Yanayobatilisha Funga
Mtu aliyefunga analazimika kujizuilia na vitendo mbalimbali ambavyo hubatilisha funga yake. Mfungaji akifanya moja wapo katika yafuatayo swaum yake itabatilika.
(i)Kula na Kunywa
Ukila au ukinywa chochote kile kwa kudhamiria hata ikiwa ni dawa utakuwa umefungulia. Vile vile ukivuta sigara au chochote kile au ukivuta dawa ya mafua kwa pua utakuwa umefungua. Pia kupitisha chochote puani au masikioni kwa kudhamiria, hata ikiwa dawa utakuwa umefu n gu a.
Ikumbukwe kuwa kujifunguza makusudi katika mwezi wa Ramadhani kwa kula na kunywa bila ya udhuru wowote wa kisharia ni kosa kubwa sana mbele ya Allah(s.w) kwa kiasi ambacho hata kama mtu atafunga umri wake wote hataweza kuilipia hiyo siku moja aliyojifunguza makusudi kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Yule anayefungua siku moja ya Ramadhani bila kuwa mgonjwa au kuwa na udhuru mwingine wa kisheria, hata akifunga maisha yake yote hataweza kuilipia funga hiyo. (Ahmad, Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah, Darimi).
Hadith hii inatuasa tusifanyie mas-khara amri za Allah (s.w). Hivyo mtu akijifunguza makusudi ajue wazi kuwa amefanya kosa kubwa ambalo halitasameheka kwa kuilipia tu siku hiyo bali ni lazima pia arejee kwa Mola wake kwa toba ya kweli.
(ii)Kujitapisha Makusudi
Mtu akijitapisha makusudi funga yake itavunjika kutokana na Hadith ifuatayo:
Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Anayeshindwa kuzuia matapishi halipi. Lakini anayejitapisha makusudi, na alipe. (Tirmidh, Abu Daud, Ib Majah).
Kutokana na Hadith hii kutapika kwa ugonjwa hakufunguzi.
(iii)Kupatwa na Hedhi au Nifasi
Mwanamke akipatwa na hedhi au nifasi hata kama imempata nyakati za mwisho kabla ya jua kuchwa, atakuwa amefungua na atalazimika kuilipia siku hiyo baada ya Ramadhani.
(iv)Kujitoa Manii Makusudi Ukijitoa manii kwa mkono au kwa kubusiana na kukumbatiana mume na mke, au kwa njia nyingine yoyote ile utakuwa umefungua.Kutokwa na manii kwa kuota au kwa njia nyingine isiyokuwa ya makusudi, hakufunguzi.
(v) Kunuia Kula na hali umefunga
Ukinuia kula hata kama hukula swaumu yako itakuwa imebatilika kwa kuwa utakuwa umevunja nguzo moja ya funga - nia.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1649
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Kitabu cha Afya
👉4 Kitau cha Fiqh
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 Madrasa kiganjani
mambo yanayofungua swaumu
post hii ijakwenda kukufundisha mambo yanayoharibu funga Soma Zaidi...
NAMNA YA KUCHINJA KATIKA UISLAMU
عَنْ أَبِي يَعْلَى شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم قَالَ: "إنَّ اللَّهَ كَتَبَ الْإِح... Soma Zaidi...
Wanaostahiki kupewa zakat
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Umuhimu wa funga ya ramadhan
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Swala ya Istikhara na jinsi ya kuiswali
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu swala ya Istikhara Soma Zaidi...
Haki na wajibu wa mtoto kwa wazazi na katika jamii
Soma Zaidi...
Jinsi ya kiswali swala ya tahajud na swala za usiku yaani qiyamu layl
Post hii itakujuza jinsi ya kiswali swala ya tahajudi. Pia utajifunza jinsi ya kuswali swala za usikubyaanibqiyamublayl Soma Zaidi...
Jinsi ya kiswali swwla ya dhuha na faida zake
Post hii inakwenda kukufunza kuhusu swala ya dhuha, faida zake wakati wa kuiswali swala ya dhuha na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...
Ni yapi mambo yanayoharibu Swaumu na Mambo yanayobatilisha funga
Soma Zaidi...
Haki ya kumiliki mali katika uislamu
Soma Zaidi...
Maana ya Ndoa na Faida zake katika jamii
4. Soma Zaidi...
Namna lengo la zakat linavyofikiwa
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...