image

Ni upi umuhimu wa kufunga katika uislamu

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kufunga kiroho, kiafya na kijamii.

Umuhimu wa Funga ya Ramadhani katika Uislamu

Funga ya Ramadhani ni miongoni mwa nguzo za Uislamu na ni faradh kwa Waislamu kama inavyobainika katika aya ifuatayo:

 

Enyi Mlioamini! Mmelazimishwa kufunga (swaum) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu. (2:183).


Kama ilivyo katika nguzo nyingine za Uislamu, mtu atakapoivunja makusudi nguzo hii hatabakia kuwa Muislamu japo atajiita Muislamu na watu wakaendelea kumuita hivyo. Katika Hadhith iliyopokelewa na Ibn Abbas (r.a), Mtume (s.a.w) amesema:

 


“Kuna viungo vitatu vinavyomuunganisha Muislamu na dini ya Uislamu na yeyote yule atakayevunja kiungo kimoja katika hivi atakuwa amekana Uislamu na kuuawa kwake ni halali.Viungo hivi ni: Kushuhudia kuwa Hapana Mola ila Allah, kusimamisha Sw ala Tano na Kufunga Mwezi w a Ram adhani.”

 


Katika Hadith nyingine Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa mtume (s.a.w) amesema:
“Yeyote yule atakayeacha makusudi kufunga siku moja ya Mwezi wa Ramadhani, hawezi kuifidia siku hiyo hata akifunga kila siku katika umri wake wote (uliobakia)” (Abu-Daud).

 

Funga ni ibada maalum iliyo muhimu sana katika kumuandaa mja kuwa mcha Mungu kwa kule kukata kwake matamanio ya kimwili. Kwa hivyo Allah (s.w) kwa ukarimu wake ameahidi malipo makubwa kwa wenye kutekeleza ibada hii, ili iwe motisha wa kuwawezesha kuitekeleza ibada hii kwa hima kubwa na kwa ukamilifu unaotakikana.
Ahadi ya Allah (s.w) ya malipo makubwa kwa wenye kufunga Ramadhani tunaipata katika Hadith kama ifuatavyo:

 


Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuw a Mtume w a Allah amesema: Mw enye kufunga Ramadhani akiwa na imani na akawa na matumaini ya kupata malipo kutoka kwa Allah dhambi zake zote zilizopita husamehewa; na mwenye kusimama kw a sw ala (Tarawehe) katika mw ezi w a Ramadhani akiwa na imani na matumaini ya kupata malipo (kutoka kwa Allah), dhambi zake zote zilizopita zitasamehew a. (Bukhari na Muslim).

 


Pia Abu-Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume w a Allah amesema:
Kila amali njema anayoifanya mwanaadam italipwa mara kumi (Al-Qur’an 6:160) mpaka kufikia mara mia saba (Al-Qur’an 2:261). Allah (s.w) amesema: “Ila kufunga kwa sababu funga ni kwa ajili Yangu, na ni Mimi mwenyew e nitakayelipa. Mwenye kufunga anakata matamanio yake ya kimwili na anaacha chakula kwa ajili Yangu. Kwa mwenye kufunga kuna furaha mbili, furaha moja anaipata wakati wa kufuturu na nyingine wakati atakapokutana na Mola wake. Na hakika harufu ya mdomo wa mwenye kufunga ni bora mbele ya Allah (s.w) kuliko harufu ya miski. Na funga ni ngao. Kwa hiyo atakayefunga miongoni mwenu hataongea maneno ya upuuzi wala hatagombana. Kama itatokea achokozwe na yeyote, au mtu ataka kupigana naye, na aseme: “Nimefunga ”. (Bukhari na Muslim).

 


Abdullah bin Amr (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Funga na Qur’an vitamwombea mtu shufaa. Saum itasema: Ee Bwana (Rabb) nilimwachisha chakula na kujamii wakati wa mchana, kwahiyo nifanye niw e muombezi wake. Na Qur-an itasema: Nilimwachisha usingizi wakati wa usiku, kwa hiyo nifanye niwe muombezi wake. Kwa hiyo vyote vitamuombea shufaa. ” (Baihaqi).

 


Vile vile Mtume (s.a.w.) katika kusisitiza umuhimu wa funga ya Ramadhani alitoa khutuba mwishoni mwa mwezi wa Shaabani kama ilivyonukuliwa katika Hadith ifuatayo:
Salman al-Farisy (r.a) ameeleza: Mtume (s.a.w) alituwaidhi mwisho wa siku ya Shaabani akasema: Enyi watu! Hakika umekujieni mwezi mtukufu, mw ezi uliobarikiw a, mw ezi ambao ndani yake kuna usiku ulio bora zaidi kuliko miezi elfu moja. Allah (s.w) amefaradhisha kufunga katika mwezi huu na kusimama (kwa swala ya tarawehe) katika mausiku yake ni Sunnah.

 

Atakayetekeleza kitendo kizuri kisicho faradhi atapata ujira wa mtu aliyetekeleza kitendo cha faradhi katika miezi mingine na yule atakayetekeleza kitendo cha faradhi atapata ujira mara 70 wa ujira wa kitendo hicho katika miezi mingine. Na ni mwezi wa subira, na ilivyo, subira malipo yake ni Pepo. Na ni mwezi wa kuhurumiana na mwezi ambao mahitaji (mapato) ya Muumini huongezwa. Atakayetoa futari kwa mwenye kufunga katika mwezi huu kuna kusamehewa dhambi zake na kuwekwa huru na Moto, na atapata malipo sawa na ya yule aliyefunga bila ya yeye kupunguziwa chochote. ” Tukauliza: Ee Mtume wa Allah! Hakuna yeyote kati yetu mwenye uwezo wa kumfuturisha mtu aliyefunga. Alijibu Mtume: Allah atamlipa yule mwenye kumfuturisha aliyefunga kwa funda la maziwa, au tende moja au funda la maji. Na yule anayekidhi haja ya mtu Allah atamnywesha kutokana na Birika (Kawthar) langu na hatakuwa na kiu mpaka atakapoingia Peponi.Na (Ramadhani) ni mwezi ambao mwanzo wake kuna kurehemewa, katikati yake kuna kusamehewa na mwisho wake kuna kuachwa huru na Moto. Na yule atakayempunguzia kazi mtumw a (mtumishi) wake, Allah atamsamehe, na atamuacha huru na Moto.

 


Hadith hizi zinatupa picha juu ya umuhimu wa funga ya Ramadhan kwamba funga ni ngao ya kumzuia Muumini na maovu yanayosababishwa na matashi ya kimwili na itakuwa ni sababu ya Muumini kuingia peponi na kuachwa huru na moto.

 

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1234


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Msisitizo juu ya kutoa zaka na sadaka
Soma Zaidi...

jamii
Soma Zaidi...

Namna ya kujitwaharisha Najisi ndogo
Soma Zaidi...

Watu hawa huruhusiwi kuwaoa katika uislamu
Hapa utajifunza watu ambao ni halali kuwaoa na wale ambao ni haramu kuwaoa. Soma Zaidi...

Namna ya kuswali swala ya maiti: nguzo zake, sunnah zake na maandalizi juu ya maiti
3. Soma Zaidi...

Kutoa vilivyo vizuri
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Nguzo za uislamu:Shahada
Nguzo za uislamu: Shahada (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Namna ya kuoga josho, kujitwaharisha damu ya Hedhi, damu ya kuzaa Nifasi na Janaba
Soma Zaidi...

Hali ya kuzuiliana kurithi katika uislamu
KuzuilianaTumeona kuwa wanaume wenye kurithi ni 15 na wanawake wanaorithi ni 10. Soma Zaidi...

Kwanini wengi wanaohijji hawafikii lengo la hijjah zao
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Utaratibu wa kuzuru makaburi na dua zinazosomwa wakati wa kuzuru kaburi
Post hii itakufundisha taratibu zinazofanyika katika kuzuru kaburi la muislamu. Soma Zaidi...

SWALA
1. Soma Zaidi...