4.
4. Kuzika.
Kusindikiza jeneza.
- Waislamu (watu) wataongozana nayo mpaka kaburini kimya kimya.
- Jeneza lisitanguliwe na watu (msafara).
- Haitakiwi watu kukaa kabla ya jeneza kukalishwa chini.
Kaburi.
- Kaburi liwe pana na kina cha kutosha, mtu kuweza kusimama na kunyoosha mkono kama kuna uwezekano.
- Kisha lichimbwe shimo dogo (mwana ndani) upande wa Qibla ndani ya kaburi.
- Urefu na ukubwa wa kaburi unategemea na ukubwa wa maiti.
Namna ya Kuzika hatua kwa hatua.
a)Waingie watu kaburini kwa idadi ya witiri; 3, 5, 7, n.k.
b)Jeneza liwekwe upande wa kaburi itakapokuwa miguu ya maiti.
c)Maiti itolewe na kutanguliza kichwa kuelekea kaburini.
d)Wapokeaji kaburini watamuweka magotini mwao ili kufungua kamba kichwani, tumboni na miguuni. Pia watafunua shavu la kulia ili liguse ardhini (mchanga) atakapolazwa ndani ya mwana-ndani.
e)Maiti italazwa katika mwana-ndani kwa ubavu wa kulia na kuelekezwa Qibla. Wakati wa kuilaza ni sunnah kusema,
Kama ilivyosimuliwa na Ibn Umar (r.a) kuwa, Mtume (s.a.w) alipokuwa akizika alikuwa akisema:
“Bismillaah wabilahi wa’alaa millati Rasuulullaahi”
Tafsiri:
“Kwa jina la Allah na kwa uwezo wa Allah na kwa mujibu wa mwenendo wa Mtume wa Allah.” (Ahmad, Tirmidh, Ibn Majah).
f)Maiti ipindishwe miguuni na kichwani ili uso na miguu iweze kugusa kuta za mwana-ndani. Kifua, tumbo na sehemu za katikati zibinuliwe nyuma kidogo.
g)Maiti iwekewe mawe au udongo nyuma ya kichwa na miguu isibinuke. Pia ni sunnah kusoma aya za Qur’an (2:1-5) au (2:285-286).
h)Baada ya maiti kulazwa na kusomewa aya hizi, ifunikwe kwa ubao na kama kuna matundu ya kupitisha udongo pazibwe kwa majani.
i)Kabla kaburi halijafunikwa, vitupiwe viganja vitatu vya udongo, na kila tupo unasoma aya ya Qur’an (20:55).
1. Tupo la 1: “Min-haa khalaq-naakum” – Kutokana na hii (ardhi) tumekuumbeni.
2. Tupo la 2: “Wa fiyhaa nughiydukum” – Na humo (katika ardhi) tutakurudisheni.
3. Tupo la 3: “Wa min-haa nukhrjukum taaratan-ukhraa” – Na humo
(katika ardhi) tutakutoweni mara nyingine.
j)Kaburi lijazwe udongo mpaka lijae na kuinuliwa kiasi cha shiburi moja na kuwekewa alama miguuni na kichwani au kupanda miti mibichi.
- Ni vizuri kumiminia maji juu yake ili kuepusha vumbi kupeperushwa na upepo.
- Ni haramu kujengea kaburi kwa namna yeyote ile, kukaa juu yake, kuwasha taa
juu yake na kuielekea wakati wa kuswali.
‘Jabir (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amekataza kuyajengea makaburi au kuyajengea nyumba juu yake au kukaa juu yake’. (Muslim)
Abu Marsad Al-ghafariyyi ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:
“Msikae juu ya makaburi na wala msiswali kwa kuyaelekea.”
(Muslim)
- Baada ya kuzika Mtume (s.a.w) alikuwa akisimama na kusema:
“Muombeeni msamaha ndugu yenu na muombeeni awe
na kauli thabiti kwani sasa anaulizwa”
- Ni sunnah baada ya mazishi kuwapa mikono wafiwa na kuwausia subira
Rejea Qur’an (2:155-156).
- Pia haifai kusema (kusengenya) mabaya ya marehemu.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1044
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Simulizi za Hadithi Audio
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Kitau cha Fiqh
👉5 Madrasa kiganjani
👉6 Kitabu cha Afya
Swala za sunnah na faida zake
Soma Zaidi...
Historia ya adhana na Iqama na jinsi ya kuadhini.
Hadithi hii inakwenda kukufundisha historia fupi ya adhana pia utakwenda kujifunza jinsi ya kuadhini na kuqimu. Soma Zaidi...
Sifa za stara na mavasi katika uislamu
2. Soma Zaidi...
Haki za raia katika dola ya kiislamu
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Jinsi Uislamu Ulivyokomesha Biashara ya Utumwa wakati na baada ya Mtume Muhammad (s.a.w)
- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s. Soma Zaidi...
Baada ya kumzika maiti nini kifanyike kumsaidia marehemu
Tumesha mzika maiti sasa imebakia mali yae nyumbani, watoto, wake na menginyeo. Soma Zaidi...
Jinsi ya kutawadha kama aalivyotawadha Mtume Muhammad (s.a.w)
Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutawadha kama vile ambavyo alitawadha Mtume Soma Zaidi...
Sanda ya mtoto
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Yajuwe masharti ya udhu yaani yanayofanya udhu kukubalika
Posti hii itakufundisha masharti yanayohitajika kwa mwenye kutaka kutia udhu. Soma Zaidi...
Mambo yasiyoharibu Swaumu na Kufunguza mwenye kufunga
Soma Zaidi...
Siku ya idi al-fitir na namna ya kusherekea idi
Soma Zaidi...
Taratibu za kumuona mchumba katika uislamu
Hspa utajifunza taratibu za kuonana na mchumba katika uislamu. Soma Zaidi...