35.
35. Kumtegemea Mwenyezi Mungu (s.w)
Muislamu wa kweli daima huwa jasiri kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu katika kila hali. Ana yakini kuwa hapana lolote litakalomfika, baya au zuri, ila litakuwa linatoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) na ana yakini kuwa ulinzi wa maisha yake na mahitajio yake yote ya kimaisha yako mikononi mwa Mwenyezi Mungu (s.w). Mwenyezi Mungu (s.w) anatuamrisha tumtegemee Yeye tu katika aya zifuatazo:
Na tegemea kwa Yule aliye na uhai wa milele ambaye hatakufa โ. (25:58)
โ... Na kwa Mwenyezi Mungu wategemee Waislamu. Na tuna nini tusimtegemee Mwenyezi Mungu, na hali Ametuonyesha njia zetu. Na tutayavumilia maudhi yenu. Basi kw a Mw enyezi Mungu w ategemee wategemeaoโ. (14:11-1 2)
โ...Na anayemuogopa Mw enyezi Mungu, (Allah) humtengenezea njia ya kuokoka (na kila balaa); na humpa riziki kwa namna asiyoitazamia. Na anayem tegemea Mw enyezi Mungu yeye hum toshea. Kw a yakini Mw enyezi Mungu anatimiza kusudio lake. Hakika Mwenyezi Mungu amekwisha kiwekea kila kitu kipimo chakeโ. (65:2-3).
Kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa kila jambo na hasa wakati wa dhiki na kuhitajia msaada, huzidisha imani na ujasiri kwa waumini. Hebu turejee aya zifuatazo:
โWale ambao watu w aliwaambia: โWatu wamekukusanyikieni. Kwa hiyo waogopeniโ. Lakini (maneno hay o) yakawazid ishia imani wakasema Mwenyezi Mungu anatutosha. Naye ni Mlinzi bora kabisa. Basi w akarudi (vitani na neema za Mwenyezi Mungu na fadhila zake), hakuna ubaya uliowagusa; na wakafuata yanayomridhisha Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kuuโ. (3:173-174)
โNa Waislamu walipoyaona majeshi (ya makafiri) walisema, โHaya ndiyo aliyotuahidi Mw enyezi Mungu na Mtume wake. Mw enyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli,na (jambo hili) halikuwazidishia ila imani na utii. (33:22).
โHakika waumini wa kweli ni wale ambao anapotajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa hofu; na wanaposomewa Aya Zake huwazidishia imani na wakamtegema Mola wao tu basiโ. (8 : 2)
Hivyo Waislamu hatuna budi kumtegemea Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kila hali. Tukifanya hivyo imani yetu itazidi na tutakuwa na moyo wa ujasiri wa kutuwezesha kupambana na hali yoyote ngumu itakayotukabili kwa sababu tunayakini kuwa halitufikii lolote, baya au zuri, ila liko katika makadirio ya Mwenyezi Mungu (s.w). Ni vyema hapa tukumbushe kuwa kumtegemea Mwenyezi Mungu (s.w) ni kutekeleza wajibu wetu kwa juhudi na maarifa katika jambo lolote tunalolifanya kisha matokeo ya jitihada zetu tumuachie Mwenyezi Mungu (s.w). Hii hasa ndio maana ya kumtegemea Allah (s.w) kama tunavyojifunza.katika aya zifuatazo:
โNaam, wanaoelekeza nyuso zao kwa Mwenyezi Mungu na wakawa ni watendaji mema, basi wao watapata malipo yao kwa Mola wao, wala haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika. (2:112).
Na kwamba, mtu hatapata ila kwa yale anayoyafanya. (53:39).
Umeionaje Makala hii.. ?
Elimu imepewa kipaumbele kikubwa kwenye uislamu. Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu nafasi ya Elimu katika uislamu.
Soma Zaidi...Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu katika uislamu? Nini naana ya elimu ya muongizo. Je elimu ya mazingiravmaana yakeni nini. Ni upi utofauti wa elimu ya muongozo na elimu ya mazingira?
Soma Zaidi...Mwenyezi Mungu amekuwia radhi (amekusamehe).
Soma Zaidi...ุนููู ุฃูุจูู ููุฑูููุฑูุฉู ุฑูุถููู ุงูููู ุนููููู ุฃูููู ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู ููุงูู: "ู ููู ููุงูู ููุคูู ููู ุจูุงููููููู ููุงููููููู ู...
Soma Zaidi...