Swala ya maiti
Mambo yanayostahiki kufanyiwa maiti ya Muislamu
Mambo yaliyo faradhi kufanyiwa maiti ya Muislamu ni manne yafu atayo:
(1)Kuoshwa.
(2)Kuvikwa sanda (kukafiniwa).
(3)Kuswaliwa.
(4)Kuzikwa.
Pamoja na haya manne kuna mambo mengine mengi yanayotakiwa afanyiwe Muislamu anayekaribia kufa na aliyekufa kama alivyotuelekeza Mtume (s.a.w). Hivyo, katika kitabu hiki tumeeleza mambo yote ya msingi yanayostahiki afanyiwe Muislamu pale anapokaribia kufa mpaka baada ya kuzikwa.
Mambo muhimu anayofanyiwa Muislamu anayekaribia Kufa.
Mauti ni jambo la lazima sana kumtokea mwanaadamu na viumbe vyote na huingia bila taarifa wakati wowote na mahali popote kama anavyotufahamisha Allah (s.w):
Popote mlipo mauti yatakufikieni, na hata mkiwa katika ngome madhubuti...” (4:78).
Kila nafsi ita onja ma uti. Na bila s haka m tapew a ujira w enu kam ili s iku ya Kiyama. Na aliyewekwa mbali na moto na akaingizwa Peponi, basi amefuzu (amefaulu kweli kweli). Na maisha ya dunia (hii) si kitu ila ni starehe idanganyayo (watu). (3:185).
Kutokana na ukweli huu ni jambo la busara mno kwa mwanaadamu mwenye akili timamu kujiandaa kukabili mauti wakati wowote na popote atakapokuwa. Ni kweli kuwa maisha ya ulimwengu yamejaa hadaa lakini hatuna budi kukumbuka kuwa maisha yote ni mtihani kwetu na Muumba wetu anatuchunga barabara na kudhibiti tuyatendayo katika kila pumzi ya maisha yetu. Kumbukumbu ya ukweli huu pamoja na kukikumbuka kifo katika kila sekunde ya maisha ndiyo nguvu pekee ya kumsukuma mja kwenye maisha ya wema anayoridhia Allah (s.w). Kifo ni tukio la lazima lisiloepukika kwa kila kiumbe. Hatuna budi kukifanya kifo kitu cha kawaida na kujiandaa kwacho badala ya kufanya zoezi la kukikimbia jambo ambalo ni muhali.
Mtu anapokaribia kufa na baada ya kufa huwa, pamoja na ujanja wake wote na vipaji vyake vyote alivyokuwa navyo, hajimudu kwa chochote na kwa hiyo anahitajia msaada wa kila jambo.
Hivyo Uislamu unatufundisha kuwa mtu anayekaribia kufa tumfanyie yafuatayo:
1. Kumuogesha, kumpigisha mswaki na kumpaka manukato iwapo kuna uwezekano.
2. Kumlaza kwa ubavu wa kulia na kumuelekeza Qibla kama kuna uwezekano. Kama hivi haiwezekani mgonjwa alazwe chali na uso wake unyanyuliwe kiasi cha kuelekea Qibla
3. Kumpa maji ya kunywa.
4. Kutamka kalima ya Laailaahaillallah bila ya kumuashiria kuwa naye atamke. Lengo la kumtamkia kalima hii ya Tawhiid ni kumkumbusha ili naye aweze kutamka kama ni mtu aliyeishi maisha yote kulingana na kalima hiyo. Kumtamkia kalima Muislamu anayekaribia kufa ni agizo la Mtume (s.a.w):
Abu Said na Abu Hurairah (r.a)wamesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Wasomeeni watu wenu wanaokaribia kufa:
“Hapana mola ila Allah”
Pia Mu’az bin Jabal amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema:
Yule ambaye maneno yake ya mw isho yatakuwa: (Hapana mola ila Allah) ataingia Peponi. (Abu Daud).
Kutokana na Hadithi hii haitakuwa rahisi kwa mtu wa motoni kutamka kalima hii bali ataitamka tu yule aliyeishi maisha yake yote kulingana na kalima hii. Kwa mtu mwema kuitamka kalima hii kunampa maliwazo kuwa amali yake njema imetakabaliwa. Kutamka huku si lazima kuwe kwa wazi. Kutamka kimoyo moyo tu kunatosha, japo ni vizuri kuibanisha kwa ulimi iwapo ipo fursa.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 847
Sponsored links
👉1
Simulizi za Hadithi Audio
👉2
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉3
Madrasa kiganjani
👉4
kitabu cha Simulizi
👉5
Kitau cha Fiqh
👉6
Kitabu cha Afya
Sharti za kusihi kwa funga
Soma Zaidi...
Mambo yaliyo haramu kwa mwenye hedhi na nifasi
Katika post hii utakwenda kujifunza mambo ambayo ni haramu kwa mwanamke aliye na hedhi na nifasi Soma Zaidi...
Mambo yanayodhaniwa kuwa yanaharibu funga lakini hayaharibu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Taratibi za malezi ya watoto wadogo baada ya talaka katika uislamu
Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi? Soma Zaidi...
JIFUNZE FIQH
Fahamu darsa mbalimbali za fiqh kama swala, twahara, zaka pamoja na funga. Zijuwe sharti za swala, funga na zaka. Soma Zaidi...
Kutoa kati kwa kati
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Siku zilizoharamishwa kufunga Sunnah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Msisitizo juu ya kutoa zaka na sadaka
Soma Zaidi...
Haki za muislamu kwa muislamu mwenziwe
Hizi ndio haki kuu tano unazopasa kumpatia Muislamu mwenzio. Soma Zaidi...