4. Kuelekea QiblaKuelekea Qibla ni sharti la nne la kusimamisha swala. Katika hali ya kawaida Muumini ni lazima aelekee “Qibla wakati akiswali.Qibla ni neno la Kiarabu linatokana na neno “Qabala” lenye maana ya kuelekea sehemu au upande ambao watu huelekeza nyuso zao. Kwa mtazamo wa Qur-an, Qibla ni sehemu wanapoelekea waislamu wakati wa kuswali. Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa Qibla ni sehemu ya katikati inayowaunganisha waumini kuwa mwili mmoja (kitu kimoja).


“Na po pote wendako geuza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu . Na hiyo ndiyo haki itokayo kwa Mola wako. Na Mw enyezi Mungu si Mwenye kughafilika na yale mnayoyatenda. (2:149)Ummati wa Muhammad (s.a.w) Qibla chake ni Ka’aba, nyumba tukufu ya Allah iliyoko mjini Makkah, Saudi Arabia. Waislamu wote ulimwenguni huielekea Ka’aba wakati wa kuswali. Swala yoyote itakayoswaliwa bila ya kuelekea upande ilipo Ka’aba, pasipo na dharura inayokubalika kisheria kama vile kuwa mgonjwa, au kuwa safarini, ha is wih i.Namna ya Kutafuta QiblaKukisia ulipo mji wa Makka, Saudi Arabia, ambao ndani yake iko Ka’aba ni jambo rahisi kwa kutumia utaalamu wa Jiografia. Chombo


kizuri cha kumuwezesha mtu kukisia ilipo Ka’aba ni ramani ya dunia. Utakapojua ulipo katika sehemu yoyote ya dunia utaweza kujua Ka’aba iko upande gani wa dira kutokea pale ulipo kwa kutumia jua au chombo cha dira (Magnetic Compass). Kwa mfano ukiwa Tanzania, utaelekea Kaskazini kamili, ukiwa Pwani kama vile Dar es Salaam na ukiwa bara kama vile Kigoma, utaelekea Kaskazini ya Kaskazini Mashariki.Kabla ya Muislamu hajaanza kuswali, hasa anapokuwa mgeni wa mahali hana budi kufanya jitihada ya kutafuta Qibla kwanza. Ni vyema mtu asafiripo awe na dira (Magnetic Compass) na ramani ili vifaa hivi vimsaidie kutafuta Qibla, vinginevyo itabidi awaulize wenyeji wa sehemu h iyo.Mtu akishindwa kabisa kukibaini Qibla baada ya kujitahidi mwisho wa jitihada zake, popote atakapoelekea patafaa, kwani hii sasa imekuwa ni dharura, huku tukizingatia kuwa “Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu”.


Na Mashariki na Magharibi ni ya Mw enyezi Mungu. Basi mahala popote mgeukiapo (alikokuamrisheni Mw enyezi Mungu mtazikuta) huko radhi za Mwenyezi Mungu. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa (mkubwa kabisa) na Mwenye kujua (kukubwa kabisa vile vile). (2:115)