image

namna ya kutekeleza Funga za Sunnah pamoja na majukumu mengine

namna ya kutekeleza Funga za Sunnah pamoja na majukumu mengine

Nia katika Funga za Sunnah



Katika funga ya Ramadhani, kutokana na hadith iliyosimuliwa na Hafsah (r.a), funga haisihi endapo mtu hatatia nia ya kufunga usiku kabla ya Alfajir kuingia. Lakini katika funga za Sunnah mtu anaweza kunuia swaum mchana kabla ya kuingia adhuhuri, endapo atakuwa hajala chochote tangu alfajir, kama inavyobainika katika Hadithi ifuatayo:
Aysha (r.a) ameeleza kuwa siku moja Mtume wa Allah (s.a.w) aliniuliza:
“Aysha, una chochote (cha kula)?” Nikasema: “Mjumbe wa Allah, hatuna
chochote ”. Ndipo akas em a: “Nim efunga ”. (Muslim).


Uhuru wa kuvunja Funga ya Sunnah



Mtu aliyefunga sunnah ana uhuru kamili wa kufungua katikati endapo ataona ni vyema kwake kufanya hivyo. Tunajifunza hili katika Hadith zifuatazo:
Aysha (r.a) ameeleza: Mtume wa Allah alikuja kwangu akasema: “Una chochote cha kula?” Nikajibu: “Hapana.” Kisha akasema: “Basi, nitafunga ”. Kisha siku nyingine alitujia tukamwambia: Mtume wa Allah, tumeletewa zawadi ya Hais (aina ya chakula). Ndipo akasema: “Nionyeshe, nilikuwa nimefunga tangu alfajir, kisha alikula. ” (Muslim).



Ummi Hani (r.a) ameeleza kuwa katika siku ya kutekwa Makka Fatma (r.a) alikaa kushotoni mw a Mtume na Ummi Hani alikuwa kuliani kw ake. Kisha Walidah (r.a) alileta kikombe cha maji, alichukua akanywa, kisha Ummi Hani naye alichukua na kunywa. Akasema: Ee Mtume wa Allah, nilifunga na sasa nimefungua. akamuuliza: Ulikuwa unalipa? Akajibu: ‘Hapana ’ Akasema Mtume (s.w.): “Haidhuru iwapo ilikuwa ni funga ya sunnah. Mtu anayefunga funga ya sunnah ana uhuru kamili. Akipenda atafunga na akipenda ataacha.” (Abu Daud, Tirmidh, Ahmad). Aliyefunga Sunnah akikaribishwa aseme: “Nimefunga”
Mtu aliyefunga akikaribishwa chakula aseme ‘nimefunga’ kama tunavyofahamishw a katika Hadith ifuatayo:



Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah (s.a.w) amesema:“Kama mmoja wenu atakaribishwa chakula akiwa amefunga s em a: “Nim efunga ”:. (Muslim).
Si vibaya mtu asiyefunga kula mbele ya yule aliyefunga, bali mfungaji hupata ujira kwa kule kuamua kwake kuendelea kufunga pamoja na kuwaona wengine wakila mbele yake. Tunajifunza katika Hadith zifuatazo:



Ummi Umrah bin Ka ’ab (r.a) amesimulia: Mtume (s.a.w) alimtembelea na akamuandalia chakula, Mtume akamwambia kula. Akasema: “Nimefunga. ” Ndipo Mtume (s.a.w) akasema: “Wakati kitu kinapoliw a mbele ya mtu aliyefunga, malaika wanamrehemu mpaka wamalize kula” (Ahm ad).



Buraidah (r.a) amesimulia kuwa Bilal alikuja kwa Mtume (s.a.w) akamkuta anafungua kinywa. Mtume w a Allah akamkaribisha Bilal akamwambia: “Kifungua kinywa, Ee Bilal.” Bilal akasema: Nimefunga. Ee! Mtume wa Allah.’ Kisha Mtume wa Allah akasema: “Tunakula riziki yetu na riziki ya Bilal ya hali ya juu. Riziki ya hali ya juu kuliko zote ni Pepo. Unafahamu Ee Bilal kwamba mifupa ya mtu aliyefunga inamtukuza Allah na Malaika wanamuombea msamaha kwa muda wote ambao watu wanakula karibu yake?” (Baihaqi).



Funga za Sunnah na utekelezaji wa majukumu



Endapo kufunga sunnah kutamfanya mtu ashindwe kutekeleza majukumu yake kwa wengine katika jamii, ni vyema kutofunga. Katika Hadith tunafahamishwa kuwa wakeze Mtume (s.a.w) walikuwa aghlabu hawafungi mbali ya Ramadhani na Shaabani kwa kuhofia kushindwa kutekeleza wajibu wao kwa Mtume (s.a.w). Katika mwezi wa Shaaban Mtume (s.a.w) alikuwa akifunga sana kuliko miezi mingine:



Aysha (r.a) ameeleza: Kama mmoja wetu aliacha siku katika Ramadhani (kwa udhuru wa sheria) katika maisha ya Mtume (s.a.w) hakuweza kuzilipa alipokuwa na Mtume wa Allah mpaka Shaaban inaingia.” (Muslim).



Hadith hii inasisitiza kuwa kwa kuchelea kutoweza kutekeleza wajibu wao kwa Mtume wa Allah, wakeze Mtume(s.a.w) hawakuthubutu kufunga walipokuwa na Mtume. Mwanamke haruhusiwi kufunga sunnah mpaka aridhiwe na mume wake.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 521


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Hekma katika hukumu za mirathi katika uislamu, na ni kwa nini wanaume wanazidi katika kurithi katika uislamu
Soma Zaidi...

Umuhimu wa uchumi katika uislamu
2. Soma Zaidi...

Kugungisha ndoa ya kiislamu hatuwa kwa hatuwa
Hapa utajifunza jinsi ya kuozesha hatuwa kwa hatuwa. Pia utajifunza masharti ya kuoa na masharti ya kuolewa. Soma Zaidi...

Namna ya kuswali hatuwa kwa hatuwq
Post hii itakufundisha jinsi ya kuswali hatuwa kwa hatuwa. Soma Zaidi...

Kumkafini maiti namna ya kushona sanda ya maiti na utaratibu wa kumvisha sanda maiti
2. Soma Zaidi...

DARSA ZA NDOA, FAMILIA, SIASA, BIASHARA, UCHUMI, HAKI NA SHERIA KATIKA UISLAMU
1. Soma Zaidi...

Kutoa kati kwa kati
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

kuletewa ujumbe
(c)Kuletewa Ujumbe na Malaika kutoka kwa Allah (s. Soma Zaidi...

malezi ya mtoto mchanga baada ya talaka
Soma Zaidi...

Yanayofaa kwa maamuma katika kumfata imamu kwenye swala ya jamaa
Soma Zaidi...

Hadhi na Haki za Mwanamke Katika Uislamu na Jamii kwa ujumla
Soma Zaidi...

Mambo yanayotenguwa udhu
Post hiibinakwenda kukufundisha mambo ambayo yanaharibu udhu. Soma Zaidi...