Hili ndilo hasa lengo la kuamrishwa kufunga
Lengo la Funga
Lengo la funga limebainishwa katika Qur-an pale ilipotolewa amri ya kufunga:
“Enyi mlioamini! Mmeamrishwa kufunga kama walivyoamrishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu ”. (2:183)
Hapa tunabainishwiwa kuwa lengo la kufunga ni kuwafanya Waumini kuwa wacha-Mungu. Neno “Taqwa ” ambalo linatafsiriwa kuwa ni “Uchamungu” lina maana pana zaidi. “Taqwa” ni hali ya kuhofu ghadhabu za Mwenyezi Mungu (s.w) ambayo humfanya mja ajiepushe mbali na yale yote yanayomghadhibisha Mwenyezi Mungu (s.w) na ayaendee mbio kwa unyenyekevu na kwa jitihada kubwa yale yote aliyoamrisha Mwenyezi Mungu (s.w) na yale yote anayoyaridhia. Maana ya ‘Taqwa’ inabainishwa vyema na Hadith ifuatayo:
Siku moja Umar (r.a) alimuuliza Ubbay bin Ka ’b (r.a) amueleweshe maana hasa ya Taqwa. Ubbay (r.a) alijibu: “Amir Muuminin, umewahi kupita njia ya kichaka chenye miba?” Umar (r.a) akajibu: “Naam, nimepita mara nyingi” Kisha Ubbay (r.a) akamuuliza ni hadhari gani uliyoichukua wakati ukipita huko? “Nilishikilia na kukusanya pamoja nguo zangu na kutembea kwa uangalifu katika kupita njia hiyo”, alisema Umar (r.a) ili sehemu yoyote ya nguo zangu isije shikwa na miba hiyo”. Kutokana na jibu hili, Ubbay (r.a) alisema: “Hii hasa ndio maana ya “Taqwa”.
Kutokana na mfano huu mtu mwenye “Taqwa” au Muttaq ni yule mwenye shauku na jitihada kubwa kuepukana na kila aina ya mwiba (uovu) katika kila hatua na kila kipengele cha maisha yake yote na wakati huo huo huwa na shauku na jitihada kubwa ya kuyakimbilia mema katika kila hatua ya maisha yake ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu (s.w). Muttaq ni mtu mwenye cheo na hadhi kubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) kama tunavyofahamishwa katika Qur-an:
“... Hakika aheshimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule aliye Muttaq (am chaye Mw enyezi Mungu zaidi) katika nyinyi. Kw a yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mw enye khabari ya mambo yote. (49:13).
Hiki ni cheo kikubwa sana ambacho hakina mfano wake katika vyeo vya hapa ulimwenguni. Cheo hiki hakipatikani kwa kuomba kura au kwa hongo, bali kinapatikana kwa kujizatiti kujiepusha na makatazo yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) na kujitahidi kutenda mema na kutekeleza maamrisho yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) kwa matarajio ya kupata Radhi ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Ni nini maana ya uchumi katika uislamu
Katikabuislamu dhana ya uchumi imetofautiana na dhana ya kidunia hivi leo ambapo kamari na riba ni moja ya vitu muhimu katika uchumi.
Soma Zaidi...Sura zinazosomwa katika Swala ya Dhuha
Swala ya Dhuha ni swala ya sunna inayosaliwa wakati wa asubuhi baada ya jua kuchomoza na kupanda angalau kiasi cha mkuki (takribani dakika 15 baada ya jua kuchomoza) mpaka kabla ya adhuhuri. Ingawa hakuna sura maalum zilizowekwa kisheria, Mtume ﷺ alisoma baadhi ya sura zenye maana ya kuhimiza kheri na shukrani.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu:Shahada
Nguzo za uislamu: Shahada (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Maana ya Mirathi na kurithi katika uislamu
Maana ya MirathiMirathi katika Uislamu ni kanuni na taratibu alizoziweka Allah (Sw) katika kuwagawawia na kuwarithisha familia na jamaa, mali aliyoiacha marehemu.
Soma Zaidi...Mambo yanayobatilisha funga au yanayoharibu swaumu.
Hapa utajifunza mambo ambayo akiyafanya mtu aliyefunga, basi funga yake itaharibika.
Soma Zaidi...