Kutawadha ni katika ibada muhimu za mwanzo kutakiwa kuzijuwa na ni lazima. Swala yako haitaweza kutimia bila ya kujuwa udhu. Inakupasa kujuwa nguzo za udhu, yanayoharibu udhu na namna ya kutawadha kifasaha. Hapa utajifunza hatuwa za kutawadha
HATUWA ZA KUTAWADHA
1. kupiga msaki
2. kusema Bismillaah na kuanza kuosha viganja vya mikono (mara tatu) -hatua 1
3. Kusukutua na kupandisha maji puani (mara tatu) - hatua 2 na 3
4. Kuosha uso kwa ukamilifu (mara tatu) - hatua 4
5. Kuosha mkono wa kulia mpaka kwenye fundo (mara tatu)
-hatua 5
6. Kuosha mkono wa kushoto mpaka kwenye fundo (mara tatu)
-hatua 6
7. Kupaka maji kichwani- hatua 7
8. Kuosha masikio (mara tatu)- hatua 8
9. Kuosha mguu wa kulia halafu wa kushoto mpaka kwenye fundo (mara tatu)- hatua 9.
Umeionaje Makala hii.. ?
Hili ni somo letu la kwanza kwenye mtiririko huu wa darsa za fiqh. Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya uislamu na nguzo zake.
Soma Zaidi...Vipi lengo la funga litafikiwa na kumfanya mfungaji awe mchamungu.
Soma Zaidi...Hapa utajifinza uharamu wa riba na sababu za kuharamishwa kwake.
Soma Zaidi...Kwa nini Lengo la Funga halifikiwi na Wafungaji Wengi?
Soma Zaidi...