picha

Mgogoro wa kuandama kwa mwezi, Je mwezi wa Kimataifa ama kila Mji na mwezi wake?

Mwezi ukionekana sehemu moja, Waislamu wote ulimwenguni watalazimika kufunga?

Mgogoro wa kuandama kwa mwezi, Je mwezi wa Kimataifa ama kila Mji na mwezi wake?

Mwezi ukionekana sehemu moja, Waislamu wote ulimwenguni watalazimika kufunga?



Waislamu wote wanakubaliana kutokana na hadithi tulizozinukuu hapo juu, kuwa mtu mmoja au watu wachache wakishuhudia kuandama mwezi wa Ramadhani, Waislamu watalazimika kufunga. Pia waislamu wote wanakubaliana kuwa watu wa wili au zaidi wakishuhudia kuandama kwa mwezi wa Shawwal, Waislamu watalazimika kufuturu na kuswali Id dil-Fitr.



Hitilafu kati ya Waislamu juu ya swala la watu wachache kushuhudia kuandama mwezi wa Ramadhani au wa Shawwal ipo kwenye umbali, kwamba ni watu wa wapi wafunge watakaposikia habari za kuandama mwezi kutoka wapi? Juu ya suala hili Waislamu wamegawanyika katika makundi mawili yafu atayo:



Kundi la kwanza ni la wale wanaosema kuwa mwezi ukionekana katika mji mmoja au sehemu moja, basi Waislamu wengine popote walipo ulimwenguni watalazimika kufunga au kufungua. Haya pia ni maoni ya Imamu Hambali, Malik na Abu Hanifa. Hawa wamejiegemeza katika hadithi tulizozinukuu hapo juu.



Kundi la pili ni la wale wanaojiegemeza katika Hadithi ifuatayo: Kurayb (r.a) ameeleza kuwa Umm Fadhl, binti wa Harith alimtuma (mtoto wake) Fadhl Syria (Sham) kwa Muawiya. Fadhl aliwasili Syria na akatekeleza yale aliyotumwa na mama yake. Alipokuwa pale Syria mwezi wa Ramadhani ulianza. (Amesema Fadhl): Niliuona mwezi wa Ramadhani ulipoandama siku ya Ijumaa. Kisha nilirudi Madina mwishoni mwa mwezi. “Abdullah bin Abbas (r.a) aliniuliza juu ya kuandama kwa mwezi wa Ramadhani na akasema: Mliuona lini? Nikajibu: Tuliuona usiku wa Ijumaa. Akaniuliza; Uliona wewe mwenyewe? Nikajibu; Ndio na watu pia waliuona na walifunga na Muawiya pia alifunga, ndipo akasema; lakini sisi tuliuona usiku wa Jumamosi. Kwa hiyo tutaendelea kufunga mpaka tukamilishe 30 au tuuone mwezi Shawwal baada ya 29 Ramadhani) Nikauliza; (Fadhili): kuonekana kwa Mwezi wa Muawiya hakukutosha? Akajibu; Hapana hivi ndivyo Mtume wa Allah (s.w) alivyotuamrisha ”. (Muslim).



Kutokana na hadithi hii kama kuna masafa marefu kati ya mji ulipoonekana mwezi na mji watu walipopata taarifa juu ya kuonekana kwake haitajuzu kwao kufuata mwandamo huo, lakini endapo mji huo utakuwa umekaribiana basi watu waliopata taarifa ya kuandama mwezi kutoka mji wa karibu watawajibika kufunga au kufungua, mwanachuoni mashuhuri anayeshikilia rai hii ni Imamu Shafii.



Kutokana na hitilafu hizi, imetokea kuwa waislamu wote ulimwenguni hawaanzi kufunga Ramadhani siku moja na kuswali Iddil-Fitr na Iddil Hajj siku moja. Wale wanaoshikilia raia ya kwanza, wanaona kuwa si vyema umma mmoja wa Kiislamu kutofautiana katika matukio haya muhimu ambayo ni alama ya dini. Isitoshe kutokana na maendeleo ya sayansi, mawasiliano ulimwenguni hivi leo yamerahisika mno. Ulimwengu mzima unaweza kupata habari kwa muda wa dakika chache juu ya mwandamo wa mwezi katika mji mmoja.



Wale wanaoshikilia rai ya pili wanaoona kuwa si vyema kufunga au kufungua Ramadhani kwa kufuata habari ya kuandama kwa mwezi kutoka popote pale bila ya kujali masafa au machweo (matlai) kati ya mji huo na pale habari ya kuandamana mwezi ilipopokelewa. Kwani kijiografia sehemu mbali mbali za ulimwengu zinatofautiana sana. Kutokana na uchunguzi wa anga umepatikana ushahidi kuwa kuna kutofautiana katika kuona mwezi ambako katika mji mmoja kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kuona mwezi endapo hapatakuwa na mawingu, katika mji mwingine ulio masafa ya mbali na matlai mengine, mwezi hauandami kabisa siku hiyo hata kama hapata kuwa na mawingu. Kwa hiyo hawa wenye mtazamo wa pili, pia kutokana na maendeleo hayo hayo ya kisayansi, wanaona kuwa hadithi zilizowaamrisha watu kufunga au kufungua kwa kupata habari ya kuandama mwezi kutoka kwa mtu mmoja au watu wachache, hazionyeshi kuwa wale walioleta habari za kuandama mwezi walitoka masafa marefu na pale alipokuwa Mtume (s.a.w).



Kutokana na rai hizi mbili, ni vema Waislamu wasigombane kwa jambo hili. Kila mtu ana uhuru wa kufuata hoja iliyomtua zaidi. Hata hivyo, lingelikuwa jambo zuri kama wanachuoni wa kila jimbo lenye uhusiano mwema kama vile Afrika ya Mashariki, wangelijadiliana na kukubaliana juu ya msimamo mmoja.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 3939

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Siku ambazo haziruhusiwi kufunga

Ni haramu kufunga katika masiku haya. Na endapo utafunga basi funga haitakuwa na malipo.

Soma Zaidi...
Tofauti kati ya fiqh na sheria

Kipengele hichi tutajifunza tofauti kati ua fiqh na sheria.

Soma Zaidi...
Ufumbuzi wa tatizo la riba.

Uislamu ndio dini pekee ambayo inatoa ufumbuzi juu ya suala la riba.

Soma Zaidi...
Hijjah

Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mgawanyiko katika kuitumia mali unayomiliki

Unajuwa namna ambavyo matumizi ya mali yako, yanavyogawanywa? Jifunze hapa mgawanyiko wa mali yako.

Soma Zaidi...
Je ni zipi nguzo za uislamu, na ni ngapi nguzo za uislamu?

Post hii itakujuza maana ya uislamu na nguzo zake.

Soma Zaidi...
HUKUMU YA KUUWA MTU (KUMWAGA DAMU) KWENYE UISLAMU

عَنْ ابْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم "لَا يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ [ يشهد أن ل?...

Soma Zaidi...
Milki ya raslimali katika uislamu

Milki ya RasilimaliIli kujipatia maendeleo ya kiuchumi katika zama zote mwanaadamu anahitaji rasilimali za kumwezesha kufikia azma hiyo.

Soma Zaidi...