Siku Zilizoharamishwa Kufunga Sunnah
(i)Siku kuu za Iddil-Fitri na Iddil-Hajj
Imeharamishwa kufunga katika siku hizi kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Abu Sayyid al-Khudri (r.a) ameeleza kwamba Mtume (s.a.w) amesema: Hakuna funga katika siku mbili - siku ya (Iddil) Fitr na siku ya (Idd ya) kuchinja.” (Bukhari na Muslim).
(ii)Siku za Tashriq
Siku za Tashriq ni mwezi 11 hadi 13 Dhul-Hijjah. Ni haram kufunga
katika siku hizi kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Ibn Al-Hazali(r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Siku za Tashriqu ni siku za kula na kunywa na kumkumbuka Allah (s.w) (kwa Takbira). (Muslim).
(iii)Siku ya Shaka
Siku ya Shaka ni siku moja kabla ya Ramadhani. Yaani mwezi 30 Shaabani ambapo inawezekana ikawa ni siku ya kufunga. Mtume (s.a.w) amekataza kufunga sunnah katika siku hii ya mashaka ila kwa yule mwenye ada ya kufunga. Kwa mfano mtu mwenye ada ya kufunga Jumatatu ameruhusiwa kufunga endapo siku hiyo itaangukia Jumatatu. Hadith ifuatayo inabainisha makatazo haya:
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuw a Mtume wa Allah amesema: “Usifunge siku moja au mbili kabla ya Ramadhani ila kwa mtu yule mwenye ada ya kufunga funga fulani (k.m. funga ya Alhamisi), yeye anaruhusiwa kufunga ” (Muslim).
Inatakiwa siku moja au mbili kabla ya Ramadhani tusifunge ili tuweze kuukabili tukiwa na nguvu mpya na ili tutofautishe funga ya Ramadhani na funga za Sunnah.
(iv) Siku ya Ijumaa
Mtume (s.a.w) amekataza funga ya Sunnah katika siku ya Ijumaa tu, lakini kama mtu ana tabia ya kufunga sunnah, ikatokea siku ya Ijumaa ni miongoni mwa siku anazofunga, basi hapana ubaya. Tunajifunza haya katika Hadith zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Na asifunge siku ya Ijumaa yeyote miongoni mwenu; ila tu akiwa ameanza kufunga kabla yake au ameendelea kufunga baada yake”. (Muslim).
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Usiuchopoe usiku kabla ya Ijumaa ukafanya usiku pekee kwa kusimama kwa swala na usiichague siku ya Ijumaa pekee kati ya siku za wiki kuwa ndio siku ya kufunga, ila kama mmoja wenu ana tabia ya kufunga sunnah na ikatokea siku ya Ijumaa imeangukia katika tarehe anayopaswa kufunga. ” (Muslim).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
(b) WarumiJamii ya Warumi nayo ni miongoni mwa jamii zinazohesabika kuwa zilianza kustaarabika mapema katika historia ya ulimwengu.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...(c) Hifadhi ya Mwanamke na Maadili ya JamiiKimaumbile wanaadam kama walivyo wanyama, wamejaaliwa kuwa na mvuto wa kimapenzi kati ya mume na mke ili kuwawezesha kutekeleza wajibu mkubwa wa kuzaana na kuendeleza kizazi.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kuhusu taratibu za ibada ya itiqaf yaani kukaa msikitini kwa ajili ya ibada.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu swala ya ijumaa taratibu zake na jinsi ya kuiiswali.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...