Nguzo za Funga
Nguzo za funga ni mbili: Kutia Nia na kujizuilia na kila chenye kufunguza tangu mwanzo wa alfajiri mpaka kuingia magharibi.Nia ni dhamira anayokuwa nayo mtu moyoni mwake kuwa atafunga. Nia ya funga ya faradhi inatakiwa iletwe kabla ya Alfajir, kwa mnasaba wa Hadith ifu atayo:
Bibi Hafsah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: ambaye hakunuia kufunga kabla ya alfajir, hana funga. (Tirmidh, Abu Daud, Nis a i).
Ama nia ya funga za sunnah, inaweza kuletwa mchana iwapo mtu hajala chochote tangu alfajir kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Aisha, Mama w a Waumini (r.a) ameeleza: Mtume (s.a.w) alikuja kwangu siku moja akaniuliza: Una chochote (cha kula)? Nilijibu: Hakuna. Kisha akasema: βBasi nitafunga.β Siku nyingine alikuja tena kwetu tukamuambia: Mtume wa Allah, tumeletewa zawadi ya Hais (aina ya chakula cha mchanganyiko wa Tende na Siagi). Kisha akasema: βNionyeshe, nilifunga tangu asubuhi. Kisha alikula chakula kile.β (Muslim).
Katika Hadith hii tunajifunza mambo mawili. Kwanza tunajifunza kuwa mtu anaweza kunuia funga ya sunnah mchana kabla ya adhuhuri, iwapo atakuwa hajala chochote tangu alfajiri.
Pili, tunajifunza vile vile kutokana na Hadith hii kuwa mtu anaruhusiwa kuvunja funga ya sunnah pasi na sababu ya kisharia.
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza faida za ndoa katika Jamii na kwa wanadamu kiafya, kiroho, kiuchumi
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ya haramu kwa mwenye hadathi kubwa
Soma Zaidi...Kuingizwa au Kutolewa EdaKatika sheria ya Kiislamu hapana suala Ia kuingizwa au kutolewa eda na Sheikh.
Soma Zaidi...Maana: ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa baina ya mume na mke mbele ya mashahidi wawili kwa kuzingatia sheria ya Kiislamu.
Soma Zaidi...