali nayo. Kwa mfano tunakoga kwa kutumia kata na tunatawadha kwa kutumia kopo au birika.

 


(d)Maji makombo

Maji makombo ni maji yaliyonywewa na binaadamu au mnyama yakabakishwa.Maji makombo yanafaa kujitwaharishia ila yale yaliyonywewa na kubakishwa na mbwa au nguruwe.


 

Udongo safi

Udongo safi ni ule ulioepukana na najisi na ukabakia katika asili yake na kutochanganyika na kitu kama vile unga, majivu au vumbi la mkaa, vumbi la mbao (saw dust) n.k. kwa kawaida udongo wote katika ardhi ni safi.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 867


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Madhara ya riba kwenye jamii
Haya ni madhara ya riba katika jamii. Ni kwa namna gani jamii inadhurika kutokana na riba? Soma Zaidi...

namna ya kuswali
11. Soma Zaidi...

Mambo yanayodhaniwa kuwa yanaharibu funga lakini hayaharibu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Nguzo za swala.
Kipengele hiki kinaelezea nguzo mbalimbali za kuswali. Soma Zaidi...

Sifa za imamu wa swala ya jamaa
Post hii inakwenda kukupa sifa za imamu wa msikitini anayepasa kuswalisha swala ya jamii. Soma Zaidi...

Umuhimu wa swala yaani kuswali kwa mwanadamu
Kwa nini ni muhimu kuswali? Post hii itakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kusimamisha swala. Soma Zaidi...

Ni yapi masharti ya Udhu na kujitwaharisha
Soma Zaidi...

Haki ya Serikali kuzuia Dhulma
Soma Zaidi...

Fadhila za kufunga mwezi wa ramadhani
Soma Zaidi...

Maana ya Funga ya ramadhani kisheria na Aina za funga
Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga. Soma Zaidi...

Jinsi ya kutekeleza funga za sunnah
Hapa utajifunza muda wa kutia jia katika funga za sunnah. Pia utajifunza kuhusu uhuru ulio nao Soma Zaidi...

MALI ZISIZORUHUSIWA KUTOLEWA ZAKA
*Suala la kumilikiwa binaadam (utumwa), japokuwa linaendelea kutajwa kwenye Sharia (katika vitabu), ni suala ambalo haliko. Soma Zaidi...