Namna ya kuoga josho, kujitwaharisha damu ya Hedhi, damu ya kuzaa Nifasi na Janaba
Masharti ya Kuoga
Masharti ya kuoga ni sawa tu na yale masharti ya udhu ila hapa yanahusu mwili mzima.
Nguzo za Kuoga
Kwanza, kutia nia moyoni kuwa unaoga kwa madhumuni ya kujitwaharisha, kutokana na janaba, hedhi, au nifasi. Mahali pa nia ni moyoni na wakati wa kunuiwa ni pale unapoanza kuosha kiungo cha kwanza.
Pili, kueneza maji mwili mzima. Ili kuhakikisha kuwa umeeneza maji mwili mzima ni vyema ufuate mafundisho ya Mtume (s.a.w). Mtume katika kuoga alikuwa akianza kwa kuosha sehemu za siri, kisha alikuwa akitia udhu, kisha alikuwa akijimiminia maji kichwani mara tatu, kisha alikuwa akieneza maji mwili mzima kwa kuanzia upande wa kulia na kumalizia upande wa kushoto, pote mara tatu tatu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Ni nini maana ya swala
Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu maana halisi ya ibada ya swala.
Soma Zaidi...Mambo muhimu ya kuzingatia katika kujenga uchumi wa kiislamu
Nazingatio muhimu katika uchumi unaofuata sheria za kiislamu.
Soma Zaidi...Taratibu za kumiliki hisa na mali ya shirika
Katika Uislamu kuwa na hisa kwenye mali inaruhusiwa. Hapa utajifunza taratibu za kumiliki hisa.
Soma Zaidi...