Hadathi



Hadathi ni hali ambayo ikimpata Muislamu, hawezi kuswali mpaka imuondokee. Kuna aina tatu za hadath:



(i)Hadathi ndogo - kutokuwa na udhu. Mtu asiye na udhu ana hadathi ndogo na huondoka kwa kutia udhu.



(ii)Hadathi ya kati na kati - humpata mtu aliyefanya tendo la ndoa (jimai) au aliyetokwa na manii kwa kuota au kwa njia nyingineyo. Hadath hii huondoka kwa kukoga mwili mzima.



Hadathi kubwa - huwapata wanawake wanapokuwa katika Hedhi (damu ya mwezi) au katika Nifasi (damu ya uzazi). Huondoka kwa kuoga mwili mzima baada ya hedhi au nifasi kwisha.