Post hii inakwenda kukufundisha maana ya neno talaka katika uislamu kisheria na kilugha.
Maana ya Talaka
Talaka ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa waliofunga mume na mke wakati wa kufunga ndoa mbele ya mashahidi wawili. Baada ya kuvunja mkataba huu kwa kufuata sharia ya Kiislamu, mwanamke aliyetalakiwa huwa huru kuolewa na mume mwingine.
Talaka katika Uislamu
Talaka katika Uislamu si jambo Ia kupendeza. Kwa hiyo mume na mke wanatakiwa wajitahidi kusuluhishana na kuvumiliana iii hatua ya kupeana talaka isifikiwe.
Talaka ni jambo Ia halali hub ruhusiwa inapokuwa hapana budi na wala Si jambo Ia kuhifanyia mas-khara kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:
Ibn Umar amesimulia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Katika halali inayochukiza mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) ni talaka ". (Abu Daud).
Kwa upande mwingine, kama Mwenyezi Mungu (s.w) angahiharamisha talaka, hali ya maisha ingahikuwaje katika famihia zile ambazo mume na mke wamekosana kiasi cha kila mmoja kutotaka kumuona mwenziwe! Kwa hiyo, mume au mke atakapofanya kosa au makosa makubwa yasiyovumihika kwa mwenziwe, Mwenyezi Mungu (s.w) ametoa ruhusa wapeane talaka na kuachana kwa wema na mapenzi kama inavyosisitizwa katika Qur-an:
Talaka (za kuweza kurejeana) ni mara mbili. Kisha ni kumuweka kwa wema au kumwacha kwa ihsani ... ". (2:229). Na mtakapowapa wanawake talaka nao wakafikia kumaliza eda yao, basi warejeeni kwa wema au tokaneni nao kwa wema... (2:231). Basi wanapofikia muda wao, ima warejeeni kwa wema, au farikianeni nao kwa wema... (65:2).
Kwakuwa ndoa ni mkataba waliowekeana mume na mke wa kuishi kwa wema na kuachana kwa wema ikibidi kuachana, hapana sababu kabisa ya kujenga chuki na uhasama kati ya wawili hawa kwa sababu tu eti wanashindwa kuuendeleza mkataba wao. Katika aya hizi tunaamrishwa kuvunja mkataba huu kwa wema kwa kufuata utaratibu aliouweka Mwenyezi Mungu (s.w) na baada ya hapo kila mmoja kuwa huru.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Kuchukuwavudhu ni ibada, lakini pia ni matendo ya kuufanya mwilivuwe safi. Katika post nitakwenda kukifundisha namna ya kutia udhu katika uislamu.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu lengo la funga na maana yake katika uislamu.
Soma Zaidi...Mwanadamu anatakiwa aishi huku akikumbuka kuwa ipo siki atakufa. Hivyo basi inatupata lujiandaa mapema kwa ajili ya kifo.
Soma Zaidi...Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali.
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kuzijuwa aina za twahara katika uislamu. Utaviona vigawanyo vya twahara kulingana na maulamaa wa Fiqh
Soma Zaidi...