Nini maana ya Husda, na ni yapi madhara yake

Nini maana ya Husda, na ni yapi madhara yake

34.

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Nini maana ya Husda, na ni yapi madhara yake

34. Kuepuka Husuda



Husuda ni miongoni mwa magonjwa makubwa ya moyo. Mtu mwenye husuda anadonda la chuki moyoni mwake juu ya neema alizoneemeshwa mwingine na Mwenyezi Mungu (s.w). Kwa maana nyingine anachukia utaratibu wa Mwenyezi Mungu (s.w) aliouweka katika kugawanya neema zake kwa waja wake. Hasidi kutokana na chuki yake dhidi ya mja aliyeneemeshwa na Mwenyezi Mungu (s.w), huwa tayari kwa hali na mali kumdhuru mja huyo asiye na hatia yoyote. Ni kwa msingi huu Mwenyezi Mungu (s.w) anatufundisha kujikinga kwake na shari za viumbe vyake, akiwemo hasidi kama tunavyosoma katika Suratul-Falaq:


Sema: Ninajikinga na Mola wa Ulimwengu wote. Na shari ya alivyoviumba. Na shari ya giza la usiku liingiapo na shari ya wale wanaopulizia mafundoni na shari ya hasidi anapohusudu(1 13:1-5)



Husuda husababishwa na kutotosheka na kutoridhika na neema za Mwenyezi Mungu (s.w). Hasidi anataka kila neema aliyotunukiwa mwingine awe nayo yeye au mwingine abakie bila neema hiyo. Anataka awe juu ya mwingine na aonekane wa maana pekee katika jamii. Akihisi kuwa kuna yeyote aliyemzidi kwa cheo, utajiri, elimu, watoto,umaarufu, hupandwa na moto wa chuki moyoni mwake ambao humsukuma kufanya visa mbali mbali dhidi ya huyo anayemhisi kuwa amemzidi au yuko sawa n aye. Muislamu anatakiwa ajitakase na uovu huu wa husuda kwa kutosheka na kile alichonacho akijua kuwa kila neema aliyopewa mwanaadamu imekadiriwa na Mwenyezi Mungu (s.w). Na hapana yeyote mwenye uwezo wa kupunguza neema ya mtu aliyokadiriwa na Mola wake hata kwa kiasi cha chembe ndogo iliyoje na hakuna yeyote awezaye kumuongezea mtu neema kuliko vile alivyokadiriwa na Mwenyezi Mungu


(s.w).
Pia Muislamu wa kweli anajitahidi kujiepusha na husuda ili asije akaziunguza amali zake njema alizozitanguliza na akawa miongoni mwa watakaohasirika katika maisha ya akhera.



Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: โ€œKuweni waangalifu juu ya husuda, kwani husuda inaunguza amali njema za mtu kama moto unavyounguza kuni. (Abu Daud).



Husuda au wivu unaoruhusiwa ni ule unaofanywa kwa ajili ya kushindana katika kufanya mema. Wivu wa namna hii sio ule wa kuchukia kuwa kwa nini fulani ameneemeshwa bali ni ule unaomfanya mja ajitahidi zaidi kufanya mema kama anavyofanya au kumzidi mwingine. Mtume (s.a.w) ametufahamisha ni husuda ya namna gani inayoruhusiwa kwa Muislamu katika Hadithi ifuatayo:



Ibn Mas โ€™ud (r.a) am ehadithia kuw a Mtume w a Mw enyezi Mungu am esem a: Hapana husuda (inayoruhusiwa katika Uislamu) ila kwa watu wawili: โ€œMtu ambaye Mwenyezi Mungu (s.w) amempa mali na akampa uwezo wa kuitumia katika njia ya Mwenyezi Mungu na mtu ambaye Mwenyezi Mungu amempa elimu na hekima akawa anafundisha wengine pamoja na yeye mwenyewe kuingiza elimu hiyo katika vitendoโ€. (Bukhari na Muslim)




                   


Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Dini File: Download PDF Views 4634

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰3 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰4 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰5 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Matukio ya kihistoria katika masiku 10 ya Dhul Hija -Mfunguo tatu
Matukio ya kihistoria katika masiku 10 ya Dhul Hija -Mfunguo tatu

Haya ni matukio ya kihistoria yanayoamiika kutokea ndani ya masiku 10 ya Mfunguo tatu.

Soma Zaidi...
Neno la awali
Neno la awali

Asalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe, muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo.

Soma Zaidi...
Elimu
Elimu

Uwanja wa elimu na maarifa

Soma Zaidi...
quran na sayansi
quran na sayansi

2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZIUumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababumaalumu ili tipate mazingatio.

Soma Zaidi...
Kitabu Cha  Darsa za Funga
Kitabu Cha Darsa za Funga

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...
Elimu
Elimu

Uwanja wa elimu na maarifa

Soma Zaidi...