picha

Zifahamu njia za kutwaharisha, aina za maji, udongo na Namna ya kujitwaharisha

Zifahamu njia za kutwaharisha, aina za maji, udongo na Namna ya kujitwaharisha

Chakujitwah aris hia



Nafsi ya mtu hutwaharika kwa mtu huyo kumuamini Allah (s.w) ipasavyo na kufuata mwongozo wake katika kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kibinafsi na kijamii.
Muislamu atatwaharika kutokana na Najisi na Hadath kwa kutumia maji safi au udongo safi kwa kufuata masharti na maelekezo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.



Sifa za Maji Safi
Maji safi kwa mtazamo wa twahara ni yale yanayofaa kujitwaharishia yaliyogawanyika katika makundi yafuatayo:

(a)Maji Mutlak (maji asili)
Maji yoyote katika hali yake ya asili ni maji safi yanayofaa kujitwaharishia. Maji asili (natural water) ni maji ya mvua, chem chem, visima, mito, maziwa na maji ya bahari.



(b)Maji mengi:



Maji mengi ni maji yaliyokusanywa au yaliyokusanyika pamoja na kuwa na ujazo wa mabirika (qullatain) au ujazo usiopungua madebe 12. Mfano wa maji mengi yaliyokusanywa ni maji ya mapipa yenye ujazo wa lita 240, maji ya mabirika (matangi) maalum yaliyojengwa kuhifadhia maji msikitini na nyumbani. Mfano wa maji mengi yaliyojikusanya ni yale ya madimbwi makubwa yanayojikusanya wakati wa mvua.



Maji mengi hayahabiriki upesi. Hayaharibiki kwa kujitwaharishia ndani ya chombo kilichoyakusanya au ndani ya mkusanyiko huo wa maji. Pia maji mengi hayaharibiki kwa kuingiwa na najisi. Bali maji mengi yatakuwa hayafai kujitwaharishia iwapo yatabadilika asili yake katika rangi au utamu (ladha) au harufu.



(c)Maji machache:



Maji machache ni yale yaliyokusanywa katika chombo au yaliyojikusanya katika ardhi yakiwa na ujazo chini ya Qullatain* au chini ya ujazo wa pipa lenye ujazo wa madebe 12 au chini ya ujazo wa lita 224. Mfano wa maji machache ni ya ndoo, maji ya mtungi na maji yaliyojikusanya kwenye vidimbwi vidogo vidogo wakati wa mvua.



Maji machache hayatafaa kujitwaharishia iwapo



(i)yataingiwa na najisi japo kidogo sana.
(ii)Iwapo yatakuwa yametumika katika kujitwaharishia humo humo kwa kuondoa najisi au Hadath.
(iii)Iwapo yatakuwa yametumika kwa kufulia au kuoshea vyombo au kuogea humo humo.
(iv)Iwapo yataingiwa na kitu kikayabadilisha asili yake katika rangi, harufu au tamu(ladha).



Kutokana na haya tunajifunza kuwa, tunapokuwa na maji machache hatuna budi kuwa waangalifu wakati wa kuyatumia ili tusiyaharibu. Tusijitwaharishe ndani ya vyombo vilivyohifadhia maji hayo, bali tuyateke na kujitwaharisha mbali nayo. Kwa mfano tunakoga kwa kutumia kata na tunatawadha kwa kutumia kopo au birika.



(d)Maji makombo



Maji makombo ni maji yaliyonywewa na binaadamu au mnyama yakabakishwa.Maji makombo yanafaa kujitwaharishia ila yale yaliyonywewa na kubakishwa na mbwa au nguruwe.



Udongo safi



Udongo safi ni ule ulioepukana na najisi na ukabakia katika asili yake na kutochanganyika na kitu kama vile unga, majivu au vumbi la mkaa, vumbi la mbao (saw dust) n.k. kwa kawaida udongo wote katika ardhi ni safi.


                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views 3281

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 ai web app    

Post zinazofanana:

Hukumu ya talaka iliyotolewa kabla ya tendo la ndoa

Endapo mtu atamuacha mke wake kabla hata ya kukutana kimwili, basi talaka hii itahukumiwa kwa namna hii.

Soma Zaidi...
Dhana ya mirathi na kurithi katika zama za ujahiliya

Mirathi katika jamii za kijahiliKatika jamii nyingi za kijahili kama vile jamii ya Waarabu kabla ya Mtume Muhammad (s.

Soma Zaidi...
Je kama maiti imekatika baadhi ya viungo je viungo vyake tunafata utaratibu gani katika kumuosha na kumkafini?

Assalamu Alaykum Warahmatu-llah Wabarakaatuh Naomba kuuliza: Je kama maiti imekatika baadhi ya viungo je viungo vyake tunafata utaratibu gani katika kumuosha na kumkafini?

Soma Zaidi...
Utaratibu wa kuzika maiti ya kiislamu, hatua kwa hatua

Kuzika Kuzika ni kitendo cha nne cha faradh tunacho lazimika kumfanyia ndugu yetu aliyetutangulia kufa.

Soma Zaidi...