Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawa mirathi
Haya ni mamno muhimu yanayozingatiwa kabla ya kuanza zoezi la kugawa mirathi ya marehemu.
Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawanya urithi
Kabla mali ya marehemu haijagawanywa kwa warihi wake, hapana budi kuzingatia yafuatayo:
(a)Haki zilizofungana na mali ya urithi:
Mali ya marehemu haitakuwa halali kwa warithi wake mpaka zitolewe haki zifuatazo:
(i)Madeni.
(ii)Zakat.
(iii)Gharama za makazi ya mkewe katika kipindi cha eda.
(iv)Usia ambao hauzidi theluthi moja (1/3) ya mali yote iliyobakia.
(b)Sharti Ia kurithi:
Kurithi kuna sharti tatu:
(i)Kufa yule mwenye kurithiwa (Si halali kurithi mali ya mtu aliye hai).
(ii)Kuwepo hai mrithi wakati akifa mrithiwa. Kwa mfano, kama wawili wanaorithiana mathalani baba na mtoto wote wamekufa. Aliyekufa nyuma (au aliyeshuhudia kifo cha mwenzie) atakuwa mrithi wa yule aliyetangulia kufa.
(iii)Kukosekana mambo yenye kumzuilia mtu kurithi.
(c)Mambo yanayomzuilia mtu kurithi
Mrithi huzuilika kurithi itakapopatikana na moja kati ya sababu zifuatazo:
(i)Kumuua amrithiye: Yaani mtu hatamrithi aliyemuua ijapokuwa kwa bahati mbaya.
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema Mwenye kuua hapati chochote katika mirathi. (Tirmidh, Ibn Majah).
(ii)Kuhitalifiana katika dini:
Muislamu hamrithi kafiri, mshirikina, mkristo au myahudi na wala kafiri, mshirikina, mkristo au myahudi hatamrithi Muislamu hata akiwa karibu naye kiasi gani katika nasaba.
Usama bin Zaid (r.a)ameeleza kuwa mtume wa Allah amesema: Muislamu hamrithi mshirikina wala mshirikina hamrithi Muislamu. (Bukhari na Muslim)
Pia Mtume (s.a.w) amesema katika Hadithi iliyosimuliwa na Abdullah bin Amri(r.a) kuwa: Watu wa dini mbili tofauti hawatarithiana. (Abu Dauwd, Ibn Majah, Tirmidh).
(iii)Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa hana haki ya kumrithi baba aliyemzaa na baba hana haki katika mirathi yake, kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Amri bin Shuab(r.a) ameeleza kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake kuwa Mtume wa Allah amesema: "Atakayezini na mwanamke muungwana au na mjakazi, mtoto atakayepatikana humo hana haki naye. Hatomrithi na wala hatarithiwa naye ". (Tirmidh)
(d)Sababu za Kurithi:
Mtu hurithi kwa sababu moja katika hizi:
(i)Kuwa na nasaba na marehemu (baba, mama, mtoto, ndugu, n.k.). (ii)Kuoana kwa ndoa halali (yaani mume humrithi mke na mke humrithi mumewe).
(iii)Kuacha huru, yaani mwenye kumpa uhuru mtumwa humrithi huru wake.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉2 ai web app 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Taratibu za kumiliki hisa na mali ya shirika
Katika Uislamu kuwa na hisa kwenye mali inaruhusiwa. Hapa utajifunza taratibu za kumiliki hisa.
Soma Zaidi...Mifumo ya benki ya kiislamu.
Hapa utajifunza njia ambazo nenk ya kiislamu hutumia ili kujiendesha
Soma Zaidi...Mambo muhimu ya kuzingatia katika kujenga uchumi wa kiislamu
Nazingatio muhimu katika uchumi unaofuata sheria za kiislamu.
Soma Zaidi...Mambo anayofanyiwa mtu anayekaribia kufa
Haya ni maandalizi anayofanyiwa mtu aliye katika kilevi cha kifo yaani sakaratul maut
Soma Zaidi...