image

Njia za kuzuia na kupunguza zinaa katika jamii

(ii) Hatua za Kuzuia Uzinzi JamiiUislamu pamoja na kutoa mafunzo ya maadii yanayomuwezesha mtu binafsi ajiepushe kwa hiari yake na kitendo kibaya cha zinaa, umechukua hatua mbali mbali ambazo huifanya zinaa isiwe kitendo chepesi katika jamii.

Njia za kuzuia na kupunguza zinaa katika jamii

(ii) Hatua za Kuzuia Uzinzi Jamii
Uislamu pamoja na kutoa mafunzo ya maadii yanayomuwezesha mtu binafsi ajiepushe kwa hiari yake na kitendo kibaya cha zinaa, umechukua hatua mbali mbali ambazo huifanya zinaa isiwe kitendo chepesi katika jamii. Kwani Uislam haukatazi tu kufanya kitendo cha zinaa bali hata kufanya kitendo chochote kitakacho shawishi zinaa ni haramu. Tumeamrishwa katika Qur'an:


Wala msikaribie zinaa. Hakika hiyo zinaa ni uchafu (mkubwa) na njia mbaya kabisa. (17:32).
Kuzuia ugonjwa ni bora na ni rahisi zaidi kuliko kutibu. Uislamu umeweka taratibu zifuatazo iii kuzuia ugonjwa mbaya wa zinaa usienee na kuiathiri jamii:(1) Mavazi na Stara ya Kiislamu
Uislamu umelichukulia kwa umakini mkubwa suala Ia kujisitiri uchi kwa namna ambayo hapana jamii nyingine ulimwenguni iliyofikia kiwango chake. Kabla ya Mtume (s.a.w) kuuhuisha Uislamu, jamii ya Waarabu ilikuwa haijali kabisa suala Ia kusitiri uchi. Watu katikajamii hiyo, walikuwa wakivua nguo hadharani wakati wa kuoga au kujisaidia bila ya kujali nani yuko mbele yao. Walizoea kukaa uchi kwa kiasi kwamba, wake kwa waume walitufu Ka'aba uchi wa mnyama.


Jambo Ia kusikitisha zaidi ni kwamba, hata baada ya Mtume (s.a.w) kuhuisha Uislamu na kuyaeneza maadili ya Kiislamu ulimwenguni kote, bado leo kuna watu katika jamii mbali mbali wanaotembea uchi hadharani. Utakuta hata zile jamii ambazo zinatambua kuwa mwanadamu anastahiki kusitiri uchi wake, hazikuweka mipaka ya uchi wa mwanadamu kwa kiasi kwamba kwa wengi wao sitara imeishia kwenye kufunika sehemu za sin tu. Ni Uislamu pekee, kwa kuzingatia umbile Ia wanaume na wanawake, umetoa mipaka ya uchi kwa wanaume na wanawake na kuelekeza namna bora ya kujisitiri ili kuondoa vishawishi vyote vya zinaa vinavyotokana na mavazi. Mafundisho ya Uislamu juu ya mavazi yanaanza na aya ifuatayo:Enyi wanadamu Hakika Tumekuteremshieni nguo zflchazo tupu zenu na nguo za pambo; na nguo za ucha-Mungu ndizo bora. Hayo ni katika (alama za) Mwenyezi Mungu iii wapate kukumbuka. (7:26).Aya hii inatukumbusha kuwa pamoja na vazi kuwa pambo kwa mwanaadam lengo lake ni kusitiri uchi na vazi linalositiri uchi kwa namna alivyoelekeza Mwenyezi Mungu na mtume wake ndilo vazi Ia ucha-Mungu. Kinyume na vazi Ia ucha-Mungu ni vazi Ia shetani ambaye daima anatushawishi kwenda uchi. Allah (s.w) anatuhadharisha na Shetani katika aya ifuatayo:


Enyi wanadamu!,Shetani asikuuieni katika matata, kama aliyowatoa wazee wenu kauikapepo, akawavua nguo zao iii lwwaonesha lupu zao. Haidka yeye pamoja na kabila yake wanaiwoneni na hali ya lawa hamuwaoni Bila shaka Sisi lumejaalia mashetani lawa marafild wa wale wasioamini. (7:27).
Mavazi ya stara na heshima yanawahusu wote wanawake na wanaume kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo: "Waambie Waislam wanaume wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao Na waambie Waislam wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao ... (24:30-31).Mipaka ya Stara (awrah) ya Mwanamume
Sitara au "awrah" ni neno Ienye maana pana zaidi ya uchi. Ambapo uchi ni ile sehemu tu ya sin ya mwanamume au mwanamke, Awrah au Sitara ni sehemu yenye mipaka mipana zaidi. Awrah ya mwanamume ni kati ya kitovu na magoti. Hivyo uchi wa mwanamume katika maadili ya Kiislamu ni sehemu yote iliyo kati ya kitovu na magoti. Hivyo ni haramu kwa mwanamume kuacha wazi sehemu yoyole ile kati ya kitovu na magoti mbele ya mtu yeyote isipokuwa mkewe na yule iliyomiliki mikono yake ya kuume (mjakazi) na ni haramu pia yeye kuangalia uchi wa mtu mwmgme kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:Sehemu yoyote ile iliyo juu ya magoti haina budi kufunikwa na sehemi yoyote iliyo chini ya kitouu ni lazima funikwe. (Darqutny) Mwanamume hana budi kufunika sehemu ya mwili wake iliyo kati ya kitovu na magoti. (Al-Nabsut). Au bin Abi Taalib (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Usfunue mapaja yako mbele ya mwingine wala usiangalie paja ?a mwingine akiwa hai au maiti. (Tasfiri-Kabiir).Mipaka ya Stara (Awrah) ya Mwanamke
Mipaka ya sitara ya mwanamke, kutokana na umbile lake mipana zaidi kuliko ile ya mwanamume. Ambapo mipaka ya satar ya mwanamume ni kati ya kitovu na magoti, satar ya mwanamke ni mwili mzima isipokuwa uso na vitanga vya mikono. Wanawake wameamrishwa kujisitiri hivi katika aya zifuatazo:


Na waambie Waislam wanawake wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao wala wasidhihirishe viungo uyao isipokuwa vinavyodhihirika (uso na viganja vya mikono) na waangushe shungi zao (mitandio yao) mpaka vfuani mwao
(24:31)


Ewe Mtume! Waambie wake zako na binti zako na wan awake wa Kiislamu wajiteremshie uzuri nguo zao(majalabibi yao). Kufanya hivyo kutawapelekea upesi wajulikane (kuwa ni watu wa heshima) wasibughudhiwe (33:59).Mtume (s.a.w) amezisherehesha aya hizi katika Hadith zifuatazo: Mtume (s.a.w) amesema; Si halali kwa mwanamke yeyote anayemuamini Allah (s. w) na Siku ya Mwisho kuacha wazi mkono wake zaidi ya hapa - kisha akaonyesha mkono wake mwanzo wa kiganja (wrist joint) (Ibn Jaryr). Mwanamke anapofikia baleghe hataiacha wazi sehemu yoyote ya mwili wake isipokuwa uso na viganja. (Abu Daud).


Katika Hadith nyingine, Aisha (r.a) ameeleza kuwa alitokea mbele ya mpwa wake Abdullah bin Al-Tufail, akiwa amejipamba. Mtume (s.a.w) hakupendezewa. Aisha akasema: "Ewe Mtume wa Allah ni mpwa wangu". Mtume (s.a.w) akasema: Mwanamke anapofikia baleghe si halali kwake kuiacha wazi sehemu yoyote ya mwili wake ila USO wake na hapa - kisha akashika sehemu ya ungio ?a kiganja cha mkono (wrist joint) kiasi cha kuacha sehemu ndogo kati ya hapo aliposhika na mwanzo wa kiganja. (Ibn Majah).
Vazi linaloonesha (transparent) hata kama linafunika mwili mpaka kwenye mipaka ya awrah iliyowekwa, pia limeharamishwa katika Uislamu kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:Aisha (r.a) amesimulia kuwa: wanawake katika ukoo wa bani Tamiimu walikuja (kwake Aisha) wakiwa wamevalia nguo nyepesi, Aisha akawaambia kama ninyi ni wanawake mlioamini kweli kweli,hizi Si nguo za wanawake walioamini" Pia akasema alikuja hint kigori akiwa amevalia shungi na gauni linaloangaza, Aisha akamuambia; yeyote katika wanawake atakayevaa hivi haamini yaliyoteremshwa katika suratun Nuur (Abuu Dawud)Pia vazi Ia Kiislamu halitakiwi likawa lenye kubana kiasi cha kuonyesha mchoro wa mwili: Umar (r. a) amesema: Msiwavalishe wake zenu nguo zinazobana kiasi cha kuonyesha makunjo yote ya mwili. (A 1-Mabsuut). Kwa nini Stara zaidi Yatakikana kwa Mwanamke? Kutokana na mipaka ya satar ya wanawake na wanaume tuliyojifunza hapa tumeona kuwa sitara yatakikana zaidi kwa mwanamke kuliko kwa mwanamume. Kuna watu wanaopenda kujua kwa nini mwanamke anatakiwa ajisitiri mwili mzima wakati mwanamume anatakiwa ajisitiri sehemu tu ya mwili? Kwani wan awake nao pia wanaweza kuvutiwa na hizo sehemu za wanaume kama wao wanavyovutiwa na wanawake kwa kuangalia sehemu zao za mwili na ndio maana kwenye Qur'an wameamrishwa wote kuinamisha macho yao na kulinda tupu zao.


Lakini pamoja na ukweli huu si kweli kabisa kudai kuwa mvuto wa umbile Ia mwanamke kwa mwanamume ni sawa na ule wa umbila Ia mwanamume kwa mwanamke. Ukiwalinganisha na wanaume, wanawake wamejaaliwa sura nzuri zaidi na umbile Ia kuwavutia wanaume. Kwa mfano, katika hali halisi mwanamume anaweza kutembea bila shati maadam amejisitiri kati ya kitovu na magoti, lakini kama hali halisi ni viroja kwa mwanamke kutembea kifua wazi. Ilivyo ni kwamba wanaume wanavutiwa kwa urahisi na umbo Ia mwanamke na wanawake ni wepesi kuhadaishwa na mapenzi ya wanaume. Kwa kuzingatia ukweli huu ndio Uislamu ukaweka mipaka ya stara na mahusiano kati ya wanaume na wanawake iii kuiepusha jamii na Zlnaa.Jambo Ia kuzingatia na wenye kuuliza swali hili ni kwamba aliyetoa mipaka hii ya satar ya wanawake na wanaume ni Allah (s.w), Mjuzi, Mwenye hekima, Mwenye kujitosheleza na aliyemkamilifu ambaye hana sababu ya kumpendelea au kumwonea yeyote kati ya wanawake na wanaume. Bali ameweka mipaka hii ya satar kulingana na umbile Ia mwanamke na umbile Ia mwanamume. Hivyo, mwanamke Muislamu anapotekeleza amri hii ya kujisitiri Kiislamu asifanye hivyo kwa kuchelea kulaaniwa na jamii bali atekeleze agizo hili kwa sbabau tu ni amri ya Allah (s.w). Kwa msimamo huu mwanamke Muislamu ataendelea kulitekeleza agizo hili hata kama mawazo ya jamii yatabadilika na kuanza kudhani kuwa mwanamke kutembea uchi kwa kuvaa kaboka, mini-skirt, n.k. ndio alama ya maendeleo. Muislamu wa kweli hana hiari katika kutekeleza amri ya Allah (s.w) kama tunavyokumbushwa katika Qur'an:


Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliye amini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na Mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi. (33:36). Masharti ya stara hulegezwa kwa mwanamke anapokuwa nyumbani kwake au katika hadhara ya wanawake au hadhara ya maharimu wake (wale walioharamishwa kumuoa) kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:


Na waambie Waislamu wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika. Na waangushe shungi zao mpaka vfuani mwao na wasionyeshe mapambo yao ila kwa wanaume zao, au baba zao, au baba za waume zao au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenziwao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi wanaume wasio na matamanio (kwa wanawake kama vile wazee) au watoto amabo hawajui mambo yaliyohusu uke (24:31). Pia masharti ya stara yamelegezwa kwa wanawake vikongwe ambao hawavutii tena wanaume kama tunavyojifunza katika Qur'an.Na wanawake wenye kujiweka ambao hawatumaini tena kuolewa si vibaya kwao kupunguza baadhi ya nguo zao lakini bila ya kuonyesha mapambo yao. Na kama wakijizuia (kupunguza hizo nguo) ndio bora kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. (24:60). Aya hii inazidi kutuonyesha kuwa hekima ya wan awake kuamrihswa kujisitiri kwa kujifunika mwili mzima ni kuzuia zinaa.(2) Kubisha Hodi.
Katika kuzuia kitendo kibaya cha zinaa Uislamu umewakataza Waislamu wanaume kuingia kwenye nyumba bila ya kuwatahadharisha wanawake waliomo ndani iii wasije wakawakuta katika hali isiyo ya stara. Qur'an inaamrisha:


Na watoto miongoni mwenu, watakapo baleghe basi na wabishe hodi kama walivyobisha hodi wale wa kabla yao. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyokubainishieni aya zake. (24:59).Hapa tunaona amri ya kubisha hodi inakuwepo baada ya kufikia baleghe. Pamoja na amri hii, watu wengine wasiokuwa wenyeji wa nyumba wanaamrishwa kubisha hodi kabla hawajaingia katika majumba ya watu kama ifuatavyo: Enyi mlioamini! Msiingie nyumba ambazo si nyumba zenu mpaka muombe ruhusa, na muwatolee salam waliomo humo. Hayo ni bora kwenu, huenda mtakumbuka. (24:2 7).Lengo Ia amri hii ni kuchunga stara na uhuru wa wakazi wa nyumba. Amri hi iliposhuka, baadhi ya watu hawakujua maana yake, kwa hiyo wakawa mara kwa mara wanachungulia dirishani iii kuwaangalia watu waliomo ndani. Siku moja wakati Mtume (s.a.w) alipokuwemo chumbani mwake, mtu mmoja alimchungulia dirishani ndipo Mtume (s.a.w) akamwambia:Kama ningal/ua kwamba unachungulia ningalisukumiza kitu jichoni mwako. Amri ya kubisha hodi imetolewa iii kuwahfadhi watu na mtazamo mbaya (kutizama visivyo ruhusiwa). (Al-Bukhari). Kisha Mtume (s.a.w) alitangaza hadharani: Kama mtu atachungulia ndani ya nyumba ya mtu mwingine bila ya ruhusa, watu wa nyumba hiyo hawatalaumiwa iwapo watalitoboajicho lake. (Muslim).Pia tunaamrishwa kwamba tukiwa na haja ya kitu katika nyumba ya mtu mwingine tusiingie ndani moja kwa moja kuomba kitu hicho bali tuombe tukiwa nje au nyuma ya pazia:"Nanyi mnapowauliza (wanawake) waulizeni nyuma ya pazia. Kufanya haya kutasafisha nyoyo zenu na nyoyo zao (33:53). Aya hii inaonyesha wazi kuwa amri hii imewekwa iii kuzuia vishawishi vya zinaa kutokana na msemo " ... kufanya haya kutasafisha nyoyo zenu na nyoyo zao Yaani huwazuia wanaume na wanawake kuwa na fikra mbaya zitakazo wapelekea kwenye zinaa.(3) Makatazo ya kuwashika wanawake na kukaa faragha nao.
Kuwashika wanawake wasiomaharimu au kukaa faragha nao ni haram katika Uislamu kwani ni vishawishi vikubwa vya zinaa. Imepokelewa kwa Uqbah bin Amir kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Tahadhari kumwita mwanamke faraghani. Answar mmoja akauiza:
Ewe Mtume wa Allah, vipi kwa kaka au mdogo wa mume wangu (vipi kwa shemeji yangu)? Mtume (s.a.w) akasema: "Amekufa!" (Bukhari, Muslim na Tirmidh).Pia Mtume (s.a.w) ameonya: Msiwatembelee wanawake waume zao wakiwa hawapo kwa sababu Shetani anaweza kuzunguka ndani ya yoyote kati yenu kama damu inavyozunguka mwilini. (At-Tirmidh). Kutoka kwa Amr bin As, Mtume (s.a.w) amewakataza waume kuwaita au kuwatembelea wanawake bila ya ruhusa ya waume zao. (Tirmidh).Pia Mtume (s.a.w) kasema: Kuanzia leo, hapana mwanamume anayeruhusiwa kumtembelea mwanamke atakapokuwa hayupo mume wake mpaka atakapokuwa ameongozana na mtu mwingine, mmoja ua wawili. (Muslim). Uharamu wa kumshika mwanamke asiye kuwa mke au maharimu, umedhihirika katika Hadith zifuatazo: Mtume (s.a.w) amesema:


Atakayeshika kiganja cha mwanamke asiyekuwa maharimu wake Siku ya Kiyama atawekewa kaa ?a motojuu ya kiganja chake (Tirmidh, Fat-h al-Qdr).
Aysha (r.a) amesema kuwa Mtume (s.a.w) alipokea kiapo cha utii (Bai 'ah) kutoka kwa wanawake bila ya kuwashika mikono. Hajawahi Mtume (s.a.w) kushika kiganja cha mwanamke ambaye si mke wake. (Bukhar).Umaimah hint Ruqaiah) amesimulia kuwa alikwenda kwa Mtume (s.a.w) akiwa ameongozana na wanawake wengine kutoa kiapo cha utii (Baiah). Mtume (s.a.w) aliwataka waahidi kuwa watajiepusha na ushirikina wizi uzin/u, fitna na kumuasi Mtume. Walipochukuakiapo walimuomba awashike mkono iwe alama ya ahadi yao. Mtume (s. a. w) alisema: Sishiki mkono wa mwanamke. Makubaliano yam domo yanatosha. (Nasai Ibn Majah).
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 293


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Namna ya kutayamamu hatuwa kwa hatuwa
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkutayamamu. Soma Zaidi...

Utaratibu wa kuzuru makaburi na dua zinazosomwa wakati wa kuzuru kaburi
Post hii itakufundisha taratibu zinazofanyika katika kuzuru kaburi la muislamu. Soma Zaidi...

Kwa nini imefaradhishwa kufunga mwezi wa Ramadhani
Unaweza kijiuliza ni kwa nini hasa kimepelekea kufaradhishwa kufunga mwezi wa Ramadhani. Soma Zaidi...

Ni yapi mambo yanayoharibu Swaumu na Mambo yanayobatilisha funga
Soma Zaidi...

Njia za kuzuia na kupunguza zinaa katika jamii
(ii) Hatua za Kuzuia Uzinzi JamiiUislamu pamoja na kutoa mafunzo ya maadii yanayomuwezesha mtu binafsi ajiepushe kwa hiari yake na kitendo kibaya cha zinaa, umechukua hatua mbali mbali ambazo huifanya zinaa isiwe kitendo chepesi katika jamii. Soma Zaidi...

TOFAUTI KATI YA MAKATOZO NA MAAMRISHO KATIKA SUNNAH
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ صَخْرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْت رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم يَقُولُ: "م... Soma Zaidi...

Kujitwaharisha najisi kubwa najisi ya mbwa na Nguriwe
Soma Zaidi...

Mgawanyiko katika kuitumia mali unayomiliki
Unajuwa namna ambavyo matumizi ya mali yako, yanavyogawanywa? Jifunze hapa mgawanyiko wa mali yako. Soma Zaidi...

Dhana ya haki na uadilifu katika uislamu
HAKI NA UADILIFU KATIKA UISLAMU. Soma Zaidi...

Jinsi ya kumuosha maiti wa kiislami mwanaume au mwanamke
Post hii inakwenda kukufundisha hatuwa kwa hatuwa jinsi ya kumuosha maiti wa kiislamu Soma Zaidi...

chimbuko la sheria katika uislamu, hukumu za sheria na kuyatambua yaliyo halali na haramu
Soma Zaidi...

Uzuri wa Benki za kiislamu
Kwa nini benki za kiislamu ni bora kuliko benki nyingine? Soma Zaidi...